Nimepooza kiuno hadi chini, msaada tafadhali

Pole sana,mjomba wangu alipooza mwili mzima,hawezi kuongea,kula ni kwa mrija,anashinda na diapers,ila hospital hawakuweza kumsaidia zaidi ya kucontrol presha isipande juu mana ni kama alitaka kupata stroke
Tulichoamua kufanya ni kuleta wachungaji nyumbani daily na kumchua
Sasa hivi amerudi normal kabisa,anatembea,anaongea,kila kitu anafanya mwenyewe!
Usikate tamaa tafuta wachungaji wenye hofu kweli ya Mungu,wakati wanaendelea na maombi unaoishi nao wasiache kukuchua lakini pia uende kwa physiotherapist,hakika utakaa sawa!
Pole kwa changamoto,yataisha tu hayo!
 
Ungepata msaada haraka kama ungejieleza vizuri,hasa chanzo cha hiyo shida...
 
Maradhi hayana adabu. Hapo ndio mtu unapokata tamaa kwamba Mungu yupo kweli. Mbona kaacha kiumbe chake kitaabike hivi?
Mi sijui sipo deep kwenye maswala ya dini. Nimejiaminisha tu kwamba yupo
Mkuu Mungu akikupenda hukujaribu na dhiki

Mkuu hapa duniani ni mapito , muhimu ni mbinguni.
Itafaa nini usipate shida yoyote na ukaishie kwenye lile ziwa liwakalo moto?.
Mungu amtie nguvu kiumbe wake , amkumbushe tumaini pekee la kweli ni yeye?
Tumaini lisilo na mipaka sio kwa duniani bali daima na daima
 
Mkuu nami napenda kujifunza
Mbona kaacha kiumbe chake kitaabike hivi?
 
Kwa wachina, wana physiotherapy yao pale riverside wanajitahid, nina mdg wangu kapata nafuu japo bd
 
Msaaada jamani mwezi wa sita huu nimefanya matibabu ya kila aina,hospital paliponifilisi na mri scan,dawa za asili na kisuuna hadi maombi
Nakata tamaa sasa
Farao alipigwa pigo la kwanza hakusikia la pili mpaka pigo la saba .
Saa nyingine matatizo ni ishara ya Mungu kukushtua umkumbuke na kuikita imani zaidi kwake na kuweka matumaini kwake.
Kwa sasa mwambie Mungu ushazunguka kote na mwisho umetua kwake .
Jikabidhishe kwake , na ikiwezekana weka nadhiri kwake akikuponya uitimize,
Kuombewa sio kitu maana yeye hakusema ukaombewe.
Bali alisema ombeni nanyi mtapewa . Hivyo ni wewe kwanza kufungua moyo wako umwamini Mungu. Ukisha mwamini sasa peleka maombi yako.
Usisahau toba ni muhimu kuliko yote
Pili kumshukuru kwa kila kitu
Tatu leta maombi
Nne maombi ya imani shukuru na kuamini atakutendea hayo.
Kuwa na saburi na tumaini ya uzima wa milele kuliko ya kidunia .
 
CHIZI VITABU pole sana kwa masahibu unayopitia,naweka hapo chini namba ya simu ni doctor wa Kikorea anatibu kwa dawa za asili kutoka kwao na anatibu sana mambo ya viungo hasa mishipa ya fahamu na maradhi ya kupooza(stroke)mimi nimemfahamu kupitia kwa mtu alikuwa anamtibu mkewe kwake.

Mimi pia nina mtihani nina bwana mdogo namuuguza alikuwa anasumbuliwa sana na maumivu ya kichwa na mwili kupooza upande mmoja tumeenda hospital za serikali na privates akafanyiwa mpaka MRI maradhi hayakuonekana nikampeleka kwa huyu doctor dawa zake zikamsaidia maumivu ya kichwa yamemuisha na kule kupooza kumeacha ila limebaki tatizo kichwani anasumbuliwa na kelele asizojua zinatoka wapi,ni gharama sana kama utaweza ku-afford nakuomba ukajaribu huko

Pole sana Mungu akusaidie 065-436-3501
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…