Matumaini yangu mlio wengi humu ndani mlikua na weekend njema.
Ni miaka sita sasa tangu nimeoa na nimebarikiwa kua na watoto wawili. Kabla sijaoa nilikua nna marafiki wengi na bahati nzuri rafiki hao angalau wanajiweza wao wenyewe na familia zao. Namshukuru sana Mungu kwa ajili yao kwa sababu kwa namna moja au nyingine ndio walionifanya nibadili maisha ya kisela ya kibachela na kuamua nami niwaige kua na familia. Niliona kabisa nahitaji kufanya hivyo ili niendane nao.
Huyu mke wangu anawafahamu vizuri rafiki zangu hata kabla sijamuoa, ingawa kuna tabia alikua anaionesha ya kuchukia/kukasirika hasa nnapomwambia nipo na marafiki zangu au la pale anaponiona na marafiki zangu. Wakija kunitembelea nyumbani alikua anawapokea vizuri na anawachangamkia.
Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya kufunga nae pingu za maisha.
Anaonesha dhahiri kwamba hawataki rafiki zangu. Hataki waje nyumbani wala hataki mimi niende kuonana nao. Anataka nikitoka kazini moja kwa moja nyumbani, weekends anataka tushinde nyumbani tu. Akisikia hodi ya rafiki yangu yoyote atanuna siku nzima. Anasema wananiharibu, amesahau hao hao ndio walionifanya nimenunua kiwanja na kujenga nyumba, nilinunua gari kwa msaada wa rafiki zangu haohao. Vingi nilivyonavyo nimevipata kwa kua inspired nao.
Hata kumchagua yeye nimuoe, ingawa hajui lakini rafiki hao ndio walinishauri kwamba anafaa zaidi yeye kuliko wengine nilio kua nao. Hataki ndugu, hataki mtu yoyote mgeni zaidi ya rafiki zake au ndugu zake tu.
Kwa sasa rafiki zangu hao pamoja na kumtetea sana mke wangu, wameshagundua kwamba wanajibembeleza sana kuja kwangu. Wote wamekata mguu, imebaki mimi kuwatafuta lakini kila mmoja sasa hivi anaonekana anahamsini zake.
Furaha ya mke wangu ni kuniona mimi tu pembeni yake muda wote. Sina mawazo mapya sababu sijumuiki na wenzangu. Nimekua kama msukule sipati marafiki wapya na niliokua nao hawapo tena.
Hivi majuzi nimepata kibarua mkoani, nimepata angalu muda wa kuwapigia, lakini muamko wao si kama wa zamani.
Naombeni ushauri wenu, nyumba yangu kubwa lakini haivutii kabisa wala siipendi kwa sababu inasisi watu wazima wawili na watoto wawili ambao nao wanashinda shule. Muda mwingi ipo kimya kama wanga vile 😭😭