Nimependa jinsi kijiji cha Namalembo walivyopanga mji wao pamoja na kutokuwa na rasimali fedha na wasomi kama mijini

Umeharibu kabisa sasa, wazee wa mipangomiji watatua na ramani zao uchwara, watajidai kurekebisha matumizi na kuanza kuuza viwanja, watakatakata kama viazi vya chips viwe vingi.
Hawa jamaa wa mipango miji nyambaff kabisa sijui hata huko vyuoni huwa wanafundishana nini. wananzengo wakitulia wenyewe wanaweza kufanya la maana sana ila sio hawa jamaa.
 
Kasulu wamepanga mji wao vizuri. Huku Songwe kuna kijiji kinaitwa Ifumbo. Kimepangwa vizuri sana. Watu hawana shida kupanga miji, shida ni serikali na wanaosimamia mipango miji. Hakuna anayejali iwapo miji imepangika, pumbavu kabisa.
 

Makambako kwa kupanga mji wamejitahidi Kuna mitaa mitatu ndo ilikuwa ovyo wamesharekebisha na eneo kubwa kwa Sasa makambako limepimwa ni vizur kulijua vizuri eneo sio kubashiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…