Nimepokea mzigo kutoka Ali Express kupitia Posta

Uzi mzuri mkuu umenimotivate na Mimi kuagiza hebu nielezee vizuri hapo kwenye sanduku la posta, ulikua na anuani yako yaposta personally (p.o box) au vipi? Sijaelewa hapo uliposema uliweka anuani ya posta ya morogoro.
Kila Mkoa hua una postal code zao au zip code, sasa uliingia hata google andika postal code/zipcode ya mkoa wako watakuletea, ndo uijaze hapo kwenye adress yako na namba ya simu ambyo unaitumia, means mzigo utakuja kwenye posta ya mkoa wako then wao watapiga simu kwa namba iloandikwa wakat wa shipment ya mzigo
 
Kwanini hukufungua desipute? Ukiibiwa kitu ni msala kwa posta wao wenyew...na mzigo usipo upata utarudishiwa hela yako kweny refund...haya mambo unatakiwa ujifunze kwanza ,hakuna kitu utaibiwa au kupoteza pesa yako..hii ni system
 
Hongera,hata mimi nimewahi kuagiza mzigo maramoja kupitia Aliexpress,sikupata usumbufu wowote na ulikuja mpaka posta wakanipigia simu nikaupata ukiwa kamili,ilikuwa ni bluetooth speaker...
Asant mkuu [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Nadhani kwa vitu vyenye thaman kubwa ni safe kutumia hawa agents wa kuagiza mizigo wenye ofis zao hapa tanzania unaongea nae bei wanakuletea mzigo na wao ndo wanasimamia kila kitu mpaka mzigo ukufikie
Akina nani?
 
Okay nimeelewa Asante.
 
postal code zinaenda mpaka levo ya kata.
 
Kumbe ata wamatombo nao wanaweza agiza mzigo ukapokea posta....hongereni waluguru
 
Umezunguka mnoo, ukihitaji msaada tafuta tukusaidie. Flash sio ya kuchukua miezi miwili njiani na unakuja kuandikia uzi. Na hiyo njia yako ya ulipaji wa pesa sio nzuri, hapo kuna makato hujatwambia.
Njia nzuri ya kulipia bidhaa mtandaoni ni ipi?
 
Nmejaribu kuangalia kwenye laptop shipping fee zao kubwa sana yaani, kwa mfano pia nmetafuta HeatPress ya 5 in 1, machine ambayo wao wanauza $120 tu ila Shipping fee naambia $250 ukijumlasha hapo $350

Heat press huwa hatupakii kwa shippers wa li express.. tunapakia kwa 3rd party hasa hasa dhl
 

Hii ni shida inawapata wengi pia. Ni MUHIMU sana kusoma Reviews za Seller/Supplier wako Kabla haujaamua kununua kwake.
Hizi platforms eBay/AliExpress zinaonesha pia huyu seller amekua akifanya biashara kwa hiyo platform tangu lini pamoja na rating ambazo buyers wamempatia. Hii inakusaidia kujua kama ni legit Au ana magumashi.

Nakumbuka 2014, niliwahi kununua laptop. Jamaa wa Dhl wakaniletea na makaratasi ya kodi za TRA. Tangu hapo nikawa discouraged kununua vitu vya thamani kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…