Nimepata uzoefu kuzuia wizi wa mtandaoni

Elezea ulivyotapeliwa ili tujuwe mbinu wanazotumia.
 
Elezea ulivyotapeliwa ili tujuwe mbinu wanazotumia.
Nahisi aibu hata kuelezea aise

Walinipigia wakijidai ni kampuni ya simu kwamba wanataka waniboreshee line yangu

Kuna namba wakawa wananitajia kumbe kule kufata maelekezo yao nawahamishia pesa bila kujua

Nilijionea hasira mwenyewe kwaku waendekeza na ni hela ambayo nilikua nikiitegemea
 
Naelewa mlivyo pigwa wewe na mleta mada hata kabla hamja sema. Ndo maana mesema hivyo

Kila siku mnaambiwa huduma kwa wateja ni 100 tu hamuelewi

Anyway vp uko pm kuna seat nije nipumnzkie kidogo bibie
 
Mkuu vipi huko Iran na Palestine?
 
Mkuu usitoe nywila hata ukiombwa na Waziri mkuu sembuse Meneja wa tawi la Benki.

Hawa wezi primitive ambao wanatuma random messages hao huwa wanawapata Wazee,Washamba,na Low IQ wenzao.
Kwa "wazee" unatudhalilisha bure, tuombe radhi.

Kuna "wazee" na wazee buana, haiingii akilini kuibiwa kizembe zembe namna hiyo eti kisa maelezo na maelekezo ya mtoa huduma za mitandao.

Kwanini nisimlambe authentications za kufa mtu hata kabla sijansikiliza?

Tena niwepesi kukimbia kama mbwa!

Wenye low Iq na wenye pupa za tamaa ndiyo wahanga wakubwa wa kwanza.

Mzee mjanja kama mimi utaanzia wapi kuntapeli mie?

Utapeli si kwa njia za mitandao pekee, hata kavu kavu mtu anakuja kwa njia ya kuazima, kukopa ama kukushawishi soko ili ukijaa tu, ndiyo iwe kantolee!

Sasa njia zote haramu za dhulmati ninazijua, hata aje vipi kwangu siyo rahisi hata kidogo.

Anayeniweza mie ni mwizi aliyejizatiti kwa kutumia nguvu lakini siyo tapeli.
 
Matapeli wanakuja na njia mpya kila siku kwa hiyo katika hilo hakuna uzoefu
 
Inawezekana vipi mtu mwenye akili zako timamu ukaibiwa kizembe zembe kwa kutumia simu?

Eti, mtu usiyemjua anakupigia simu na kukuuliza taarifa zako za siri na wewe unampatia. Hiyo ni akili au makamasi?

Hata kama mtu huyo unamfahamu bado ni uzembe kumpatia taarifa zako za siri ikiwepo password na taarifa zingine muhimu.

Mtu yeyote anayeibiwa kwa njia ya mtandao ni uzembe wake mwenyewe.
 
Tuko watu wapole na wema pia wanatupata sana.Mtu huwezi hata kutoa sauti ya ukali au unaona shida usijeukaambiwa huna ushirikiano.
 
Matapeli wanakuja na njia mpya kila siku kwa hiyo katika hilo hakuna uzoefu
Baada ya kutulaumu tunaoibiwa lawama kubwa ziwaendee mashirika ya simu na vitengo vya polisi vya wizi wa mtandao. Inatakiwa kuwe na update kila baada ya muda kutahadharisha njia mpya.Sio kila siku maneno ni hayo hayo usitoe namba yako ya siri kwa mtu usiyemjua.Haitoshi hiyo. Unajua kwa nini anti virus za mtandao kila siku ikifika jioni wanatengeneza kinga za hali ya juu baada kuona wapi virus wamepenya kutwa nzima.
Kwanza kauli ya shirika la simu Inabidi uende polisi.Sisi hapo hatutoweza kukusaidia. Ni kauli za kutoa ushirikiano kwa wezi kabla ya kumsaidia aliyeibiwa
 
Kwenye mitandao ya benki
Matapeli wanakuja na njia mpya kila siku kwa hiyo katika hilo hakuna uzoefu
Mashirika ya simu yachukue uzoefu wa huduma za mabenki.Kadi ya nida ya mteja ikitumika kusajili laini nyengine kwenye mtandao wao papo hapo itoke ujumbe kwenda kwa mwenye kadi hiyo.Mwenyewe atajuwa iwapo ni yeye au ni mwizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…