Nimepigwa hard disk speed ni ndogo sana, tusiwe na haraka tuchukue muda kuzikagua kuepuka huu upigaji

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
UPDATE / MREJESHO:

Tatizo lipo kwenye case ni usb 2.0, nimetesti kuiunganisha moja kwa moja kwenye desktop speed ni nzuri MB 50 kwa sekunde, chief mkwawa kanishauri ninunue case ya usb 3.0

1712175853711.png

model ni HTS545032A7E380

Nilienda kununua hard disk ya GB 320 kwa elf 25 maalum kwajili ya kuifanya iwe external.

Testing niliyofanya ni kuona kama inasoma na kuiformat, nikalipia.

Sikuitumia kama wiki 2 hivi, Leo nahamisha faili la GB 70 na kitu yani ilibidi nisubiri saa na dakika 15, speed inasoma M16 hadi 17 kwa sekunde,

nimefomati, nimebadili reader, n.k. lakini wapi,

nimerudi dukani ila sikuchukua risiti hawanikumbuki ndio nishaingizwa mjini.

kuna mtaalam kanijuza nikitaka kununua nyingine nichague iliyoandikwa 7200 rpm na kuendelea, hii niliyonunua 5400 rpm ni za zamani sana
 
Hard disk ni teknolojia inayopotea kwenye industry mkuu, kwa Bei uliyouziwa na speed sidhani kama wamekuibia, mana flash drive ya gb 32/64 kuzipata kwa Bei hiyo ni kipengele.
Tumia cloud kuhifadhi data za msingi
 
Tumia cloud kuhifadhi data za msingi
Mkuu hio huduma labda kwa nchi za mbele huko intenet ina speed na haina kikomo, mafaili mtandaoni unapandisha na kushusha utafkiri umechomeka external.

pia ninatunza vitu kama muvi za kudownload , vitabu pdf, software za kuvunja, miziki, n.k. Ni vitu ambavyo vinaweza kufutwa, haya mambo ya copyright wenzetu wanachukulia serious sana.
 
Ukizingitia item per price haujaibiwa boss ulicholipia ndicho ulichopata tatizo labda ungelipia 50k then ukapata bidhaa iyo hapo ndipo ungisema umepigwa,
Ushauri wangu kwa wakati mwingine, nunua SSD hizi technology yake ni yakisasa, speed iko juu pia ni portal na handling yake ipo vizuri hata incase ukidodosha sio rahisi kuharibika
 
View attachment 2953291

Nilienda kununua hard disk ya GB 320 kwa elf 25 maalum kwajili ya kuifanya iwe external.

Testing niliyofanya ni kuona kama inasoma na kuiformat, nikalipia.

Sikuitumia kama wiki 2 hivi, Leo nahamisha faili la GB 70 na kitu yani ilibidi nisubiri saa na dakika 15, speed inasoma M16 hadi 17 kwa sekunde,

nimefomati, nimebadili reader, n.k. lakini wapi,

nimerudi dukani ila sikuchukua risiti hawanikumbuki ndio nishaingizwa mjini.

kuna mtaalam kanijuza nikitaka kununua nyingine nichague iliyoandikwa 7200 rpm na kuendelea, hii niliyonunua 5400 rpm ni za zamani sana

model ni HTS545032A7E380

pia nimeona kwengine mtandaoni ikilalamikiwa ipo slow sana
Hapana, si vizuri kusema umepigwa au labda tu hujui ulikuwa unataka kununua nini?
Na kingine ni RPM sio kipimo cha harddisk kutransfer data haraka (kutoa au kuingiza). Jua kwamba RPM hiyo 54000 ni mzunguko wa disk kwa dakika 1. (Ndani ya hard disk kuna cd ndogo) ndiyo iliwekewe huo upimaji.

Cha pili, load unayoipa pia ita determine speed, nilivyoona hii post yako ikabidi nami nijaribu kwenye hard disk yangu. Nikaweka 7GB tranfer rate ikawa 23mbps (sasa hapa ni uwezo wa pc pia na source, kwa mfano mimi natumia SSD na pc ni 8cores, i7 6th gen). Then nikajaribu 35GB ikawa inaenda zaidi ya 35mbps.

Kwa hiyo ili useme umepigwa lazima ujue factors ambazo zinakuonesha disk ni mbovu au nzima.

Nyongeza, kama disk kwenye rotation yake ina scrach hivi, hiyo maisha yake yako mwishoni. Vinginevyo disk iko poa kabisa kwa speed hiyo.
 
Kuna mtu alishanielekeza namna ya kucheki life span ya Hard disk.

Hard disk ikitumika sana na vile inakuwa formated kila mara inashuka ubora.
 
Gb 500 ni chini ya 20,000 kama unanunua used, pia ni sahihi 7200rpm ina speed kuliko 5400rpm.

Angalia na file pia unalohamisha, kama vifile ni vidogo vidogo vingi speed inashuka.

Jambo jengine ni controller kama Case ya hdd haina usb 3.0 controller hata kama hdd ina speed hutapata hio speed.

Kama wengine walivyo shauri kama huna matumizi makubwa sana tafuta ssd, kama 50,000 ssd mtumba 256GB
 
Asante kwa mchango mkuu, nimeona nayo case ya hdd ni usb 2.0 ambayo speed yake ya juu ina copy 40 MB kwa sekunde

nimepigwa kote kote hdd na case
Hiyo case ya usb2.0 iko slow sana na wakati mwingine kwenye pc nyingine itagoma kusoma, kanunue case ya 3.0
 
RPM sio kipimo cha harddisk kutransfer data haraka (kutoa au kuingiza). Jua kwamba RPM hiyo 54000 ni mzunguko wa disk kwa dakika 1. (Ndani ya hard disk kuna cd ndogo) ndiyo iliwekewe huo upimaji.
Rpm ni kipimo kinachopewa uzito kwenye speed ya hdd, kadiri mizunguko inavyoongezeka na speed inakuwa kubwa.
 
Gb 500 ni chini ya 20,000 kama unanunua used, pia ni sahihi 7200rpm ina speed kuliko 5400rpm.

Angalia na file pia unalohamisha, kama vifile ni vidogo vidogo vingi speed inashuka.

Jambo jengine ni controller kama Case ya hdd haina usb 3.0 controller hata kama hdd ina speed hutapata hio speed.

Kama wengine walivyo shauri kama huna matumizi makubwa sana tafuta ssd, kama 50,000 ssd mtumba 256GB
Ssd now pia hazina bei. AliExpress ssd za 1tb mpya ni 120000+

Unanunua na kava kwa 25000 tena linatumia type c.

Na uzuri ziko vzr tu.
 
Gb 500 ni chini ya 20,000 kama unanunua used, pia ni sahihi 7200rpm ina speed kuliko 5400rpm.

Angalia na file pia unalohamisha, kama vifile ni vidogo vidogo vingi speed inashuka.

Jambo jengine ni controller kama Case ya hdd haina usb 3.0 controller hata kama hdd ina speed hutapata hio speed.

Kama wengine walivyo shauri kama huna matumizi makubwa sana tafuta ssd, kama 50,000 ssd mtumba 256GB

asante kwa feedback, nimeona tatizo lipo kwenye case ni usb 2.0, nimetesti kuichomeka hard disk moja kwa moja kwenye desktop computer ya mezani nimeweza kuhamisha file kwa speed ya 50 MB kwa sekunde,

hapa nikinunua hio case ya usb 3 nitapata speed hio ?
 
Hiyo case ya usb2.0 iko slow sana na wakati mwingine kwenye pc nyingine itagoma kusoma, kanunue case ya 3.0
Ni kweli, Tatizo lipo kwenye case ni usb 2.0, nimetesti kuiunganisha moja kwa moja kwenye desktop speed ni nzuri MB 50 kwa sekunde,
 
asante kwa feedback, nimeona tatizo lipo kwenye case ni usb 2.0, nimetesti kuichomeka hard disk moja kwa moja kwenye desktop computer ya mezani nimeweza kuhamisha file kwa speed ya 50 MB kwa sekunde,

hapa nikinunua hio case ya usb 3 nitapata speed hio ?
Ndio mkuu, issue ni kwamba hizi za kkoo karibia zote sio 3.0, kama unapata external mbovu ama ladha used kuna possibility kubwa kuwa usb 3.0.
 
Mkuu hio huduma labda kwa nchi za mbele huko intenet ina speed na haina kikomo, mafaili mtandaoni unapandisha na kushusha utafkiri umechomeka external.
Sidhani kama una data za msingi utaconcern sana bandwidth, mana speed ya internet inaweza kuwa shida yako binafsi na ISP pamoja na package unazotumia.
pia ninatunza vitu kama muvi za kudownload , vitabu pdf, software za kuvunja, miziki, n.k. Ni vitu ambavyo vinaweza kufutwa, haya mambo ya copyright wenzetu wanachukulia serious sana.
Mafile kufutwa siokweli kwasabu unaweza kuincrypt.
 
Back
Top Bottom