Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
ebo!!! weeee kate vipi tena? ulinidanganya?
Hongera sana mamii.Wapwaz na Binamuz wote.
Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.
Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.
Nimewamiss si kidogo!!!Natafuta muda nionane na baadhi yenu.
With love
Regia
By the way NN FYI calabash pale yupo FLORA, muulize big braza ODM akupe 'habari yake'
Hata hao CCM pia wanaishi mijini. Akina Chenge. Karamagi, Nchimbi, Rostam na wengineo uwajuao wote wanaishi mijini. Huko majimboni kinachoweza kufanyika ni kujenga ofisi ya chama ya Wilaya au hata ya Kata na kuweka viongozi wa chama ambao wanaishi pale. Ndivyo mfumo wetu wa maisha ulivyo hapa Tanzania. Kwa hiyo unaposema wapinzani hawawezi kushinda kwa kuwa wanakwenda vijijini wakati wa uchaguzi tu, sio kweli.
Regia hajaenda Bahamas na Regia si fisadi. Mafisadi ni wabadhirifu wa fedha na mali na rasilimali za umma. Regia hayuko kwenye hiyo nafasi ya kuweza kuwa fisadi.
Regia kawakacha wana Kilombero? Ndivyo walivyokwambia hivyo au tena unasadiki?
Umejawa namadharau kupita kiasi!!!! Hujui mipango yake lakini unatoa hukumu kulingana na post zake za hapa. Au umemwuliza ukaongea naye kwa mapana na marefu kuhusu hiyo mipango yake na ukaona kuwa hana mipango?
Ingekuwa hivyo wala hata asingethubutu kuweka jina lake na familia yake kwenye mstari wa mbele ambako kuna kila aina ya visanga vikiwemo kejeli na dharau toka kwa watu kama wewe. Kajitosa, kagombea na haikwenda kama ilivyotarajiriwa kutokana na sababu mbalimbali za dhuluma halafu wewe unadiriki kusema anasubiri huruma za grand poobahs wa CHADEMA. Hapa mwombe radhi.
Sorry Safari. Beautiful imagery but it is "Glad you are back" and not "Glad your back". Mind your language.
Eliza yuko wapi?
Hongera sana Mpendwa Regia, Karibu tena
hahah..Askofu.....kwani alikwambia ako wapi....of course yupo ile 'baa nyingine' lol
...kama wewe unavyowafaham masista wa makanisa yoteInaonekana wahudumu wa bar zote unawafahamu
Inaonekana wahudumu wa bar zote unawafahamu
...kama wewe unavyowafaham masista wa makanisa yote
Kwani pale juzi ulikuwa unaita jina gani?
La Yesu
Flora na Asha wamegeuka Yesu siku hizi?
Wapwaz na Binamuz wote.
Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.
Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.
Nimewamiss si kidogo!!!Natafuta muda nionane na baadhi yenu.
With love
Regia
Mr/Mrs/Ms Kiranga, now u seem to be coming to terms with reality.....I must admit, it's quite some progress on your learning curve.This is no defense at all, basically ni kama mtu kashikwa anafanya kitu kibaya, halafu anajitetea kwa kusema "mbona na wengine wanafanya". If anything it is admission of wrongdoing.
Washtakiwa wa genocide ya Rwanda wakitoa utetezi wa kusema mimi niliua lakini nchi nzima iliua, hii defense itakuwa haina mantiki. Majaji watasema wewe ndiye tunakutaka tuwaonyeshe mfano wengine wote. Regia Mtema ni mgombea aliyepita wa upinzani, na mimi nawasema hawa wapinzani kwa sababu wao ndio walikuja under the banner of good governance na kuleta mabadiliko.CCM tunawajua, kuna wengine wetu wanafikiri CCM is beyond repair, ndiyo maana unaweza hata usinisikie kuongelea sana kuhusu CCM, lakini tukiwa tunaona uozo ule ule wa CCM kutoka kwa hawa wapinzani wanaosema wanataka kuleta mabadiliko tunapata mshtuko.
Unapouliza "sasa akikaa huko Kilombero una hakika kuwa atapata kazi ya kumuingizia kipato" unaonyesha kutoelewa kuwa tunachopigania katika mabadiliko ya uongozi ya taifa letu ni kikubwa kuliko kipato cha mtu mmoja. Na kama Regia Mtema naye ana mtazamo kama wako, then hii ina confirm suspicions za cynics kwamba hawa wanasiasa wanajiingiza katika siasa kwa maslahi binafsi tu.
Hivi Nyerere angeamua kujali kipato zaidi ya kujenga TANU wakati anafanya uamuzi wa kutaka kujiuzulu ualimu ili aweze kupata muda zaidi wa kufanya kazi za vyama na asiviolate code of conduct ya ajira yake ya ualimu, leo angekuwa na historia hii aliyoacha?
Hivi Barack Obama alivyo graduate from an Ivy League school, angeamua kukubali zile lucrative offers za kazi Wall St. ambazo zingemlipa mara nyingi tu kuliko mapato yake kama community organizer leo angekuwa na historia aliyonayo ?
Hivi Nelson Mandela angesema aangalie personal gains kutoka law career na asirisk kufungwa na kupoteza kipato historia leo ingekuwaje ? Angeweza ku achieve yote aliyoweza ?
Political achievements zinataka personal sacrifice, to whom much is given, much is required. Ukitaka wananchi wakuamini na kukupa dhamana ya uongozi, inabidi uwaonyeshe kwamba unafanya sacrifice zinazotakiwa kwa wao kukuamini hivyo. Nyerere, Mandela na Obama wote walishafanya sacrifices kubwa kabla hata ya kuwaomba wananchi kura, ndiyo maana walishinda bila matatizo.
Regia Mtema anafanya sacrifice gani? Au anataka dhamana ya uongozi tu, lakini hata sacrifice ya kuachia ofisi za viyoyozi za mijini hataki ?
Whether kaenda Bahamas, Dar au Morogoro mjini, kujinadi kama mdau wa Kilombero bila ya kuwa na primary domicile huko si fresh, na kuwakacha wananchi wa Kilombero wiki moja tu baada ya uchaguzi ili kurudi kwenye mitandao na viyoyozi is even worse.
Tofauti kati ya Kiranga na Regia Mtema ni kwamba, Kiranga hajawahi kugombea nafasi ya kutaka kuwawakilisha wananchi wa Kilombero, kwa hiyo hana haja wala wajibu wa kuwa karibu na watu wa Kilombero.
Lakini Regia Mtema ndiyo kwanza anatoka kugombea ubunge na ameonyesha kuwa mdau mkubwa wa watu wa Kilombero.
Wanaotaka dhamana kubwa kutoka kwa wananchi inabidi watuonyeshe kwamba wanafanya kazi kubwa na wananchi hawa, vile vile wasiotaka dhamana hata ndogo kutoka kwa wananchi hawa, watu kama kina Kiranga ambao hawana ndoto ya kugombea public office, hawana wajibu wa kuwa karibu na wananchi hawa. Wakifanya hivyo kwa matakwa yao ni sawa, lakini pia wana haki na uhalali wote wa kuingia katika spaceship na kwenda Andromeda Galaxy for all that we care.
You can't eat your cake and have it still. Huwezi kujinadi kama mdau mkubwa wa watu wa Kilombero, halafu uchaguzi ukiisha wiki moja tu unajitoa Kilombero na "kurudi" mjini kwenye uafadhali wa maisha. Kama unaishi kwenye uafadhali huu wa maisha utapata wapi uchungu wa kudai uafadhali huu wa maisha wa mjini ufike vijijini?
Ndiyo maana vijijini hakuendelei, wabunge wote na wapinzani wao wako mijini, wanaenda vijijini nyakati za chaguzi tu.