Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Utakuwa upo mbali sana kutoka usawa wa nchi, mbona huku ndani sasa hata tuliokua tunajua kumbe ilikuwa wajinga wa kutupwa. (Nchi hii haijawahi kuwa na mwizi, tapeli, laghai, muongo, na katili wa mfano wake)
Tulia wewe mtoto mdogo,Escrow,Meremeta,IPTL,EPA yalikuwa maigizo? Kama wewe sio dhalimu hauwezi kumchukia Magufuli na hiki ndio kipimo chake.
 
Mkuu kuwa mkweli, kwenye haya uliyoyaorodhesha ni lipi ambalo halikuwa tabia ya Jiwe? Bila kumwonea wala kumpendelea
Chuma alibeba jukumu la kuwanyoosha.Alitumia style gani au nani aliumia sisi watanzania tuliemchagua tulipendezwa na kazi yake hakuwa na huruma hata kidogo.

Mwwnyezimungu amrehu John wa Chato 🙏
 
Kama ulikuwa na tabia za wizi,utapeli na kuishi kwa ujanja ujanja mjini hakuna jema la Hayati JPM utakaloliona.
What about makonda na Sabaya? Maana walikusanya utajiri kipindi cha huyo mtu kwa njia ovu na hawakufanywa chochote, au hao walikuwa hawagusiki mkuu?
 
Hakua na sifa za kiongozi yule bali
sifa zote za Mtawala
 
Chuma alibeba jukumu la kuwanyoosha.Alitumia style gani au nani aliumia sisi watanzania tuliemchagua tulipendezwa na kazi yake hakuwa na huruma hata kidogo.

Mwwnyezimungu amrehu John wa Chato 🙏
Alitisha watu, but hakuwa better kama unavyosema hapa! Ila ameshakufa (Kaweka rekodi rais wa kwanza kufia madarakani), haya na tusonge Mbele sasa, harudi tena! miaka 9 ijayo tunaongozwa na Samia, inawauma baadhi ya watu ila hamna cha kufanya hahaha
 
Muulize Yule Mpare wa Oysterbay Makao na Yule Msukuma wa Upanga Makao kisha malizia na Daktari wake, Bibi Mmoja wa Kisiwani na Mswahili wa Pwani na Manesi Wawili wa Mzena.
Ila yule bibi wa kisiwani nahisi alikuwa mweupe kwenye hii ishu, alishtukizwa tu
 
Mkombozi aliyeunda Genge la wahuni na Majangili kama Sabaya, Musiba, Bashite, Mchungaji Mashimo etc
Atakuwa Mkombozi wa wahuni
Mbona hautaji wezi aliowashughulikia accordingly,wauza madawa ya kulevya,wapora rasilimali za nchi na waonevu wa wanyonge.Au umesahau wahuni kama wakina Papaa Msofe,Ndama na wahuni wengine ambao jela iligeuka kuwa mapumziko yao
 
Na bado hujalia siku ukipata mtu wa karibu nae akakusimilia kifo chake, utaenda chato mwenyewe kuona hata kaburi yake.

Siumii kwa nini amekufa maana kila mtu ataonja kaburi, kinachoniuma ni yale mazingira alokufa.
Mmhh kulikuwa kuna nnn kwani? Ata dm poa tu mi binafsi ndani kwangu kuna picha yake kwangu He was my hero
 
Naomba nikushauri kidogo: mtu yeyote akikujibu vibaya au kukutukana, achana naye; ilimradi kwenye bandiko lako hujatukana mtu yeyote bali umetoa mtazamo wako kwa staha na hoja.

Sisi wasomaji tunaojali maoni na utu wa mtu, tutajua nani anachangia au kukosoa kwa staha. Wajibu wanaokuheshimu na kukukosoa au kukushauri kwa heshima. Ukiona upumbavu wowote, mahali popote, mwachie mwenye nao!
 
Mkuu natamani niijue hiyo waallah ata uni DM tu
 
Mkuu Yesu alikufa akiwa na miaka 33,alianza ministry akiwa na miaka 30 akafanya kazi kwa miaka 3 peke ake haikuwa 32.
Magufuli alianza siasa akiwa na miaka kama 35 hivi sina uhakika na akafariki akiwa na miaka 61. Kwa nini Mungu alimwacha Magufuli miaka hiyo yote na akamchukua yesu mapema kama kifo ni adhabu itokanayo na kilio cha wanachi?
 
Mkuu hii nchi haitakuja kupata Rais kama JPM, ngoja tupambane na hali zetu kila mtu apiganie ugali wake.
 
Hv wale waliokuwa wakitekwa na kupotezwa walikuwa paka vle????au kwa kuwa co miongon mwa ndugu zako???
Kama ulikuwa na tabia za wizi,utapeli na kuishi kwa ujanja ujanja mjini hakuna jema la Hayati JPM utakaloliona.
 
Kwangu mimi JPM JPM alikuwa rais muuaji, mwenye chuki kali sana kwa wanamkosoa na kumpinga, mbinafsi aliyepitiliza kiwango cha kawaida na mungu mtu aliyependa kusujudiwa mpaka na nzi. MUNGU AMEWATENDEA HAKI WATANZANIA.
It's too early, with time you shall pick things that Magufuli could do best whilst many other Presidents can not. Politicians are crop of people who appreciate people who favour them or what they like.

Magufuli was pro people President hence few individualist would always suffer.
 
Na bado hujalia siku ukipata mtu wa karibu nae akakusimilia kifo chake, utaenda chato mwenyewe kuona hata kaburi yake.

Siumii kwa nini amekufa maana kila mtu ataonja kaburi, kinachoniuma ni yale mazingira alokufa.
Dada naomba unisimulie na mimi PM

Nilimpenda Mno JPM [emoji174].
Hadi Sasa nahisi kama ni ndoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa kuwa ndugu zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…