Nimepewa Taarifa na washikaji zangu kijiweni kwamba kuna watu wananitafuta

Nimepewa Taarifa na washikaji zangu kijiweni kwamba kuna watu wananitafuta

Hii Nchi kuna magenge ya uhalifu Yana abuse mamlaka na kufanya wajisikiavyo ,jeshi la polisi ,TISS na vyombo vingine vya dola vimekuwa vikitumika kufanya shughuli za utekaji na mauaji ya raia kwa muda mrefu , hii kitu ni mbaya sana .
Na hamna aliye salama ,kuishi nchi kama hii ni laana kabisa ,muda wowote maisha yako yanapotezwa tu
 
Watz wako kama mazezeta tu yanakesha na mada za simba na Yanga wakati kuna issue critical kama hii .
Watu wanapotezwa tu kama kumbikumbi
 
Mkuu sijawahi KUTEMBEA na mke wa mtu na sidhani kama nitakuja KUTEMBEA nae!

Ni Machokoraa tu Hawa wanaoteka Teka watu hovyo!
Huyo atakuwa @GENTAManataka akufanyizie. We si ulitamba humu JF kuwa Genta ni boya tu nahana uwezo wa kukifanya lolote? Anakuwimda sasa.

Pole and watch your step. Hali ni mbaya na huu upepo sijui umetokea wapi. Sasa watanzania tunakuwa kama digidigi. Kila saa tunakuwa makini kwani mafisi yanatuwinda bila sababu. Mungu atuepushie mbali hii Roho Mbaya.
 
SNITCH, anaweza kuwa wa hapohapo kijiweni....So trust nobody....
 
Dawa ni kuacha ukondoo na kumiliki silaha za moto tu .
Wakijipendekeza hao malaya ni kuwafanya alichowafanya Tajiri Zacharia
Hahahaaa umenikumbusha kitu Zacharia aliwatengua viuno vibaya mno alafu walivyo wajinga wakikutana na mazito wanaenda kulia lia kuwa walikua kwenye kazi zao za kawaida wakashambuliwa kumbe Zacharia alikua na habari zote
 
we endelea na ubishi wako mwenzako nilibambikiwa kesi ya bangi sababu nilimtukana polisi aliekua anataka rushwa kwa lazima
nilienda kutambika mbuzi mmoja na kuku
yule afande alianza kutambaa kama kiwete wamefika hadi nyumbani kwangu lakini wapi nadhani alishajiua nyau yule yani alipwe kwa kodi zangu na bado alete uhuni nilipita naye moja kwa moja.
Hahaha

Ova
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!


Nimepewa Taarifa na washikaji zangu hapo Dar es salaam ya kwamba kuna watu (Mwanamke 1 & Wanaume 2) wananitafuta!

Nikiwa Niko hapa Mbeya takribani miezi miwili Sasa nikiwa kwenye shughuli zangu nyingine,nilipigiwa simu na jamaa zangu wawili Kwa nyakati tofauti na wakanialifu ya kwamba kuna watu wamekuwa wakienda pale kijiweni kunitafuta na wanadai ya kwamba nimewahi kukopa pesa kwenye taasisi Yao (Jina kapuni) na nimeshindwa kulipa Deni Kwa wakati na kila wakinipigia simu sipokei na wakati mwingine nimewapigia Block!

Mbaya zaidi hao watu wananifahamu Kwa Majina yangu halisi kama ambavyo kijiweni nafahamika kwenye daftari la Umoja wa madereva bodaboda/Bajaji hapo Bunju!

Binafsi sijawahi kukopa pesa kwenye taasisi yeyote Ile hapa nchini na kwasasa sihitaji mkopo wa aina yeyote,Pili,Hakuna mtu yeyote au taasisi anayenidai pesa au kitu chochote!
Kutokana na matukio yanayoendelea hapa nchini,washikaji zangu walikuwa na mashaka na hao watu na wao wamenitaarifu ya kwamba hao watu kimionekano ni watu eidha kutoka Jeshi la Polisi au idara nyingine ya Kiusalama hapa nchini,kwasababu naarifiwa maswali ya dodoso waliyokuwa wakiulizwa siyo ya kawaida!

Hapo kijiweni Kuna jamaa alitoweka kwenye mazingira ya kutatanisha tangu mwezi wa 5 hadi Leo hii haijulikani Yuko wapi!

Juzi moja Kuna jamaa alinipigia simu huku akinichangamkia kishenzi akitaka nikamchukue maeneo ya IPTL nimpeleke Mbezi,Binafsi nikajua anaweza akawa miongoni mwa abiria wangu,kwakuwa hakujua kama sipo Dar es salaam nilimwambia "Mimi Niko mbali kidogo boss,ngoja nimshutue mshikaji wangu aje akuchukue hapo,nampatia namba yako"

Jamaa "Mimi nakutaka wewe kaka maana huwa uko makini sana barabarani"

Mimi "Sawa boss lakini Niko mbali (Sikutaka kumwambia nilipo) sidhani kama nitawahi ndiyo maana nakuomba nikuitie mtu ninaye muamini atakupeleka na utafika salama"

Jamaa "Hapana kaka,wewe kama ni pesa nitakuongezea Mimi nakutaka wewe"

Hapo ndipo nilipopata mashaka kwasababu abiria wa bodaboda tunawafahamu na siyo rahisi kihivyo,pili,Jamaa bado aliendelea kunipigia Simu japo nilimwambia nimetoka lakini hakukata tamaa!,baada ya kuona huo Usumbufu sikupokea hadi Leo.

Sasa,nafahamu mko humu na mnanisoma vizuri tu,Niwaambie mambo yafuatayo nyie Vishoka!

Mimi naitwa UMUGHAKA wengine hupenda kuniita UMUGHAKA WA BHAGHAKA

Dar es salaam narejea Mwezi Ujao,na kama kawaida Dar es salaam Sina shughuli nyingine zaidi ya Udereva wa Bodaboda!

Siku mtakapokuja kijiweni eidha ni kunikamata au Kwa jambo lolote lile baya,Njoeni kabisa mkiwa mmetubu na kuziaga familia zenu maana ni eidha mfe nyie au nife Mimi.

Narudia tena

Siku mtakapokuja kijiweni hakikisheni mmetubu na kuziaga familia zenu maana ni eidha mfe nyinyi au nife Mimi.

NATAKA NIFANYE KITUKO AMBACHO NAAMINI DUNIA NZIMA ITAGEUZA MACHO YOTE KUITAZAMA TANZANIA.


Mimi ndiye
UMUGHAKA
Bangi mbaya sana aisee 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ukiona rafiki wa zamani, ndugu mliopotezana muda mrefu au kidemu chako cha zamani wanakutafuta ghafla na kwa nguvu kimbia wala usigeuke nyuma.​
Nilitafitwa mwanka 2020 kupitia kwa jamaa yangu wa kijiweni nikiwa nje ya dar baadae nikapigiwa simu amekufa kwao iringa
 
Unajipa wasiwasi usio na maana, kama ni vyombo vya sheria au idara ya usalama ingekua inakutafuta na namba yako wanayo Wala hata wasingehangaika kuja kijiweni ungedakwa huko huko mbeya kama kuku
Sio rahis kama unavyodhan kuna jamaangu kasumbuana na maafande mwaka wa 3 huu hatumiag smart phone na line anavunja anaweka nyingine, Tanzania bado sana kama watu wanakutafuta kimya kimya ila kama wanaweka public announcement ni rahis kukupata, maaskari wengi ni 4m 4 failure kwahiyo hata approach za kuwapata watu wao ni zakizaman sana na zakitoto..
 
Back
Top Bottom