Nimepokea mzigo wa kwanza kutoka AliExpress

Nimepokea mzigo wa kwanza kutoka AliExpress

Kaselele

Senior Member
Joined
May 19, 2022
Posts
171
Reaction score
476
Wakuu habari.

Baada ya kusoma ule uzi ambao jamaa alielezea jinsi ya kuagiza smart watch kutoka AliExpress na mimi nikasema wacha nijaribu.

Kuna simu yangu ilivunjika kioo nilipouliza dukani nikaambiwa kinauzwa laki na nusu.
Nikasearch AliExpress nikakuta kinauzwa 58,000.

Niliweka oda na nikatakiwa kulipia, kwenye malipo nilitengeneza TigoPesa master card ya miezi mitatu, ndipo nikarudi aliexpress kufanya malipo.

Nilichokifanya nilichaguwa supplier mwenye shipping fee ya chini kabisa ambapo nilipata wa gharama ya TZS 3000. Kwenye malipo tigo walinikata 6000 (sijui walikata kwa kutumia rate gani)

Mwisho wa siku kioo cha laki na nusu dukani kimefika mkononi mwangu kwa 67,000 ndani ya wiki mbili.

My take:
Ukinunua kitu AliExpress usichoke kusearch suppliers tofauti.

IMG-20230930-WA0003.jpg
, kwenye kitu unachokitaka kuna suppliers wana "free shipping"
 
Duuh ndio ufungue Uzi kabisa...
Anyway siku ukipigwa Lete pia uzi
 
Back
Top Bottom