Pole sana dada.
Wanaume wanaopiga wanawake wengi wao wana shida kwenye uanaume wao au aina ya malezi waliyopata. Kama sio ana ishu ambayo inampunguzia uanaume wake(kama vile matatizo ya nguvu za kiume,uume mdogo,kuonewa na wanaume wenzake physically);-->Wenye shida hizi huhisi kama vile ili ku-prove uanaume wao(male ego) ambao unakuwa umeshuka kwa kasi ya ajabu, basi ni lazima na muhimu wawanyanyase na kuwapiga viumbe ambao ni dhaifu kwao(wanawake, watoto); Na huwa wanakuwa wakali wakali muda wote bila sababu yoyote ya msingi.
Au utakuta something went wrong wakati wa malezi yake(malezi ya mzazi mmoja,mama yake kunyanyaswa na baba yake mbele yake alipokuwa mdogo, historia ya kuwa sexually abused alipokuwa mdogo, malezi ya kimila ambayo yanasisitiza katika kuwaona wanawake kama sio binadamu au kama vile watoto).
Ni ukale wa kizamani sana kupiga mwanamke karne hii(japokuwa nakubali asilimia 100 kuwa mara nyingine wanawake huwa wana tempt sana uwapige---lakini hii kwa mwanaume wa kawaida asie na shida kisaikolojia atajizuia, na akizidiwa sana atampiga mwanamke kofi moja au mawili; Na sio kufikia extent ya kumpiga hadi kumtoa ngeu)