Nimependa jinsi kijiji cha Namalembo walivyopanga mji wao pamoja na kutokuwa na rasimali fedha na wasomi kama mijini

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kijiji cha Namalembo kinapatikana kata ya Msikisi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Shughuli kubwa ya kiuchumi kwenye kijiji cha Namalembo ni Kilimo huku Mahindi na ufuta ikiwa ni mazao yanayolimwa zaidi moja likiwa la chakula na lingine biashara.


Kijiji cha Namalembo(Picha kwa msaada wa Google Earth)​

Kijiji cha Namalembo bado kinakua na eneo la mji uliojengwa si kubwa na wengi wanafahamiana, ukienda mgeni wanajua huyu si wa hapa. Kijiji hiki kina shule moja pekee ambayo ni shule ya msingi Namalembo na zahanati ya kijiji.

Taasisi nyingine iliyopo ni mamlaka ya maji yenye ofisi na tenki kubwa la maji la kuhudumia kijiji hiki japo wananchi huwa hawatumii maji hayo mpaka wakati wa kiangazi kwa madai ya gharama, wanachota maji kwenye visima vinavyotuamisha maji kipindi cha mvua.


Pamoja na kijiji kutokuwa na taasisi kubwa ya elimu zaidi ya shule ya msingi na wasomi wa kuhesabu pia ukata wa rasilimali fedha, wamefanikiwa kupanga mji wao. Ukinunua ardhi katika kijiji hiki kwa mtu lazima Serikali ya kijiji ifike kabla mauziano haya hayajatamatika.

Sera ya kijiji ni kila ekari inabeba kaya sita za makazi(wastani wa sqm 1600 kila kaya), kaya tatu zinaangalia juu na kaya tatu zinaangalia chini na kunakuwa na barabara kubwa na pana upande wa juu na chini ambazo kila kaya itakuwa inatazamana nayo kwa urefu. Kwa upana kila baada ya nyumba tatu(ekari moja) inakatisha barabara ndogo ya mtaa ambazo baadhi ya sehemu hazionekani sana kutokana na kutopitiwa mara kwa mara lakini zinajulikana kama njia rasmi, wengi hupita barabara kubwa na barabara za mitaa zilizozoeleka.

Ni mji ambao utapendeza na mpango wake kuonekana zaidi siku zijazo hata kurekebisha mji huu ni rahisi ikihitajika kwasababu angalau kuna mipangilio msingi. Mashamba wameyatenga na mji, yapo ukiumaliza mji.

Pamoja na mipango yote barabara zake ni mbovu kupitiliza, jambo ambalo Serikali inaweza kuwasaidia angalau kuzichonga.

Kwanini sera hii ya wakazi hawa isifatwe mijini, hasa nje ya miji mikubwa kama Dar, Pwani na mingineyo? Watu wanajenga miji mipya bila hata chochoro za kupita na baadhi ya viwanja kutokuwa na njia kabisa baada ya kila jirani kubana.

Pia, Soma=>Mipango miji Tanzania
 
Wakaze hapo, pia wasaidiwe kuwa na Maeneo rasmi ya Kijamii: Masoko, Ofisi za Serikali, Zahanatu, Maeneo ya Michezo, Kituo cha basi nk.Aidha wakiweza kila mwanakijiji apewe Hati ya Kimila.

Shida huja watu wakiongezeka na kisha wenyeji wanaanza kuuza Ardhi vikawa vipande Vidogo ndipo zile Njia za Kupita huanza kuvurugika ikawa kama baadhi ya mitaa ya Majiji.
 
Eneo la soko wanalo pamoja na kwamba walichelewa kuliweka kwenye mipango ya mji mapema, kuna eneo katikati ya mji wao lilikuwa la timu ya mpira lililojumuisha uwanja wa mpira wa miguu. Walikubaliana na timu husika na kuligeuza kuwa eneo la soko, eneo hili limezungukwa na fremu za maduka zilizopanga.

Katikati ya eneo hili wameacha eneo kubwa la wazi ambalo litajengwa soko siku zijazo, kwa sasa eneo hilo wamewapa mama ntilie kuendeshea biashara zao lakini hawaruhusi kujenga majengo la kudumu.
 
Umeharibu kabisa sasa, wazee wa mipangomiji watatua na ramani zao uchwara, watajidai kurekebisha matumizi na kuanza kuuza viwanja, watakatakata kama viazi vya chips viwe vingi.
 
Hakuna waharibifu wa mipango miji kama watu wa serikali za mitaa... wao akija mtu na millioni wanapiga hesabu ya ganji wala hawajali kiwanja kinachouzwa kikoje.. yaani ni njaa njaa njaa kwa kwenda mbele.
Mipango miji na kausha damu nihali kadhalika
 
Yaani mipango miji hapa Tanzania ni kizungkuti aisee. Miji yote ni uwanja wa fujo. Mimi huwa najiuliza hizo DC huwa wanafanya nini huku kwenye miji midogo inayokuwa kwa kasi?

Angalia pale mafinga, mji unakuwa ila sasa, shaghala bhaghala. Ona pale Iringa hapo stand ya zamani pogolo wamejenga hovyo. Yaani aaaa hata mitaa hakuna vurugu tu. Ona Makambako mji unajiendea tu, hamna mipango yoyote mji mbovu kama nini. Yaani tufike mahali hawa watendaji wawe ndio wasimamizi wa miji hii maana mmm. Angalia Mbeya napo hovyo kabisa.
 
Kasulu Mjini pia wamejitahidi mitaa imepangika hadi vijijini wamevipanga vizuri sema pale Kijiji cha Makele wamepanga French style viwanja vya pembe tatu
 
Nimependa size ya Viwanja na mpangilio kwa kila heka. Safi sana.
 
Toka huko weweeee..
Huwezi toboa ukiwa huko
Tatizo lako la akili linazidi kukua.Hoja ya mleta mada ni mipango miji wewe unawaza kutoboa.Huko Dar es salaam mmetoboa wote?au mnasubiri zali la mentali.Kwa akili hizi CCM haiwezi Toka madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…