Nimepokea mzigo kutoka Ali Express kupitia Posta

Nimepokea mzigo kutoka Ali Express kupitia Posta

Boss naweza kukuguide, free out of any charge.....utafanya wew mwenyewe....mim ntakuwa nakupa tu maelekezo, mtendaji utakuwa ni wewe....na kwa yetote humu jukwaani

#0622506787...if it'll be inbox au public , pote sawa
Pamoja Mkuu ntakuchek
 
Kuna store nyingine wazinguaji ukiagiza kitu wanakaa na order mpaka siku za kupokea parcel zinakaribia ndo wanaship fasta mfano hyo hapo juu tang septmber 10 bt nashukuru wiki ijayo naweza pata
Capture%2B_2022-10-11-15-02-04.jpg
 
Habari wana Jamvi, nilikua nina mashaka sana na kuagiza mizigo Ali Express kwamba ntapokeaje mzigo wangu.

Nikafanya majaribio nilinunua bidhaa mbili Moja ni flash ambayo ipo kama kadi ya master card (GB16) na nyingine ni Case ya external hard disk.

Niliingia kwenye aliexpress nikatengeneza profile yangu na kwenye adress niliweka morogoro na nkaweka postal code ya morogoro ambyo ni 67000. Basi nkaenda kwenye kulipia bidhaa.

Malipo niliyafanya kwa kuingiza namba za Visa Card yangu ya CRDB then nkaweka security code (namba 3, zilizopo nyuma ya kadi yako) nilipomaliza basi wao wakakata kiasi cha pesa kinachohitajika moja kwa moja kutoka CRDB.

Bidhaa zangu zote nilizonunua zilikua hazizid elf 10 bei yake kwa pesa ya kitanzania na zote nilichagua za free shipping. Baada ya kuweka order ilikua mwez wa 12 mwishon nkatulia kusubiri na kila siku nlikua naingia kwenye shipped items naona progress mzigo umefika wapi.

Nmesubiria sana mpaka mwez wa kwanza ukaisha kwenye track ya mzigo wangu naona zmeshafika destination country, nikawa nasubiria.

Mpaka mwanzon mwa mwezi wa 2 kama tar 4 ivi nkapigiwa simu na Posta Mkoa Morogoro naambiwa kuna package zako 2 hapa, nkaenda pale nkapewa control number. Kila mzigo pale posta nmelipia 2350. Jumla nkalipa 4700. Nkapewa package zangu.

Bidhaa ni nzuri na hazina shida yoyote nmekua confident kuagiza mizigo kwa hawa jamaa.

View attachment 2116927
Kwenye adress uliweka morogoro kwa maana ya sanduku la posta ama maana kwa mfano mimi sina sanduku la posta hapo ndo nakwamaa wewe ulijazaje mkuu
 
Na kama hauna mkuu inakuaje hapo manuva mengine
Unatumia la mkoa au wilaya. Mzigo utakapofika pale utapigiwa simu ili kuufata kwa sababu mzigo utakua na maelezo ya unapokwenda, maelezo ambayo ulijaza wakati unaagiza, maelezo ikiwemo namba ya simu
 
Sanduku la posta sio lazima uwe nalo

Mimi sina Sanduku la posta ila nimeagiza vitu kibao na nimevipata

Wewe kwenye Addres jaza nchi uliyokuwepo ambayo ni Tanzania,jaza mkoa wako,wilaya na mtaa wako kisha malizia na zip code za eneo unalokaa umemaliza kazi
Kwahyo mzigo wako ukifika unapigiwa simu unaenda kuupokelea wapi posta au?
 
Unatumia la mkoa au wilaya. Mzigo utakapofika pale utapigiwa simu ili kuufata kwa sababu mzigo utakua na maelezo ya unapokwenda, maelezo ambayo ulijaza wakati unaagiza, maelezo ikiwemo namba ya simu
Kwamfano la mkoa au wilaya unalipataje mkuu ili nilitumie hilo hilo kwa eneo nilipo now
 
Kwahyo mzigo wako ukifika unapigiwa simu unaenda kuupokelea wapi posta au?
Ukishanunua bidhaa itakuwa na tracking number ambayo utaitumia kujua mzigo wako mahali ulipo kuanzia unapotoka kwa muuzaji mpaka unaingia nchini

Kwahyo mzigo ukishaingia nchini we unaenda posta kuuchukua maana wanaweza wasikupigie so usitegemee sana kupigiwa we track tu mzigo wako inatosha

Mpaka sasa nimeagiza mizigo kama saba hivi lakini kwenye hiyo saba ni mizigo miwili tu ndo ambayo nilitumiwa message nikachukue mzigo wangu mara nyingine zote nilikua na track nikiona imefika naibuka nabeba mzigo nasepa

Hapo chini Nimeweka message waliyowahi kunitumia posta

Screenshot_20221212-151448_Messages.jpg
 
Kwahyo mzigo wako ukifika unapigiwa simu unaenda kuupokelea wapi posta au?
Na kuhusu sehemu ya kupokea mizigo mara nyingi huwa ni kwenye ofisi za posta pale lakini wakati mwingine supplier anatumia wasafirishaji ambao hawaleti mizigo posta

Mfano mwezi huu kuna mzigo nilinunua lakini suppliers hakutumia njia ya posta na mimi nilikua sifahamu hilo kwahyo mimi nilienda posta nikawaonesha tracking number ndo wakaniambia Huo mzigo wako umepokelewa na Kampuni nyingine ya Speedaf ambayo ofisi zake zipo mikocheni so nikaenda zangu mikocheni mtaa wa Ursino nikabeba mzigo wangu

Hapo chini nimeweka tracking ya huo mzigo niliochukua juzi kati
Screenshot_20221206-111510_Chrome.jpg
 
Kwenye adress uliweka morogoro kwa maana ya sanduku la posta ama maana kwa mfano mimi sina sanduku la posta hapo ndo nakwamaa wewe ulijazaje mkuu
Kwenye kipengele cha Address jaza Morogoro, kuna sehem inahitajika ujaze Postal Address au Postal Code pale andika 67,000 hiyo ndo postal code ya Mkoa, inamaana mzigo ukifika pale utapigiwa au kutumiwa meseji kwa namba ya simu ambayo uliijaza katika taarifa zako
 
V
Ukishanunua bidhaa itakuwa na tracking number ambayo utaitumia kujua mzigo wako mahali ulipo kuanzia unapotoka kwa muuzaji mpaka unaingia nchini

Kwahyo mzigo ukishaingia nchini we unaenda posta kuuchukua maana wanaweza wasikupigie so usitegemee sana kupigiwa we track tu mzigo wako inatosha

Mpaka sasa nimeagiza mizigo kama saba hivi lakini kwenye hiyo saba ni mizigo miwili tu ndo ambayo nilitumiwa message nikachukue mzigo wangu mara nyingine zote nilikua na track nikiona imefika naibuka nabeba mzigo nasepa

Hapo chini Nimeweka message waliyowahi kunitumia posta

View attachment 2444035
VIPI kuhusu charges za kodi
 
Sanduku la posta sio lazima uwe nalo

Mimi sina Sanduku la posta ila nimeagiza vitu kibao na nimevipata

Wewe kwenye Addres jaza nchi uliyokuwepo ambayo ni Tanzania,jaza mkoa wako,wilaya na mtaa wako kisha malizia na zip code za eneo unalokaa umemaliza kazi
Ivi izo zip code ndio kitu gani
 
Back
Top Bottom