Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Nimepiga simu Tanesco, wamesema mita yangu ilikuwa inadaiwa 18,000 kwa mwaka wa fedha ulioisha(2023/24) hivyo wamekata pesa hiyo niliponunua umeme leo.
Nikawauliza mbona wamekuwa wakinikata kila mwezi, hili deni wanalosema sijalipa mwaka mzima limetokea wapi?
Majibu(TANESCO ): Hizi taarifa zake ziko TRA za kodi za majengo, anaeshugulika na kodi za majengo ni TRA na sio Tanesco, Tanesco tunatumika pale kipindi mteja ananunua umeme kodi ya majengo inalipwa kupitia manunuzi yake ya umeme lakini kutokana na kumbukumbu za TRA bado huyu mteja anadaiwa hiki kiasi.
Kwahiyo kama kutakuwa na changamoto nyingine yoyote, kama yeye ana uhakika alikuwa akilipia kila mwezi anaweza akaonana na maafsa wa TRA ofisini wakamuangalizia deni lake kodi za majengo na watampa ufafanuzi zaidi kwasababu wao wana rekodi yake ya kodi za majengo kwa kipindi chote.
Nilipohoji mimi siwajui TRA kwasababu aliyechukua hela yangu ni Tanesco, akajibu wao hawana jukumu la kukata mtu bali ni TRA na ninaponunua umeme moja kwa moja TRA wanachukua hela husika. Nikamwambia mimi siwezi kwenda TRA kwasababu hizi hela huwa sizipeleki TRA na hili jambo TRA wameshwahi kuliruka simu ikaanza kupiga makolrokocho na mwisho ikakatwa.
Pia, soma=> TRA: Hatuhusiki na ukusanyaji wa Kodi kupitia LUKU
www.jamiiforums.com
Kwanini hizi mamlaka mbili zimeamua kutuibia watanzania, kwanza kodi yenyewe tangu mwanzo imekaa kiunyonyaji, baadae wakaamua kuiongeza kwa 50%, nusu nzima waliongeza na sasa wameona haijatosha wameamua kututoza mara mbili mbili

TANESCO: Hakuna kodi iliyoongezeka kwenye Majengo, pesa iliyokatwa ni deni la Julai 2023
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuhoji kuhusu makato ya Tsh. 2,000 kwenye LUKU, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema hakuna ongezeko la Kodi ya Majengo isipokuwa pesa hizo zimekatwa kufidia madeni yaliyotakiwa kulipwa 2023/24. Pia Soma: -