Nimerudi salama-Niliwamiss sana

Nimerudi salama-Niliwamiss sana

Status
Not open for further replies.
Karibu mamaa ya shoka.
Tupo pamoja, tutapeana coordinates kwa ajili ya kukupongeza. Wewe ni mshindi na sisi tunajua hivyo!
 
Karibu mamaa ya shoka.
Tupo pamoja, tutapeana coordinates kwa ajili ya kukupongeza. Wewe ni mshindi na sisi tunajua hivyo!
jumatano tutakutana.............!

regia mwenyewe nadhani anaelekea kanda ya kati kesho(dodoma)!

kesho na jumatano tutaijadili kwa kina safari yetu ya kwenda dodoma
 
Wapwaz na Binamuz wote.

Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.

.............................

Hongera sana Regia .Ingawa the end result siyo uliyotegemea naamin milestone ulizoaachive this time zitakusaidia na zitaisaidia CHADEMA next time.

Ebu tukumbushe mchangamanuo wa kura zako na na za washindani wako.
 
Regina you put a great fight. Upo mioyoni mwa wana Kilombero na moyoni mwangu. Mungu awe nawe na akutangulie kwa kila utakalolifanya
 
Big up mama, Umezihirisha tena kuwa akinamama/dada mnaweza!
 
Gender Sensitive, you had a courageous fight but they stole the election from you!! All the same with time mjengoni utaingia! Keep hope alive.!
 
Hongera sana dada, umekuwa mfano kwa akina mama wengine na nina imani wengi watajitokeza katika chaguzi zijazo ili kukuunga mkono!
 
Dada Regia ............Iam really honoured cant say more........... Karibu sana Jamvini na tambua kuwa TUPO pamoja. Sie tunajua kuwa umetuwakilisha vizuri na unastahili kupongezwa kwa ujasiri wako kwanza wa kujitoa...sisi hatusemi tumeshindwa lah bali tumekosa ushindi kwa style yetu..... tufunge mkanda na kujifunza kutokana na yalotokea katika uchaguzi wa Mwaka huu ili 2015 tusifanye makosa kwa kuyarudia yaliotukosesha ushindi mwaka huu.
 
Ndugu zangu wapenzi,nipende kuchukua fursa hii kuwashukuru wote mlionikaribisha tena kwa moyo mmoja na kunitia moyo.Asanteni sana na MUNGU awabariki sana.

Wish you all the best.

With love
Regia
 
Unajitahidi sana, lakini unavyozidi kujitahidi ndivyo unazidi kujiadhiri.

Actually speed in the wrong direction is very relevant. Because the more you move in the wrong direction the further away from the right destination you get. One must always head in the right direction.

Na hapa Regia amekuwa na speed in the wrong direction. Badala ya kuzama zaidi Kilombero na kuwajua zaidi wananchi wa Kilombero, yeye wiki moja tu baada ya uchaguzi kawakimbia.

Speed in the wrong direction, very relevant.

we chizi i mean mwehu, mpaka akaamua kugombea kilombelo maana yake anawajua fika huko, na kuamua kurudi wiki moja baada si dhambi, ataenda tena kilombero na tena na tena kama ilivyokuwa kawaida yake huko nyuma, na suala la kuimarisha chama amelifanya miaka yote huko kilombero na ndo maana akapata ushindi mkubwa ulioibwa na ndugu zako wa ccm (maake kwa ninavyosoma post zako)..na si lazima eti muda huu baada tu ya uchaguzi basi ndo alitakiwa abaki aimarishe chama, anafanya kutokana na aonavyo yeye na si uonavyo wewe mwehu, na ndo maana alivoenda kugombea ubunge alitoa kama taarifa kwa watu na si kuomba ruhusa kwa sababu suala la kumruhusu agombee lilikuwa la chama chake na wananchi wa kilombero....we kiranga kweli kiranga....ni mwehu wa kutosha kabisa
 
Hii concept nzima ya "kurudi" kutoka Kilombero mimi napata tabu nayo sana. Inaonekana Kilombero -pamoja na majimbo mengine ya vijijini- ni sehemu za kwenda wakati wa uchaguzi tu, uchaguzi ukiisha watu wanarudi kwenye shughuli zao za kawaida mijini.

Badala ya wagombea walioshindwa mwaka huu kubaki huko vijijini kuimarisha vyama vya upinzani, kuisadidia jamii pamoja na kupanga mikakati ya kushinda hivi viti katika uchaguzi ujao, tunaona increasingly "wanarudi" mijini.

Wapinzani wakiendelea kushindwa katika kila chaguzi zijazo watashangaa kweli kwa mwendo huu wa kwenda majimboni nyakati za chaguzi tu, na chaguzi zikiisha wanarudi mijini kwenye mitandao na urahisi wa maisha ?

Tunawatendea haki wananchi kweli kwa mwenendo huu ?[/QUOTE

Kakwambia haendi tena??


we kweli ni mwehu.....nadhani hujamaliza dawa zako za ugonjwa wa kichaa ulokuwa unaugua kwa muda mrefu sasa..
 
Ndg Kiranga mbona umemkomalia sana dada yetu! Hayo mambo ya Kilombelo anayajua saana. Inatakiwa Offisi ya chama husika ipange mikakati ya kutoa ushauri na kupambana kwenye majimbo husika si Kilombelo pekee. Tunahitaji kujipanga na kuangalia nini la kufanya ili tuwe karibu saana na wananchi pote Tanzania. Maandalizi ya 2015!

Mpaka hapo hongela sana kwa ujasili ulio onyesha wa kuthubutu, mambo mengine tafuta ushauri wa kisheria mbona kina Mabere Marando wapo.
HONGERA SAANA WATU KAMA WEWE NI WAKOMBOZI WA JAMII.
 
Hongera sana Regina na karibu home. tunashukuru kuwa umerudi in one piece, well and sound, that is the most important thing.
 
Maisha lazima yaendelee, lakini si lazima yaendelee mjini tu, hususan kwa watu waliotoka kujinadi kama wadau wakubwa wa maendeleo ya watu wa majimbo ya vijijini.

Wabunge wote pamoja na wadau wengine wanaojinadi kuwa au kutaka kuwawakilisha wananchi wa majimbo ya vijijini inawabidi wawe wakazi wa huko huko vijijini, sio mnawapelekea wananchi wagombea ubunge watalii ambao hata wananchi hawawajui. Na wakishindwa uchaguzi wiki moja tu wanakitoa "kurudi" mjini kwenye viyoyozi wakisubiria uchaguzi ujao.

Naelekea kukubaliana na Kiranga. Mojawapo ya mambo yaliyomwangusha Batilda Buriani hapa Arusha yalikuwa maelezo ya wapinzani wake ambayo wananchi waliyakubali, kwamba Batilda hakai Arusha mjini kwa hiyo hana hisia za kweli kuhusu shida za Arusha, kwamba hata akishapata ubunge atarudi Dar kwenye shughuli zake, na kwamba ati wakati wakazi wa Arusha wakiteseka na ujenzi holela na miundombinu mibovu ya usafi wa mazingira, Batilda atakuwa amepumzika kwao Zanzibar na mumewe wakipunga upepo ufukweni.

Ni kwanini tunawachagulia watu wa vijijini wagombea kutoka mijini, je hii si dharau kwa watu wa vijijini? Watu wanatoka Dar kwenda kugombea Karagwe, Tunduru nk kama vile huko hakuna watu? Nimewahi kumsikia mbunge wa jimbo moja la mkoa wa Singida akichangia hoja bungeni ambapo alilalamikia foleni ya magari barabara za Dar es salaam, wakati jimboni kwake watu wanatumia punda kubebea mazao kwenye barabara za vumbi vichakani! Anazungumzia adha za Dar maana ndiko anakoishi. Hili nadhani linapaswa kutazamwa kwa umakini zaidi ili kupata uwakilishi halisi zaidi kuliko sasa ambapo wengine wanapata wabunge wa 'kukodi' kutoka Dar!
 
pole sana Dada - yaani natamani nikuone LIVE - next time ukienda kuongea na wanachi wa pale ni PM nikupe company - usiogope mafao ya chakula, usafiri - nitakuwa nayo sitakuwa mzigo kwako

again BLESSINGS - pumzika kidogo Dar halafu jipange upya - "yote yawezekana kwake aaminiye"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom