Zero One Two
JF-Expert Member
- Sep 16, 2007
- 9,346
- 3,028
Hamjambo wakuu?
Mimi ni mke wa mtu. tuko pamoja sasa miaka 3 ila mwaka huu mwamzoni tulienda likizo home town kwao na niligundua kua mume wangu alienda party na mpenzi wake wa zamani. Mimi alinambia kua ameenda safari ya siku 2 ila mwenye party alinitumia picha za party na nikamuona amekaa na ex wake huyo wanacheka.
Nilipo muuliza alinambia maneno mengi ila akaomba msamaha na nikaamua kusamee na kuendelea na mapenzi yetu.
Ilikua ni mara ya kwanza ananifanyia hivo na kusema kweli naamini hakuendelea.
Tatizo ni kwamba hata kama niliamua kumsamehe nashindwa kabisa kusahau. Kila nikikumbuka nalia sana na tunaishia kujiskia vibaya, yeye kama mimi. Ananiomba tena msamaha na nikimwambia yamesha pita haamini. Sina hasira yoyote na sijawahi mlipiza kwa namna yoyote, sema tu najiskia vibaya sana na naogopa kosa lake lile litakuja kutia sumu katika mapenzi yetu.
Jamani nisaidieni. Nifanye nini ili uchungu upotee na mume wangu aamini kua kweli nimesha samehe?