Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Kijiji cha Namalembo kinapatikana kata ya Msikisi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Shughuli kubwa ya kiuchumi kwenye kijiji cha Namalembo ni Kilimo huku Mahindi na ufuta ikiwa ni mazao yanayolimwa zaidi moja likiwa la chakula na lingine biashara.
Kijiji cha Namalembo(Picha kwa msaada wa Google Earth)
Kijiji cha Namalembo bado kinakua na eneo la mji uliojengwa si kubwa na wengi wanafahamiana, ukienda mgeni wanajua huyu si wa hapa. Kijiji hiki kina shule moja pekee ambayo ni shule ya msingi Namalembo na zahanati ya kijiji.
Taasisi nyingine iliyopo ni mamlaka ya maji yenye ofisi na tenki kubwa la maji la kuhudumia kijiji hiki japo wananchi huwa hawatumii maji hayo mpaka wakati wa kiangazi kwa madai ya gharama, wanachota maji kwenye visima vinavyotuamisha maji kipindi cha mvua.
Pamoja na kijiji kutokuwa na taasisi kubwa ya elimu zaidi ya shule ya msingi na wasomi wa kuhesabu pia ukata wa rasilimali fedha, wamefanikiwa kupanga mji wao. Ukinunua ardhi katika kijiji hiki kwa mtu lazima Serikali ya kijiji ifike kabla mauziano haya hayajatamatika.
Sera ya kijiji ni kila ekari inabeba kaya sita za makazi(wastani wa sqm 1600 kila kaya), kaya tatu zinaangalia juu na kaya tatu zinaangalia chini na kunakuwa na barabara kubwa na pana upande wa juu na chini ambazo kila kaya itakuwa inatazamana nayo kwa urefu. Kwa upana kila baada ya nyumba tatu(ekari moja) inakatisha barabara ndogo ya mtaa ambazo baadhi ya sehemu hazionekani sana kutokana na kutopitiwa mara kwa mara lakini zinajulikana kama njia rasmi, wengi hupita barabara kubwa na barabara za mitaa zilizozoeleka.
Ni mji ambao utapendeza na mpango wake kuonekana zaidi siku zijazo hata kurekebisha mji huu ni rahisi ikihitajika kwasababu angalau kuna mipangilio msingi. Mashamba wameyatenga na mji, yapo ukiumaliza mji.
Pamoja na mipango yote barabara zake ni mbovu kupitiliza, jambo ambalo Serikali inaweza kuwasaidia angalau kuzichonga.
Kwanini sera hii ya wakazi hawa isifatwe mijini, hasa nje ya miji mikubwa kama Dar, Pwani na mingineyo? Watu wanajenga miji mipya bila hata chochoro za kupita na baadhi ya viwanja kutokuwa na njia kabisa baada ya kila jirani kubana.
Pia, Soma=>Mipango miji Tanzania