Nimepoteza uwezo wa kwenda shuleni kufundisha baada ya nishati ya mafuta kupanda

Nimepoteza uwezo wa kwenda shuleni kufundisha baada ya nishati ya mafuta kupanda

Mimi ni mwalimu
Kwa kupanda kwa nauli NIMEPOTEZA UWEZO wa kwenda shuleni kufundisha kwa siku mbili.
Naomba ushauri.
Ufafanuzi:-
Nauli ya bajaji ilikuwa sh 500/= kwenda,
Na sh 500/= kurudi.
Jumla sh 1000/= kwa siku.
Sasa nauli mpya ni sh 700/= kwenda,
Na sh 700/= kurudi.
Jumla sh 1400/=kwa siku.
Tofauti ya sh 400/= kwa siku.
Huwa naenda shuleni siku tano kwa wiki moja.
Ongezeko la sh 400/= kwa siku maana yake ni ongezeko la sh 2000/= kwa wiki.
Kwa gharama za zamani za sh 1000/=kwa siku
Ni wazi NIMEPOTEZA uwezo wa kwenda shuleni kwa siku 2 kaman nitalipa sh 1400/=kwa siku.
Hisabati
5000/1400=3....
(Siku 3)
Nyie walimu mnatakiwa mpigike hadi muwe na akili.
Mmewadhulumu Watanzania miaka nenda miaka rudi.
Majambazi na vibaka wa kura zetu.
 
Nyie walimu mnatakiwa mpigike hadi muwe na akili.
Mmewadhulumu Watanzania miaka nenda miaka rudi.
Majambazi na vibaka wa kura zetu.
Siyo kweli ingieni madarakani na msiwatumie walimu.
Walimu ni waaminifu kuliko uavyofikiri.
Unataka kuniambia wanaofaulu mitihani wote ni feki , na wanaofeli ndiyo wako sawa?
Usipomuamini mwalimu utamwamini nani?
Mkiingia madarakani chukueni wanaj.... wasimamie uchaguzi.
 
Nyie walimu mnatakiwa mpigike hadi muwe na akili.
Mmewadhulumu Watanzania miaka nenda miaka rudi.
Majambazi na vibaka wa kura zetu.
Yaani mkuu wewe umeongea unavyotakikana, waalimu hawa sio wa kuwaonea huruma, ni mbwa mwitu kwenye ngozi za kondoo, wanapiga piga kelele sasa baada ya kulambishwa pipi
 
Pole mwalimu. Anza kufanya mazoezi ya lazima ya kutembea kwa miguu. Utapata shida mwanzoni, lakini baadaye utazoea.
 
ulikosa kusema ccm ili uzi wako ukamilike maana mood wa JF ni ccm kindaki .
 
Haya ndio maisha, hii changamoto ya nauli inawakumva watu wengi. Tafuta suluhisho la haraka ili hali isiwe mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom