Nimepokea taarifa za kuhuzunisha kuhusu bondia Floyd Mayweather

Nimepokea taarifa za kuhuzunisha kuhusu bondia Floyd Mayweather

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Bondia asiyepigika Floyd Money Mayweather hatimaye amekubali kufanya rematch na Conor McGregor ila safari hii haitakuwa boxing tena bali UFC kwa dau la 1 billion USD

Na hatoishia kwa Conor tu bali atapambana na mabondia wengine watatu wa UFC kwa dau lisilopungua pia 1 billion usd

Kiukweli natamani haya mapambano Floyd ayavunje tu hao jamaa wa UFC wanamtamani kweli kwa kuwa wamemshindwa kwenye boxing sasa wamemualika kwao kwa kumdanganya na dau nono na mwishoe Floyd amewakubalia.

Hizi tamaa za Floyd zimenikwaza sana mimi kama shabiki wake nambari moja ulimwenguni

Falsafa zake Floyd ipo siku zitamtokea puani , yeye husema kuwa haangalii sana kupoteza pambano yeye huangalia pesa atakazo ingiza baada ya pambano.

Lakini siku zote bwana pesa huisha ila heshima uliyojiwekea na kuitunza kamwe haiwezi kuisha au kushuka.

Sasa kwa mwendo huu naona kabisa ile record yake ya undefeated inaenda kupotea.
 
Wewe shabiki namba moja haujui kua jamaa alishapigana mpaka mieleka? Halafu alipigana na Big Show na akashinda, game nzima ilikua rigged.

Same shit can happen huko kwenye ufc.
Mkuu hii comment umeandika ukiwa na akili timamu kweli?

Hivi hujui kama lile pambano lilikuwa kama maigizo tu?

Muda mwengine utumie akili za kiutu uzima kidogo kwenye kuchangia mijadala.
 
Hahaha mkuu huko ufc ataenda kufa cz kule ni mangumi na mateke lakini naomba niseme tu floyd yupo vizuri sana kwenye ngumi lakini kwenye mateke na wepesi macregor yupo fiti sana kwa ufc floyd kumpiga macgregor ni ndoto
 
Mkuu hii comment umeandika ukiwa na akili timamu kweli?

Hivi hujui kama lile pambano lilikuwa kama maigizo tu?

Muda mwengine utumie akili za kiutu uzima kidogo kwenye kuchangia mijadala.
Usinidhalilishe kwamba haujui kiingereza au? Sasa rigged si ndiyo maana yake ile kitu ilikua maigizo?

Na ndo nasema inawezekana hata kwenye ufc ikawa hivyo hivyo.
 
Hahaha mkuu huko ufc ataenda kufa cz kule ni mangumi na mateke lakini naomba niseme tu floyd yupo vizuri sana kwenye ngumi lakini kwenye mateke na wepesi macregor yupo fiti sana kwa ufc floyd kumpiga macgregor ni ndoto
Floyd hawezi kushinda kule atajiharibia tu.
 
Usinidhalilishe kwamba haujui kiingereza au? Sasa rigged si ndiyo maana yake ile kitu ilikua maigizo?

Na ndo nasema inawezekana hata kwenye ufc ikawa hivyo hivyo.
Sio rahisi kama unavyofikiria
 
Watu wengine bhana. Kwani ujui ndondi skuizi ni siasa skuizi?
 
Sio rahisi kama unavyofikiria
Inawezekana.

Mkataba hua unakua kwamba "Wewe A utachukua asilimia 48 ushinde ushindwe wewe B utachukua asilimia 52 ushinde ushindwe"

Ndiyo maana Mayweather kawakimbia wakina Rigo, Crawford, GGG, Banks Jr n.k. kwasababu alifocus kwenye pesa. Katumia muda mwingi sana ulingoni na journeyman kuliko real boxers.
 
Back
Top Bottom