Nimepokea mzigo kutoka Ali Express kupitia Posta

Nimepokea mzigo kutoka Ali Express kupitia Posta

Ungetupa ABC’s tu mkuu.
Mbona ni suala la kutupa uzoefu tu kwa kuandika kuwa ni njia “X” Au fanya hivi. Inbox si itajaa? Au kuna malipo inabidi tuchangie?
Huyo jamaa ni mawenge et nifate inbox [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Habari wana Jamvi, nilikua nina mashaka sana na kuagiza mizigo Ali Express kwamba ntapokeaje mzigo wangu.

Nikafanya majaribio nilinunua bidhaa mbili Moja ni flash ambayo ipo kama kadi ya master card (GB16) na nyingine ni Case ya external hard disk.

Niliingia kwenye aliexpress nikatengeneza profile yangu na kwenye adress niliweka morogoro na nkaweka postal code ya morogoro ambyo ni 67000. Basi nkaenda kwenye kulipia bidhaa.

Malipo niliyafanya kwa kuingiza namba za Visa Card yangu ya CRDB then nkaweka security code (namba 3, zilizopo nyuma ya kadi yako) nilipomaliza basi wao wakakata kiasi cha pesa kinachohitajika moja kwa moja kutoka CRDB.

Bidhaa zangu zote nilizonunua zilikua hazizid elf 10 bei yake kwa pesa ya kitanzania na zote nilichagua za free shipping. Baada ya kuweka order ilikua mwez wa 12 mwishon nkatulia kusubiri na kila siku nlikua naingia kwenye shipped items naona progress mzigo umefika wapi.

Nmesubiria sana mpaka mwez wa kwanza ukaisha kwenye track ya mzigo wangu naona zmeshafika destination country, nikawa nasubiria.

Mpaka mwanzon mwa mwezi wa 2 kama tar 4 ivi nkapigiwa simu na Posta Mkoa Morogoro naambiwa kuna package zako 2 hapa, nkaenda pale nkapewa control number. Kila mzigo pale posta nmelipia 2350. Jumla nkalipa 4700. Nkapewa package zangu.

Bidhaa ni nzuri na hazina shida yoyote nmekua confident kuagiza mizigo kwa hawa jamaa.View attachment 2116927
Kwa mawazo yangu hawa posta wanafaa kwa mizigo midogo midogo yenye thamani ndogo, lakini kwa mizigo kama simu, tv etc. miongoni wa wafanyakazi wa posta sio waaminifu unaweza kujikuta umepoteza vitu vyako ulivyotumia gharama kubwa kuagiza.
 
Kwa mawazo yangu hawa posta wanafaa kwa mizigo midogo midogo yenye thamani ndogo, lakini kwa mizigo kama simu, tv etc. miongoni wa wafanyakazi wa posta sio waaminifu unaweza kujikuta umepoteza vitu vyako ulivyotumia gharama kubwa kuagiza.
Simu haina shida,lakin piah hata ikitokea mzigo wako umepotea tuseme mikonon kwa posta bado utapewa refund..mzigo wako hauwez kuonekana umeupata wakat haujaupokea posta...na posta wao wanalijua hilo ukipotea mzigo ni msala kwao Tena posta masta atakiwasha hadi mzigo upatikane...mambo sio kama zamani
 
Kwenye gharama za shipping ; kila bidhaa/supplier huwa anaandika shipping agent wake; hilo ndio linaleta tofauti ya bei.
Wanunuzi wa mitandaoni ni muhimu sana kuzingatia shipping agent;
Kwa mfano kama unanunua bidhaa kwa nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini wapo shipping agency zao zina gharama sana especially kama mzigo unakuja Tanzania.
 
Me naomba kufahamu mfano nataka kuagiza printer machine ya epson hivi maswala ya TRA yanaweza husika hapo?
 
Inategemea..kariakoo redmi note 10 inauzwa hadi 650 uko wakat aliepress simu ilikua ni 450 tu,redmi note 11 imetoka inauzwa 392k,bongo wanapiga 700 uko... Bluetooth speakers ya anker soundcore motion plus bongo 450 wakat aliepress laki 2 na 10 tu,jbl charger 5 wanauza hadi 350 wakat bongo inapigwa 600+ ,hizo item zote hakuna hela utalipia,na incase ukikutana nayo ni 2300 ikizid 5900 kama sio bure kabisa..
Nipe jina la huyo supplier
 
Baada ya kuusoma huu uzi nkapata courage ya kuagiza mzigo.

Nikaingia Aliexpress chap, nkaagiza tar 02/04, ukaanza kuwa processed tar 05/04,

then tar 29/04 natumiwa ujumbe kutoka posta nkachukue mzigo wangu, tena posta wilayani kabisa huku.

Niko confident sasa kuendelea kuagiza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana
 
Nmejaribu kuangalia kwenye laptop shipping fee zao kubwa sana yaani, kwa mfano pia nmetafuta HeatPress ya 5 in 1, machine ambayo wao wanauza $120 tu ila Shipping fee naambia $250 ukijumlasha hapo $350
Chagua kwa meli ukiagiza kwa ndege huwa ni gharama kisa zile battery
 
Back
Top Bottom