Nimeponyeka kutapeliwa na rafiki wa facebook

Aisee hii kitu imenitokea wiki iliopita lakin mim nilimkaushia sikumpa namba yangu ya WhatsApp. Kwa sababu kuna ndugu yangu alinielezea juu ya utapeli wao Kwa hiyo nilishtuka mapema
Hata mm ilinitokezea kuna mmoja aliingia na kunitumia ujumbe wa salam nikamjibu mwisho akahitaji namba yangu ya watsap nikamkaushia.
 
🏃🏃🏃🏃kuna dogo hapa kitaaa alitengenezwa hivo hivo hadi akatumiwa picha ya parcel imeandikwa anuani na majina yake nkamwambia ww unaibiwa akabisha matokeo akatuma usd 120 kwa westernunion afu bilabila alikwapua hela dukani kwao akijua mzigo ukiingia Anauza iphone X moja tu kila kitu byeee🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Mkuu hawa wamekuwa wengi sana mimi mwenyew kanitumia mapicha ya laptop, i
I phone, galaxy anasema kuna.mzigo katuma ethiopia ukifika ethiopia atacheki ndege ya mizigo inayokuja tz ahaaa na tumefahamiana juzi tu. matapeli ni wengi now
 
Nakumbuka ilikua live macho macho na TAPELI kampala sehemu moja Garden city/Jinja road alinikosa kidogo. Kisha akaniambia ur very lucky my friend.
 
Nami nilipona kutapeliwa na mtu wa aina hii huko Twitter akanitumia ujumbe kujitambulisha kwamba yeye ni Daktari yuko Ujerumani ila huwa anasaidia watu wenye shida kwani aliachiwa fedha nyingi za urithi na wazazi wake na kwamba hana familia, anaona ni vema azitumie kuwasaidia wenye shida kama alivyoachiwa maagizo na Baba yake ya kuwajali wenye shida.

Akajieleza kwamba anakuwa busy na kazi za utabibu hivyo muda mzuri wa kuwasiliana ni baada ya kutoka kazini na tuwasiliane kwa email

Kwanza aliuliza historia ya maisha yangu nikamweleza akasema yeye ni Mwanamke na anapenda kusaidia wanawake wajane akaomba niwatafute wajane wenzangu kila mtu aeleze matatizo yake, kilichofuata baada ya hapo tunaambiwa tumeni pesa tuwatumie mizigo yaani zawadi kutoka Ujerumani.

Nilishtuka kuona kajichanganya kanitumia email kwamba tuwasiliane ni tafaouti na alonitumia siku ya kwanza nikafungua email nyingine nikajitambulisha kwa jina lingine nikijifanya ni mtu mwingine nikauliza juu ya Shirika la kusaidia wenye shida ya matibabu akasema yeye si Daktari wala hajishughulishi kutoa msaada.

Tangia siku hiyo nikakata mawasiliano na sijawahi kumtafuta wala hajanitafuta, nikawaeleza wale wenzangu tukaachana na mpango wa kutuma pesa na kupenda misaada.







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ulikosea. Ungemwambia akutumie kitambulisho chake ili umtumie pesa. Akituma hapo ndo ungejua kumbe wala si mzungu. Anakutumia kitambulisho chake na pesa haumtumii. Halafu unamwambia unakwenda kumshitaki.
Wengine hutuma hadi passport zao kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…