Nimepewa likizo ya bila malipo kisa Corona

Nimepewa likizo ya bila malipo kisa Corona

mkuu, utajiaribia tu huko mbeleni, ugonjwa unapita huu, vumilia tu, Kisha utarud job. ukifanya tofauti utakosa yote...cha muhimu weka chaki pembeni tafuta njia nyingine......wazaz wamegoma kulipa ADA, je utapataj mshahara??? wamiliki wanamadeni mpaka kwenye p.u.m.b.u. we ona hivyo hivyo tu mtu akiitwa boss, moyoni anatamani awe mwajiriwa asiwe boss...kama umewahi kumiliki hata vibarua tu utanielewa nilichokuwa nakisemaa........
 
Huwa nawaza mwanaume ambae ni bread winner wa familia ikitokea anasimamishwa kazi,kufukuzwa au kama hivi likizo bila malipo huku hana njia nyingine ya kumuingizia kipato, na haya maisha yetu ukute hata akiba hana[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Sijuuui tu yaani, pole sana mkuu.

Ila hizi shule haziwatendei haki, kipindi chote mmewatengenezea faida ila wanaact kama hili janga mmelisababisha nyie!!! Thats not fair.
 
mkuu pole sana, wale wa kukejeli waendelee kukejeli.
 
Huwa nawaza mwanaume ambae ni bread winner wa familia ikitokea anasimamishwa kazi,kufukuzwa au kama hivi likizo bila malipo huku hana njia nyingine ya kumuingizia kipato, na haya maisha yetu ukute hata akiba hana[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Sijuuui tu yaani, pole sana mkuu.

Ila hizi shule haziwatendei haki, kipindi chote mmewatengenezea faida ila wanaact kama hili janga mmelisababisha nyie!!! Thats not fair.
Yaani ni hatari sana kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na hill janga la korona nimepewa likizo ya bila malipo. Mimi ni mwalimu katika shule moja private, likizo hii tumepewa wafanyakazi wote.

Ninapitia wakati mgumu sana ninapenda kuwashauri vijana ambao bado hamjaoa nivema mkaoa wadada wafanyakazi pia jaribu kuwa na biashara pembeni.

Wanajamii ninaomba msaada kama tunawezachukua hatua za kisheria kwa hili sababu hatukupewa hata nauli ama tupambane na halo zetu
Pambana na hali yako bro
 
Mkuu sidhani Mimi niko huku kwenye nchi ambazo corona wanashambulia sana nafanya kazi kampuni moja ya kimataifa mwezi hatuingii kazini sasa lakini kila kitu tunalipwa Kama kawaida. Huo ni uonevu

Mkuu mikataba inatofautina. Hakuna uonevu hapo yeye ni kwamba mkataba aliousign ndo unambana nina uhakika boss wake alijiondoa liability yote kipindi cha majanga kwenye huo mkataba.
Kama sio hivyo auweke hapa mkataba wake wa kazi tuusome wote tuuchambue. Tatizo bongo pa kifara sana vijana wengi wapo mtaani maisha magumubtukipata gepu pa kuhemea huna jinsi mkataba wewe una sign tu na option mengine tutajua mbele kwa mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu ,sisi wa utalii ndio hamna kitu kabisa,bora ninyi shule zikifungua mambo yataendelea vizuri
 
  • Thanks
Reactions: amu
Dunia imeendelea kupoteza mvuto wake.

Cha kufanya na cha msingi sana ni kutengeneza mahusiano mazuri na Mungu aliyetuumba ili kama ni mapenzi yake turejee kwake, maana kwa vyovyote vile kule kwake ni pazuri kuliko hapa duniani.

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo basic anaitoa wapi huyo mwenye shule? Wazazi hawataki kulipa ada!
Hapa tutakuwa tunawapa kiburi wamiliki wa hizi shule. Kwa kawaida wazazi hulipa ada kuanzia nusu muhula (miezi sita) inamaana mpaka sasa ada iliyolipwa kwa muhula huu lazima iwe ndani ya bajeti. Labda kama mishahara itaanza kusuasua mwezi july hapo ndipo kidogo waajiri watahalalisha umafia wao na ukatili kwa wafanyakazi wao. Kinachowapa jeuri ni kuwa wafanyakazi watanyenyekea ili shule zikifunguliwa wasifukuzwe kazi.
 
Pole mkuu..

Ndio maana kichwa changu huwa kinaniambia "we kobe hakikisha unakuwa na jiwe la pembeni!"
Kumbe kichwa changu kipo sahihi..
Ktk maisha ni lazima tuwe na option zaidi ya moja ili kujiongezea usalama zaidi.
Mkuu kuwa na more than one option ni jambo jema mno,tena hizo option ziwe category mbali mbali
mimi nimewekeza sehemu tatu tofati tofauti lakini zikiwa ni za idara moja,nilifanya hivyo baada ya kuona zinanilipa haraka na pesa yangu inarudi ila hii Covid 19 imezipiga mtama mapema sana tena mwanzoni gonjwa lilipotua Tz,nina siku 40+ nakula hakiba tu,hakuna ninachoingiza,mambo yangu yamevurugika vibaya mno.
Siku harakati zangu zikirudi barabarani nitakuwa na vitega uchumi kila idara hata kama zingine zitakuwa zinaleta kiapato kidogo ni afadhari mno kuliko kukaa bila kuingiza chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa nawaza mwanaume ambae ni bread winner wa familia ikitokea anasimamishwa kazi,kufukuzwa au kama hivi likizo bila malipo huku hana njia nyingine ya kumuingizia kipato, na haya maisha yetu ukute hata akiba hana[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Sijuuui tu yaani, pole sana mkuu.

Bread winner akikwama ni muda wa mke kuonesha umuhimu wake, kwa heshima lakini sio masimango na kuuza mechi.... ndo muda huo utajua kama una mke au kimeo.
 
Bread winner akikwama ni muda wa mke kuonesha umuhimu wake, kwa heshima lakini sio masimango na kuuza mechi.... ndo muda huo utajua kama una mke au kimeo.
Unajua hapo wote mnakuwa stressed eeh!! Kumbuka mke ni mama wa nyumbani. Sasa issue inakuwa nani yuko tayari kuchukulia stress za mwenzie ili hali nawe una stress. Shida inaanzia hapo. Hapo ni kuomba hekima ya kimbingu tu iwasaidie mvuke salama.
 
Hapa tutakuwa tunawapa kiburi wamiliki wa hizi shule. Kwa kawaida wazazi hulipa ada kuanzia nusu muhula (miezi sita) inamaana mpaka sasa ada iliyolipwa kwa muhula huu lazima iwe ndani ya bajeti. Labda kama mishahara itaanza kusuasua mwezi july hapo ndipo kidogo waajiri watahalalisha umafia wao na ukatili kwa wafanyakazi wao. Kinachowapa jeuri ni kuwa wafanyakazi watanyenyekea ili shule zikifunguliwa wasifukuzwe kazi.
Wazazi tunalipa ada kila miezi 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom