Wivu na muonea nani.....?Kwa hiyo wote tuwe wapigaji....... mtaiuza nchi hii, halafu mtapangiwa cha kufanya.
Unaakili kama za wauza ngada wa Mexico, kwa kuwachekea wauza unga ,matokeo yake vijana wengi wanadream ya kujiunga na Cartel na nchi ishakuwa ya wauza unga,serikali ishapoteza control kwani kila kijana anatafuta kazi ya kulima,kusafirisha na kuuza unga. Nchi hii tunawachekea mafisadi ndio maana vijana wengi wanadream za kupata nafasi kwenye mashirika makubwa ili wapige hela na si kuyaendeleza, halafu wanaopiga hela wanatafuta sana kuonewa huruma na jamii kwa misaada yao,kama wauza ngada wa Mexico.
Uzuri sina akili ya upigaji kwani nina alternative kama tano za kuingiza hela bila kupiga. Ninacho ongea hapa ni kwa ajili ya maendeleo ya Tz na vizazi vijavyo.