Nimesamehe ila nashindwa kusahau

Nimesamehe ila nashindwa kusahau

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2007
Posts
9,346
Reaction score
3,028
Hamjambo wakuu?
Mimi ni mke wa mtu. tuko pamoja sasa miaka 3 ila mwaka huu mwamzoni tulienda likizo home town kwao na niligundua kua mume wangu alienda party na mpenzi wake wa zamani. Mimi alinambia kua ameenda safari ya siku 2 ila mwenye party alinitumia picha za party na nikamuona amekaa na ex wake huyo wanacheka.
Nilipo muuliza alinambia maneno mengi ila akaomba msamaha na nikaamua kusamee na kuendelea na mapenzi yetu.
Ilikua ni mara ya kwanza ananifanyia hivo na kusema kweli naamini hakuendelea.
Tatizo ni kwamba hata kama niliamua kumsamehe nashindwa kabisa kusahau. Kila nikikumbuka nalia sana na tunaishia kujiskia vibaya, yeye kama mimi. Ananiomba tena msamaha na nikimwambia yamesha pita haamini. Sina hasira yoyote na sijawahi mlipiza kwa namna yoyote, sema tu najiskia vibaya sana na naogopa kosa lake lile litakuja kutia sumu katika mapenzi yetu.
Jamani nisaidieni. Nifanye nini ili uchungu upotee na mume wangu aamini kua kweli nimesha samehe?
 
Unamwitaje mwanamke mwenzio demu!?Hata hivyo huwezi jua labda anaenda nae kwenye party na sherehe kwasababu yeye ni “demu“.
 
Unamwitaje mwanamke mwenzio demu!?Hata hivyo huwezi jua labda anaenda nae kwenye party na sherehe kwasababu yeye ni "demu".
Sasa demu si kiswahili cha dame ambayo ni mwanamke tu?
 
Kuna kosa moja kubwa sana unalifanya shem. Inaonekana unamwamini huyo mwanaume kuliko navyotakiwa kuaminika binadamu. Utakuja jinyonga siku ukithibitisha katembea nje ya ndoa.

Nakushauri muamini, lakini jua kama binadamu ana 'haki' ya kukosea kwani binadamu tumeumbwa na udhaifu fulani...
 
Na kushauri kwa usalama wa mahusiano yako jitahidi kutomuhusisha huyo jamaa yako unayo kumbuka.
unampa muda mgumu sana na anaweza akachoshwa na gubu hilo .

So jaribu kutafuta sehemu ndani yako na lifukie hilo once and forever.
Mwanamke unatakiwa kuwa mvumilivu na jasili
 
dada kama wampenda mumeo na wataka kuendelea kumuamini basi nakuomba usimfuatilie kwani utakufa siku ukimbamba ana kazi ya nje.
we faidi utamu wa nyama ya bata...usimfuatilie bata maisha yake.
 
Forgive and forget,..............thats how we live baby
 
Kuna kosa moja kubwa sana unalifanya shem. Inaonekana unamwamini huyo mwanaume kuliko navyotakiwa kuaminika binadamu. Utakuja jinyonga siku ukithibitisha katembea nje ya ndoa.

Nakushauri muamini, lakini jua kama binadamu ana 'haki' ya kukosea kwani binadamu tumeumbwa na udhaifu fulani...
Kaka najua na naelewa binadamu tumeumbiwa na kasoro na ndio maana niliamua kusamahe kosa lake sababu hat mimi sijakamilika kwa mambo mengine. Na kama nilikubali kua na mume wangu ni sababu namuamini. ikiwa imani hiyo itapotea basi itabidi nifikirie upya uhusiano wetu. Siwezi sema kwa aasilimia 100 kua hawezi cheat (hata yeye hawezi jua) ila nina uhakika kwa kiasi fulani he is trust worthy. Tatizo ni hilo kovu, linauma kama donda...
 
Unahitaji kupata msaada wa maombi pamoja na ushauri nasaha ili uweze kusamehe na kusahau
 
Eti ehhh??Vizuri unaelewa hivyo maana hata wewe huko kwenye party mumeo hua anakuita demu!
Madame... Mademoiselle....., Madam...... wabongo wanafupisha demu
Actually kuitwa Madam ni heshima kubwa sana kama vile kumuita mtu Lady
 
Kama swali ni Je naweza kusahau....Jibu ni hapana... na kwanini usahau sababu kama unaomba kuwa na uwezo wa kusahau vitu naona unaomba ugonjwa
 
Hujasamehe bado
Kwa nini unasema hivo? nilivo kua na hasira nilifikiria kufanya kitu ili na yeye aumie kama nilivo umia ila nikaona two wrongs don't make a right na nikaamua kusamehe. Nilivo samehe nikawa sina hasira tena na mapenzi yangu kwake, trust na ukaribu vyote vikarudi pale pale. Haikua instant na kuna wakati hasira ilirudi tena ila leo nahisi kama nimesamehe kweli... tatizo ni kwenye kusahau sasa. Kwa maana nyingine nataka nikikumbuka yalio tokea nisisikii maumivu yoyote sababu yamesha pita... Nisaidieni jamani.
 
msamehe tu dear.lzm kujifunza kupokea kila hali,hawa watu wanakuaga kama watoto smtymz.yaan kama unawatoto kunajinsi watoto wanadanganyaga unamwangalia mtoto unamuonea huruma unamuacha.cha msingi angalia kama bado anakupenda na kama hajabadilika na kama kaomba msamaa plz msamehee na puuzia.huyo mwingine hatakama ni ex lkn ww ndo ulikua best ndo maana uko ndan bwana.
 
hujasamehe, ndo maana una kinyongo, na ukiwa na kinyongo namna hyo utakufa kwa presha. Maana wajua ni 'safari' ngapi za namna hyo amefanya?

Just forgive n forget, 'baadhi' ya wanaume ndo walivyo. . Kwi!
 
Hamjambo wakuu?
Mimi ni mke wa mtu. tuko pamoja sasa miaka 3 ila mwaka huu mwamzoni tulienda likizo home town kwao na niligundua kua mume wangu alienda party na demu wake wa zamani. Mimi alinambia kua ameenda safari ya siku 2 ila mwenye party alinitumia picha za party na nikamuona amekaa na demu wake huyo wa zamani wanacheka.
Nilipo muuliza alinambia maneno mengi ila akaomba msamaha na nikaamua kusamee na kuendelea na mapenzi yetu.
Ilikua ni mara ya kwanza ananifanyia hivo na kusema kweli naamini hakuendelea.
Tatizo ni kwamba hata kama niliamua kumsamehe nashindwa kabisa kusahau. Kila nikikumbuka nalia sana na tunaishia kujiskia vibaya, yeye kama mimi. Ananiomba tena msamaha na nikimwambia yamesha pita haamini. Sina hasira yoyote na sijawahi mlipiza kwa namna yoyote, sema tu najiskia vibaya sana na naogopa kosa lake lile litakuja kutia sumu katika mapenzi yetu.
Jamani nisaidieni. Nifanye nini ili uchungu upotee na mume wangu aamini kua kweli nimesha samehe?

Kwa hiyo red umenikosesha hamu ya kuchangia. Wewe ni mwanamke kweli unamwita mwanamke mwenzio DEMU????Kha napata mashaka kama wewe ni mwanamke unatabia chafu sana
 
Madame... Mademoiselle....., Madam...... wabongo wanafupisha demuActually kuitwa Madam ni heshima kubwa sana kama vile kumuita mtu Lady
Haya hongereni kwa mnaojua kifaransa!Wengine hatukuvuka darasa la saba!
 
Back
Top Bottom