Nimepiga mkwara mzito huyu manzi, huwa siendekezi ujinga.

Nimepiga mkwara mzito huyu manzi, huwa siendekezi ujinga.

Yeah,ni kweli kabisa, mimi nimeishi kwa mjomba alikuwa muuza duka na mke wake hakuwa kazi yoyote ile, lakini mke wake alikuwa mgawaji sana yaani majirani wanakuja kuchota maji kwenye bomba kila siku afu bili inakuja kubwa basi uncle anashangaa ndani tupo watatu afu bili inakuja 70,000 kumbuka apo mke wake ashaniambia nisisseme kama anagawa maji, siku moja uncle akailia doria akafanya kama anaenda kazini afu akachili room kwangu ,,,,weeee!!! Asubuhi tyu mke anapika chai mpaka ya majirani, majirani wakaja kuchota maji pale kama wote Daaah mi siku hiyo nakumbuka nilikuwa internship kwenye taasisi fulani ivi ila siku hiyo nilirudi kuchukua document fuln haaaa!!! Ile nafika tuu na uncle ndiyo anatoka ndani kuja kuwachezesha ngoma aiseee aliwatukana akamtukana na wife daaah si majirani si mke wote hawakuwa na hamu tena ,,,,,, bili ilianza kuja 25000 na matumizi mengine ya kawaida yakapu'ngua japo majirani walipunguza mazoea na nyumba yake
 
Kiongozi punguza roho mbaya siku mkeo atakapo kuja kukutwa na shida na wewe haupo nyumbani atasaidiwa na nani?
 
Picha lilivyo hapo hakosekani shosti anayetaka kufanya mapinduzi, shemeji akae kwa password
😂Hiyo kweli lazima kuna shosti yake anataka kuleta kanga yake hapa...... anavyoona kwa mwenzie vitu havikauki ndani anatamani ingekuwa kwake😂
 
Yeah,ni kweli kabisa, mimi nimeishi kwa mjomba alikuwa muuza duka na mke wake hakuwa kazi yoyote ile, lakini mke wake alikuwa mgawaji sana yaani majirani wanakuja kuchota maji kwenye bomba kila siku afu bili inakuja kubwa basi uncle anashangaa ndani tupo watatu afu bili inakuja 70,000 kumbuka apo mke wake ashaniambia nisisseme kama anagawa maji, siku moja uncle akailia doria akafanya kama anaenda kazini afu akachili room kwangu ,,,,weeee!!! Asubuhi tyu mke anapika chai mpaka ya majirani, majirani wakaja kuchota maji pale kama wote Daaah mi siku hiyo nakumbuka nilikuwa internship kwenye taasisi fulani ivi ila siku hiyo nilirudi kuchukua document fuln haaaa!!! Ile nafika tuu na uncle ndiyo anatoka ndani kuja kuwachezesha ngoma aiseee aliwatukana akamtukana na wife daaah si majirani si mke wote hawakuwa na hamu tena ,,,,,, bili ilianza kuja 25000 na matumizi mengine ya kawaida yakapu'ngua japo majirani walipunguza mazoea na nyumba yake
Ni hatari aisee yaani ukiwachukulia poa hawa majirani uchwara wanakutia hasara na ukiishiwa wanakuona boya hata salamu hawatokupa..
 
Ebwanaeeeeeeee, za leooo.

Moja Kwa moja kwenye mada.... Hivi nyie wanawake mkoje.... Hasa mnaoshinda nyumbani wakati sisi tupo kutafuta na kuvuja majaisho huko mtaani.

Iko hivi... Mimi huwa sipendi kununua vitu kidogo kidogo maana naona inakuwa gharama Sana kuliko ukanunua kwa wingi, mfano mafuta nanunua kidumu cha Lita tano, unga wa sembe nanunua mfuko kg 50, mchele debe 1, sukari mifuko labda kumi, maharage debe 1, dagaa wa kigoma nusu debe, nafanya hivi ili kuepusha kununua mahitaji kidogo kidogo.

Maana najua hivyo vitu vikiwemo ndani nitakachodaiwa ni vitu vidogo vidogo tu labda nyanya nk.

Ndani tunaishi wawili tu na kuna wapangaji wengine majirani kadhaa huko ambao wa like ni wengi kuliko wa kiume na bibie anamashosti zake kadhaa kati ya hao majirani.

Sasa kuna kamuda flani nikaanza kuusoma mchezo kwamba nanunua vitu kwa wingi lakini havichelewi kuisha, yaani Kidumu cha mafuta Lita 5 kinakaa wiki mbili tu na ndani tuko wawili. Nikirudi jioni utasikia mume... Mafuta ndiyo yanaishia yamebaki kidogo sana cheki!!! Kesho njoo na mengine... Nikimuuliza bibie hii Lita tano imekatika ndani ya wiki mbili? Anasema ndiyo mume si tunamtumia!!!?

Mimi nikawa namchora tu. Hapo nikawa nishagundua anawapa na mashosti zake walalahoi kila wakitaka kupika wanakuja na tuvikombe twao kuomba mafuta ya kupikia, maji ya kuoga wanachemshia kwenye gesi yangu wapuuzi hawa.

Nikiwa sipo pia anawapa sukari, mchana nisipokuwepo anawagaia dagaa, jioni kabla sijarudi anakuwa kashawapa mchele kidogo na maharage kidogo maana anaona si vipo tuu!!? Kumbe tunatafuta Kwa jasho.

Sasa Jana niliwahi sana kurudi geto yaani saa saba niko ndani na sikutoka tena, inafika mida ya saa nane nikasikia bibie anaitwa kwa nje huko, na hawa kumbikumbi hawakujua kama kamanda nipo ndani... eti flani EEE.... bibie akaitika... Abeeee.... . Nigaie dagaa Shoga yangu si unajua tena mwenzio taabaniiiii..... maaamaaeeee nilitoka na jicho moja jekundu kuliko kawaida nilimtukana yule manzi vibaya mno nusu nimtie kelbu ya shingo na hajawahi kuniona katika hali hiyo hata siku moja.

Na nikarudi ndani kwa bibie nikampiga mkwara mmoja ambao hajawahi kuusikia wala kuuona kwenye muvi yoyote ile iwe ya kutisha ama ya mapigano. Na nikamwambia hivi vitu vikiisha safari hii utajua kwa kuvitoa na sinunui hivi vitu teeenaaa, hii gesi ikiisha jiandae kupikia kuni huko nje maana huku ndani sijawahi kupikia mkaa na sitihitaji kuona mkaa wa aina yoyote ile humu na nikirudi lazima nile sasa kazi kwako wewe si mama huruma? Nakutafutia mtaji utakuwa unatembeza kuni barabarani na nikirudi nikute chakula on time.....

Hapo kainama analia lia kama mtoto Mimi namkanda tu. Hapo naongea mafuta kidumu cha Lita 5 kimebaki nusu na kina wiki moja Tu.

Na vikiisha hivi ataona msoto atakaokula huyu hanijuiiiii.....

Amuulize mwenzie alietoka hapa kabla yake nae alikuwa na mbanga hizo hizo, vitu vilivyoisha alikula msoto wa maparachichi na juice ya embe miezi miwili mfululizo mpaka akatia adabu, nikitoka mihangaikoni jioni nambebea maparachichi mawili ya Jero na juice ya embe ya Jero,( huku Mbeya maparachichi mawili jero), na asubuhi ni karanga za kuchemsha.... kuna mama mmoja alikuwa anapitisha kila asubuhi nikawa namnunulia za buku anakula asubuhi mpaka mchana.

Nilikuwa namwambia sina hela ya gesi bibie wewe si ulikuwa unawaalika mashosti waje kuchemsha maji ya kuoga hapa? Hapo Mimi nishajipigia kitimoto yangu kilo na ndizi sita (Huku Mbeya nusu ya kitimoto ni 3,000 na kila nusu inandizi 3, hivyo kilo ni ndizi 6), sasa bada ya huo msoto aliokula aiseee nilikuja kununua kidumu cha Lita 5 cha mafuta ya kupikia kilikaa mwaka mmoja na miezi miwili.

Sasa bado na huyu we subiriiiiiii

Kwa watu wawili ukinunua hivyo vitu, hata kama mnakula milo 6 vitaharibika.
 

Attachments

  • 12.jpg
    12.jpg
    20.9 KB · Views: 4
HAHAHAHHAHHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHHAHAHAAHHAHAHAHAHHAAHHAHA

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Aiseee Sina Mbavu
 
Kiongozi punguza roho mbaya siku mkeo atakapo kuja kukutwa na shida na wewe haupo nyumbani atasaidiwa na nani?
Sio uchoyo man.... Nilishawasoma hawa mashosti jirani zake ni wale wanaokuona wanamuona WA maana sababu ndani kwake kuna tuvitu vitu Ila asingekuwa navyo ni wale majirani wanakaaga kikundi kwa pamoja kuwasengenya watu hasa majirani zao. Wao tumewakuta. Sisi hapa ni wageni toka tumehamia tuna miezi mitatu tu sasa wanataka kutumia hiyo advantage sasa kamanda nikawapa za uso mixa mitama ya shingo mtaalam....
 
Usisahau mrejesho kwa hivyo unanunua inatakiwa mwezi ndio viishe maana mpo wawili tu
Jua kali sana mwambie
Jua ni kali kweli na sio mwezi tu..... kwa mwanamke anayezingatia matumizi mazuri kidumu cha mafuta lita 5 kinatakiwa kikae hata zaidi ya miezi miwili. Labda kama anaogea sawa....
 
Mimi ni mwanamke lakini nakusupport ile ile. Hekima! Hekima! Hekima!, Busara! Busara! Busara! Hata sisi ndo tungekua tunatoka kwenda kutafuta, tusingekubali vitu vifujwe ndani. Lets say ana mtoto, akamnunulia penseli leo na mtoto akaenda akampa 'shosti' yake shuleni akija akasema imepotea. Mwezi mzima kila siku anasema imepotea angeelewa?

Umimi unatuponza sana sisi wanawake. Mbaya zaidi huwa tunafikiri kushare na majirani ndo ujirani mwema kumbe si hivyo. Am pretty sure, siku mkifulia hao aliokua anawasaidia kwa mrengo wa "ushirikiano na majirani", wangemkataa.

Mkuu wangu wa kaya alishaniamshiaga jaramba mapema sana kuhusu mazoea ya sana na majirani. Akasema, ni rahisi sana mtu kukuattack coz anakujua inside out. Na most of the times wale tunaowasaidia sana na kuwaweka karibu, kwa sabbu wanatujua kama chu** zetu, wanajuaga angle za kupiga kwenye mshono.

Yes tushirikiane lakini kwa kiasi ili hata unayemsaidia ajifunze kumtegemea Mungu wake aliyemuumba. Mtu anapokulilia kila siku shida na ukamtatulia, humsaidii, unamharibu au pia anaweza kukuharibu wewe. Tusijipe roles za kuwa Saviours kwa watu hasa binadamu wa sasa hivi au wa miaka hii..dakika sifuri kukupiga na kitu kizito hatushindwi.

Unakuja kugundua baadae shosti ulokuwa unamsaidia, mtoto wake wa tatu si wa mume wake bali wa mume wako, na hivi hukuweza kushtukia kwa sabbu shosti kafanana na mwanae, inakuwa too late. Yote in the name of a good heart. Yes tuwe watu wema lakini kwa busara na kiasi.
 
Hahahahaaaaa,umefanya vizur

Ndo wanawake wengi walivyo afu unakuta wale mashost anaowapatia wanakuwa wanamsema jinsi alivyomjinga kwa hyo tabia yake ya kugawa gawa vitu na huwa wanafanya makusudi unakuta pesa wanazo ila wanafanya kukomoa,binadamu ni wajinga mno
 
Back
Top Bottom