Nimepewa likizo ya bila malipo kisa Corona

Nimepewa likizo ya bila malipo kisa Corona

selukeng'e

Member
Joined
May 11, 2015
Posts
10
Reaction score
24
Kutokana na hill janga la korona nimepewa likizo ya bila malipo. Mimi ni mwalimu katika shule moja private, likizo hii tumepewa wafanyakazi wote.

Ninapitia wakati mgumu sana ninapenda kuwashauri vijana ambao bado hamjaoa nivema mkaoa wadada wafanyakazi pia jaribu kuwa na biashara pembeni.

Wanajamii ninaomba msaada kama tunawezachukua hatua za kisheria kwa hili sababu hatukupewa hata nauli ama tupambane na halo zetu
 
Kutokana na hill janga la korona nimepewa likizo ya bila malipo. Mimi ni mwalimu katika shule moja private, likizo hii tumepewa wafanyakazi wote. Ninapitia wakati mgumu sana ninapenda kuwashauri vijana ambao bado hamjaoa nivema mkaoa wadada wafanyakazi pia jaribu kuwa na biashara pembeni. Wanajamii ninaomba msaada kama tunawezachukua hatua za kisheria kwa hili sababu hatukupewa hata nauli ama tupambane na halo zetu
Kama ni kweli sheria ya kazi haisemi hivyo.
 
Kutokana na hill janga la korona nimepewa likizo ya bila malipo. Mimi ni mwalimu katika shule moja private, likizo hii tumepewa wafanyakazi wote.

Ninapitia wakati mgumu sana ninapenda kuwashauri vijana ambao bado hamjaoa nivema mkaoa wadada wafanyakazi pia jaribu kuwa na biashara pembeni.

Wanajamii ninaomba msaada kama tunawezachukua hatua za kisheria kwa hili sababu hatukupewa hata nauli ama tupambane na halo zetu

Tatizo lenu mkipata kazi hamsomi mikataba yenu ya kazi vizur mnaishia tu kukimbilia kuisign
Kipengele cha force majeure kinasemaje kwemye mkataba wako wa kazi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu..

Ndio maana kichwa changu huwa kinaniambia "we kobe hakikisha unakuwa na jiwe la pembeni!"
Kumbe kichwa changu kipo sahihi..
Ktk maisha ni lazima tuwe na option zaidi ya moja ili kujiongezea usalama zaidi.
 
Tatizo lenu mkipata kazi hamsomi mikataba yenu ya kazi vizur mnaishia tu kukimbilia kuisign
Kipengele cha force majeure kinasemaje kwemye mkataba wako wa kazi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sidhani Mimi niko huku kwenye nchi ambazo corona wanashambulia sana nafanya kazi kampuni moja ya kimataifa mwezi hatuingii kazini sasa lakini kila kitu tunalipwa Kama kawaida. Huo ni uonevu
 
Unapaswa kulipwa basic salary kwa kipindi chote utakacho kuwa likizo
Jr[emoji769]
Mkuu Mleta mada kasema ni Shule binafsi, na mitaji yao ni sisi wazazi tunapopeleka watoto wetu.
sasa tumeambiwa wakae nyumbani na tumerudishiwa bila hata ya nauli kila mtu kafuata mtoto wake Bwenini baada ya Tangazo la March 17
Wakurugenzi / Wamiliki pesa wameshajengea majengo na magari ya kifahari, Bima wala Mifuko ya kijamii hawakuwawekea kwa hiyo wao ni tofauti na wale wa Magufuli kwani ajira zao ni za form 6 au Gaduate
Ajira zao nyingi hazotambuliki, Mkurugenzi akifilisika au akikosa kuafaulisha basi na wao
@Selukeng'e vumilia Wazazi tunawatunza watoto wetu majumbani mpaka gonjwa liishe
 
Pole sana mkuu.Mnaosema plan mbili zaidi sawa.Unaweza ukawa na palan A mpaka plan Z ila siyo kwamba plan A iharibiwe na mpuuzi/wapuuzi bila mpangilio.Maumivu ya kunyimwa mshahara yasikie tu.Cheki vijiakiba ujipumzishe nyumban kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ilitakiwa kusaidia sector binafsi kipindi hiki kwa kuzipa subsidies na misamaha ya kodi ili ziweze kujiendesha.

Lakini TZ ni hola hola hamna kitu.

October ballot box, change!!
 
Kutokana na hill janga la korona nimepewa likizo ya bila malipo. Mimi ni mwalimu katika shule moja private, likizo hii tumepewa wafanyakazi wote.

Ninapitia wakati mgumu sana ninapenda kuwashauri vijana ambao bado hamjaoa nivema mkaoa wadada wafanyakazi pia jaribu kuwa na biashara pembeni.

Wanajamii ninaomba msaada kama tunawezachukua hatua za kisheria kwa hili sababu hatukupewa hata nauli ama tupambane na halo zetu
Pole sana mkuu sector ya ualimu hasa private wamiliki wa shule wamefanya uhuni sana,kama una mkataba na haujaisha mpeleke front(UBAONI) mwajiri.
 
Back
Top Bottom