Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Nikweli ile roho ya uzalendo na uchapa Kazi aliyoijenga Magufuli imeondoka kabisa. Mambo yamekua Yale Yale, Uzembe umerudi kwa kasi yakutisha kabisa.


Mama anajitahidi kujitutumua lakini anazidiwa ujanja na michwa Ambayo ilizibwa pumzi kabisa na Magufuli.


Mbaya zaidi ni mama kupangua safu ya Magufuli Ambayo Angeitumia ingemsaidia sana kuongoza maana tayari safu ile ilikua imesha jua namna nzuri ya kupambana na majangili na wazembe kwenye SERIKALI.
Anakosea sana kuwatoa watu wenye weledi, uwezo, wasiokuwa na masihara.

Waziri wa maji, umeme na nishati, walifanya kazi kubwa sana. Wametupwa huko kisa walikuwa karibu na Marehemu.

Kiongozi mpya unabidi utumie uzoefu ulioukuta vizuri. Hakuna sababu kuanza upya na watu wapya wasio na uzoefu bila sababu za msingi.
 
Watu tutabisha tu ila kusema kweli Magufuli was a bold leader, ni aina ya viongozi ambao ni adimu kupatikana kutokana na kuwa na sifa za kipekee.....
 
Wasukuma mna tabu sana. Nani asiye na dini nchi hii ambaye alikuwa rais?
Unakosea sana kuleta ukabila. Kuna wasukuma waislamu, wakristo, maskini, wananchi wengi na wenye dini za asili.

Wengi wapo kwenye baraza la Mawaziri, walinzi wakuu wa rais.

Mlinzi mkuu wake ni huyo msukuma, tunafanyaje?

Kadi ya ukabila is a losing game in TZ.

Tunawabagua wasukuma, wanaume, watu wa Magufuli, wakristo, wapinzani.

Tunabaki na nani?
 
Binafsi nimeipenda style ya samia. Kwanza Ndani ya miezi 6 katoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu 7000 hii itachochea uchumi, ameanzisha ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya mia nne 400 unaendelea nchi nzima, anaendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake haijasimama ,ule wa SGR isaka mwanza ameuanzisha yeye, Juzijuzi ametangaza ujenzi wa madarasa elfu 15000 kwangu mimi hii ni hatua kubwa sana kwa miezi 6 sijui miaka mitano atafanya nini. la zaidi nchi ina amani na utulivu ingawa kuna kasoro ndogondogo. Huyu mama namkubali ingawa CCM siipendi
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, mradi wa SGR wa mwanza Isaka kuanzia mchakato wa zabuni mpaka mkataba wake umesainiwa Chato JPM akishuhudia, hata advance payment ya mobilization wamelipwa JPM akiwa hai, mama kaweka Jiwe la msingi how comes useme mradi kauanzisha mama?
 
Ni kweli hakuna ushahidi kwamba Maraisi wa Haiti, Tanzania, Ivory’s Coast, Eswantini, and Burundi waliuwawa kwa kukataa chanjo za COVID-19.

Marais wangapi duniani wamekufa kipindi hicho kifupi?

Ila wote waliokufa walikataa chanjo.
Mkuu, naona waongelea kitu kingine na mimi nimeongea kitu kingine kabisa.
 
Mkuu, naona waongelea kitu kingine na mimi nimeongea kitu kingine kabisa.
Nasema hivi wote walikataa chanjo, wote wamekufa kwa muda mfupi, kupitia vyanzo tofauti.

Dunia nzima inashangaa. Kitu kimoja kijachowaunganisha wote walikataa chanjo.

Wanasema za kuambiwa changanya na zako.

 
MKUU. Kama Taifa lingejua kwamba Ndugu Magufuli Angelala bila kumaliza muda wake basi tungepindua Meza kwa Maombi lakini tulifichwa mpaka mauti inamkumba mpendwa wetu.

Nikweli ile roho ya uzalendo na uchapa Kazi aliyoijenga Magufuli imeondoka kabisa. Mambo yamekua Yale Yale, Uzembe umerudi kwa kasi yakutisha kabisa.


Mama anajitahidi kujitutumua lakini anazidiwa ujanja na michwa Ambayo ilizibwa pumzi kabisa na Magufuli.


Mbaya zaidi ni mama kupangua safu ya Magufuli Ambayo Angeitumia ingemsaidia sana kuongoza maana tayari safu ile ilikua imesha jua namna nzuri ya kupambana na majangili na wazembe kwenye SERIKALI.
Jinga sana wewe, safu yenyewe ndio hawa kins Polepole na Bashiru?
 
Tangu mwaka uanze nahisi huu ni uzi wako wa maana kuliko zote.

Anyway binafsi jpm nillikuwa namkubali kawaida tu hasa nikiwa sehemu ya changanyikeni kama humu, nilikuwa simchukii kama wengine, kuna vitu alikuwa akifanya nasema huyu kweli rais hata kama sisem ila moyoni nasema hili jembe.

Siku niliposikia habari za kifo chake trh 9 nilisikia maumivu ambayo sikujua yametoka wapi.

Miliogopa hata kumwambia mtu yeyote maana alienihakikishia kafa alinitaka nifunge mdomo wangu.
Nilikuwa nikiingia humu nakuta watu wanachangia nyuzi kibao eti jpm yupo wapi na mimi najilazimisha kuchangia as if sijui kinachoendekea.
Pili moyo haukuamini nilichoambiwa nikawa akisemea ' huyu mbwa nae mwongo jpm atakufaje kizembe hivi?

Siku moja nikataka kumwambia mama yangu moyo ukasema hapana yupo hai yule fala mzushi.
Trh 17 usiku nikaota eti kafa nikastuka usingizini nikajisemea hapana ni nawazo yaliyo kichwani mwangu coz nishapewa hiyo habari wiki moja kabla.
Niliamka nikapiga magoti nikasali mikasema hii ndoto isiwe kweli, nikaingia jf nikakuta mtu kapost eti kwa nini wasitangaze tu rais kashakufa kha! Ndo niliamini yale maneno.

Baada ya kutangaza nilipata maumivu ambayo sikujua yametoka wapi, maana niliona Tanzania ambayo jpm alikuwa akiitengeneza ikiyeyuka.

Niliona ujinga ukirudi kwa kasi, wizi, miradi yake ikifa, nidham ya watumishi ikirudi 0, ufisadi nje nje , majambazi wakirudi kwa kazi, unyanyasaji wa wanyonge, viongozi kula mishahara ya bure,kupewa kazi kwa kujuana, vyeti feki,
Nikaona lile genge sugu la majambazi wanaotesa nchi wakifurahia kifo chake, nililia sana nikasema Mungu alitupa malaika ila wengi tulichukulia poa.
Huko ulipo jpm ulale salama, hakuna siku imepita bila kukukumbuka. Binafsi nimekumiss sana.

Rip jpm.
Mkuu huyu jamaa tulikua hatujui tu Mungu katupa kiongozi bora maaana alidili na majangili yaliyo kwapua mali za masiikini.Leo wanyonge ndo wameanza kukiona cha moto mambo ya kunyanyaswa yanarudi kwa kasi sana mara machinga huku bodaboda na vitu vinapanda bei wala viongozi huwasikii wanakemea wako kimya km hawapo vile inaumiza sana nikimkumbusha ngosha mwenzangu.
 
Pole sana mkuu, Binafsi Magufuli naamini ndiye Rais bora ambae aliiwaza Tanzannia ya miaka 2050, Magufuli alikuwa kiongozi sema Watanzania wengi wanataka wanasiasa.

Hii picha hapa chini iko ndani kwangu tena chumbani kwangu!

View attachment 1991351

umenipa idea mkuu,sijui kwanini sikuwa nayo mpaka sasa[emoji24][emoji24][emoji24]
 
bahati mbaya tutamkumbuka mzee tukiwa tunataabika sana.

wewe genta ulikwenda mbali mpaka kukosoa kiingereza,acheni twende na kiingereza sasa.
 
Asante kaka kwakuutambua ukweli nakuusema hadharani sometimes mihemko inatufanya tuwe species tofauti nawenzetu(other human race)na ndyo maana tubaendelea kuwa forever slaves mtu kiongozi Kama Magufuli alikataa kuwa mtumwa kwavitendo pongezi kwake mwendo ameumaliza
 
Nlitofautiana na mwendazake katika nkushindwa kuongeza mishahara kwa miaka yake yote aliyokaa madarakani..kwa Hilo hata aje Nani,.amtetee namna gan lakini sitoweza kumuelewa
 
Back
Top Bottom