Nimepewa dawa zilizoexpire( kuisha muda wake) katika Zahanati ya Serikali!!!.

Nimepewa dawa zilizoexpire( kuisha muda wake) katika Zahanati ya Serikali!!!.

Sisi wadau wa afya waandamizi seniorz tunajua tuna jua dawa Ina expired date mfano January so kuisha nguvu ni miezi mitatu after expired.

Kuna mengi nayo yajua ngoja ninyanaze nisije kua Kama tundu lissu ☺️☺️
Weee!! Mimi hata ikiexpire lisaa limoja sintoitumia. Ila Hawa watu wamenifungua macho
 
Hii Zahanati ndo kawaida yake kuuza dawa zilizo expire naikumbuka sana mana hata mimi waliniuzia dawa zime expire
Dr mambo jambo kasema wanafanya FEFO, sijui fefo ndo kitu gani ila wawe wanasema basi kuepusha taharuki.
 
Expiry date haimaanishi dawa inakua sumu hapohapo

Ni muda ambao mzalishaji anakua hana tena guarantee ya 100% ya ubora na ufanisi wa dawa zake
Ahaa, ndo nimefahamu sasa. Shukrani.
 
Tarehe 04 / 01 / 2025 nilienda Zahanati flani hapa mjini, ni ya Serikali baada ya kuwa sijiskii vizuri, nikapewa dawa kadhaa na panadol.

Leo jioni kichwa kikawa kinauma sana, nikasema nimeze Panadol ambazo nilibakiza nilizopewa Zahanati.

Binafsi siwezi kumeza Panadol Huwa nazitafuna tu, sasa wakati natafuna nishushie na maji nikawa natizama kasha la Panadol, jicho likapiga kwenye Manufacturer na expire ndo naona imeandikwa E... 1 / 2025. Sikuamini nikarudia kuangalia tena labda nimeona vibaya , Kila nikiangalia nakuta ni hvyo hvyo.

Ikabidi ninunue maziwa faster nikanywa. Kumbe ndomna homa haishuki, kichwa hakipoi tangu nilipotoka hospital nipo vile vile kma vile sijaenda, kumbe nimepewa dawa zimeexpire.

Inabidi nichukue hatua gani nyingne kuondoa hiyo sumu mbali na maziwa , maana nimepanga ninywe maziwa siku 3 mfululizo, kama Kuna hatua nyingne nisaidieni.

Pia tuwe makini kuangalia expire date hata katika hospital za Serikali, mimi nilikuwa naangalia nikinunua dawa maduka binafsi , Serikalini huwaga siangalii kwakua naamini Serikali haiwezi kudhuru wananchi wake ila kumbe nilikuwa najidanganya, hata huku watu sio waaminifu.

Naenda kutafuta vikasha vile vingine nione, jpo vipo kwenye taka ila siwezi kuwa na amani mpka nisibitishe expire date zake pia.
Weka picha tuone hio expiry date
 
ukiondoa kutokunywa maziwa pia expire huwaga huangalii pia
Siangaliagi kwa hospital za Serikali ila binafsi Huwa naangalia lazima. Baada ya hili tukio, itabidi nazenyewe niwe nakagua.

Maziwa nakunywa ila sio Kila siku.
 
Siangaliagi kwa hospital za Serikali ila binafsi Huwa naangalia lazima. Baada ya hili tukio, itabidi nazenyewe niwe nakagua.

Maziwa nakunywa ila sio Kila siku.
sio dawa tu mkuu chochote kile kukagua expire ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom