Nimesababisha depression kwa mtoto wa watu

Nimesababisha depression kwa mtoto wa watu

Habari za jioni wapendwa.

Mimi ni mtumishi wa afya katika moja ya hospitali zilizoko jiji la Makalla. Mwanzoni mwa wiki iliyoisha alikuja mrimbwende mmoja kumuuguza rafiki yake aliyekua kalazwa hospitalini kwetu.

Nilimwelewa sana huyu mlimbwende nikajisemeha huyu mtoto siwezi muacha hivihivi. Nilipambana mpaka nikapata namba, tukaanza wasiliana, nikamtemea mistari akajaa. Tukakubaliana weekend ya jana jpili aje kunisalimia magettoni ( kumchakata). Japo nilimgusia swala la kupima afya zetu akakubali bila ubishi.

Sasa jana mtoto katimba nikamkaribisha vizuri magettoni, story mbili tatu hivi, baadae nikamuuliza tunaweza kucheki afya zetu akakubali nikatoa vipimo na kuanza kumpima yeye kwanza. Majibu yalitoka yenye mkanganyiko, kipimo kilisoma kwenye T na C ikabidi nitulie baada ya muda nikarudia tena na majibu yakaja kama ya kwanza. Nilitumia ORAQUICK HIV SELF-TEST.

Kiukweli stimu za kumgegeda zilikata nikabaki tu nampigisha story. Japo alianza kulia pale nikambembeleza akatulia. Nikamwambia majibu si kwamba una HIV bali unahitaji kipimo cha kutumia damu. Nikamshauri akiwa tayari anaweza kwenda kituo cha afya karibu yake au akaja napofanya kazi tukamcheki zaidi.Alinyong'onyea sana mpaka nikajuta kwann nilimpima.
Aliondoka akiwa mnyonge sana.

Leo nimeongea nae kashindwa kwenda kazini mawazo yamemjaa na hukula toka asubuhi, imebidi jioni hii ninunue msosi na kumpelekea anapoishi. Kwa sasa naondoka narudi magettoni lakini sina amani, amejawa na mawazo sana japo nimemshauri vya kutosha kwamba majibu hayakuonesha kwamba ana HIV lakini imekua ngumu kwake kuelewa. Naogopa asije fanya maamuzu mabaya, mbaya zaidi anaishi mwenyewe.
NIKOSA AMANI JUU YA HUYU BINTI WA WATU.

View attachment 1818882
We ni mshamba sana kwanin usitumie kondomu, unapima na mtu pale unapotaka kua na malengo nae
 
Kwanini uliharakisha kupima? Unataka kumuoa ama kula na kusepa? Mwanzoni ungetumia mpira kisha huko mbeleni ndio mnapima..
Muongo huyu, atakua alikutafunna! Hakunaga kitu kama hicho labda kama "mnara" unakamata network kwa shida
 
Shadow7 Kama UKIMWI haupo, hiki kilichopo sasa ni kitu gani? Deception . Nitagini hiyo sehemu mnapoongelea suala hilo nami nijue hoja yenu.
Kwenye Huo uzi hakusema kuw hakuna Ukimwi, bali hakuna HIV anayesababisha Ukimwi ( upungufu wa kinga mwilini).. akaendelea kuandika ukimwi unasabbishwa na mambo mbali mbali kama matumizi ya antibiotics kwa muda mrefu, ukoesfu wa antioxidant, malnutrition na nk. Na kuwa upungugu wa kinga mwilini hauwezi kumuambukiza mtu mwingine upungufu wako.....

Endelea kuufuatilia huu mjadala
 
Back
Top Bottom