Chief Kumbyambya
JF-Expert Member
- Jun 16, 2022
- 719
- 2,408
Ebwanaeeeeeeee, za leooo.
Moja Kwa moja kwenye mada.... Hivi nyie wanawake mkoje.... Hasa mnaoshinda nyumbani wakati sisi tupo kutafuta na kuvuja majaisho huko mtaani.
Iko hivi... Mimi huwa sipendi kununua vitu kidogo kidogo maana naona inakuwa gharama Sana kuliko ukanunua kwa wingi, mfano mafuta nanunua kidumu cha Lita tano, unga wa sembe nanunua mfuko kg 50, mchele debe 1, sukari mifuko labda kumi, maharage debe 1, dagaa wa kigoma nusu debe, nafanya hivi ili kuepusha kununua mahitaji kidogo kidogo.
Maana najua hivyo vitu vikiwemo ndani nitakachodaiwa ni vitu vidogo vidogo tu labda nyanya nk.
Ndani tunaishi wawili tu na kuna wapangaji wengine majirani kadhaa huko ambao wa like ni wengi kuliko wa kiume na bibie anamashosti zake kadhaa kati ya hao majirani.
Sasa kuna kamuda flani nikaanza kuusoma mchezo kwamba nanunua vitu kwa wingi lakini havichelewi kuisha, yaani Kidumu cha mafuta Lita 5 kinakaa wiki mbili tu na ndani tuko wawili. Nikirudi jioni utasikia mume... Mafuta ndiyo yanaishia yamebaki kidogo sana cheki!!! Kesho njoo na mengine... Nikimuuliza bibie hii Lita tano imekatika ndani ya wiki mbili? Anasema ndiyo mume si tunamtumia!!!?
Mimi nikawa namchora tu. Hapo nikawa nishagundua anawapa na mashosti zake walalahoi kila wakitaka kupika wanakuja na tuvikombe twao kuomba mafuta ya kupikia, maji ya kuoga wanachemshia kwenye gesi yangu wapuuzi hawa.
Nikiwa sipo pia anawapa sukari, mchana nisipokuwepo anawagaia dagaa, jioni kabla sijarudi anakuwa kashawapa mchele kidogo na maharage kidogo maana anaona si vipo tuu!!? Kumbe tunatafuta Kwa jasho.
Sasa Jana niliwahi sana kurudi geto yaani saa saba niko ndani na sikutoka tena, inafika mida ya saa nane nikasikia bibie anaitwa kwa nje huko, na hawa kumbikumbi hawakujua kama kamanda nipo ndani... eti flani EEE.... bibie akaitika... Abeeee.... . Nigaie dagaa Shoga yangu si unajua tena mwenzio taabaniiiii..... maaamaaeeee nilitoka na jicho moja jekundu kuliko kawaida nilimtukana yule manzi vibaya mno nusu nimtie kelbu ya shingo na hajawahi kuniona katika hali hiyo hata siku moja.
Na nikarudi ndani kwa bibie nikampiga mkwara mmoja ambao hajawahi kuusikia wala kuuona kwenye muvi yoyote ile iwe ya kutisha ama ya mapigano. Na nikamwambia hivi vitu vikiisha safari hii utajua kwa kuvitoa na sinunui hivi vitu teeenaaa, hii gesi ikiisha jiandae kupikia kuni huko nje maana huku ndani sijawahi kupikia mkaa na sitihitaji kuona mkaa wa aina yoyote ile humu na nikirudi lazima nile sasa kazi kwako wewe si mama huruma? Nakutafutia mtaji utakuwa unatembeza kuni barabarani na nikirudi nikute chakula on time.....
Hapo kainama analia lia kama mtoto Mimi namkanda tu. Hapo naongea mafuta kidumu cha Lita 5 kimebaki nusu na kina wiki moja Tu.
Na vikiisha hivi ataona msoto atakaokula huyu hanijuiiiii.....
Amuulize mwenzie alietoka hapa kabla yake nae alikuwa na mbanga hizo hizo, vitu vilivyoisha alikula msoto wa maparachichi na juice ya embe miezi miwili mfululizo mpaka akatia adabu, nikitoka mihangaikoni jioni nambebea maparachichi mawili ya Jero na juice ya embe ya Jero,( huku Mbeya maparachichi mawili jero), na asubuhi ni karanga za kuchemsha.... kuna mama mmoja alikuwa anapitisha kila asubuhi nikawa namnunulia za buku anakula asubuhi mpaka mchana.
Nilikuwa namwambia sina hela ya gesi bibie wewe si ulikuwa unawaalika mashosti waje kuchemsha maji ya kuoga hapa? Hapo Mimi nishajipigia kitimoto yangu kilo na ndizi sita (Huku Mbeya nusu ya kitimoto ni 3,000 na kila nusu inandizi 3, hivyo kilo ni ndizi 6), sasa bada ya huo msoto aliokula aiseee nilikuja kununua kidumu cha Lita 5 cha mafuta ya kupikia kilikaa mwaka mmoja na miezi miwili.
Sasa bado na huyu we subiriiiiiii