Nimeshangaa eti vikao vya Bunge vinaendelea ilihali hayupo anayejali

Nimeshangaa eti vikao vya Bunge vinaendelea ilihali hayupo anayejali

Mchana wa leo rafiki yangu ambaye ni msaidizi wa kigogo fulani nimeshangaa ananiaga eti anatakiwa kupanda flight kuelekea Dodoma boss wake ametakiwa na Bunge kwenda kutoa maelezo kwenye Kamati mojawapo ya Bunge kuhusu sintofahamu ihusuyo shamba la mwekezaji kule Rukwa.

Wallah kwanza sikufahamu kama vikao vya Bunge vinaendelea.

Pili nimejiuliza kwa nini Bunge la sasa halina mvuto kabisa!?
Bunge la sasa sawa na kutoa hela mfuko wa kulia unahamishia kushoto.
 
Hivi kutokana na maendeleo ya teknolojia kwa nini vikao vingine vya bunge visikae kwa njia ya 'zoom meeting' kwenye maeneo Yao ya majimbo kuliko kukaa miezi kadhaa kulipana posho lukuki. Kukutana Dodoma kuwe kwa vikao vya majumuisho.
 
Mchana wa leo rafiki yangu ambaye ni msaidizi wa kigogo fulani nimeshangaa ananiaga eti anatakiwa kupanda flight kuelekea Dodoma boss wake ametakiwa na Bunge kwenda kutoa maelezo kwenye Kamati mojawapo ya Bunge kuhusu sintofahamu ihusuyo shamba la mwekezaji kule Rukwa.

Wallah kwanza sikufahamu kama vikao vya Bunge vinaendelea.

Pili nimejiuliza kwa nini Bunge la sasa halina mvuto kabisa!?
Hata mimi sikujua kama bunge linaendelea na vikao, kiherehere chako ndo kimesababisha nijue
 
Kiufupi wananchi hawana imani na bunge la sasa
 
Kwani Mpina yupo au bado anatumikia adhabu?
Kama yupo niambieni ili lau na mimi nifuatilie bunge
 
Mchana wa leo rafiki yangu ambaye ni msaidizi wa kigogo fulani nimeshangaa ananiaga eti anatakiwa kupanda flight kuelekea Dodoma boss wake ametakiwa na Bunge kwenda kutoa maelezo kwenye Kamati mojawapo ya Bunge kuhusu sintofahamu ihusuyo shamba la mwekezaji kule Rukwa.

Wallah kwanza sikufahamu kama vikao vya Bunge vinaendelea.

Pili nimejiuliza kwa nini Bunge la sasa halina mvuto kabisa!?
Wale amsha amsha wa bunge lililopita muliwaondoa kwa hila, mmebaki wenyewe mbogamboga, no one is interested. Tunamisi sana bunge la akina Zitto, Lissu, Mnyika, Heche, Sugu na wale wa CUF. Lilikuwa la moto sana.
 
Hivi yule Mohamed uliyemtaja bado yupo hai ?
Mtu wa Shagihilu 😂
Yule ni wa palepale Ndoleleji, Shagihilu alikuwa anaenda kuswali kwa sababu pale Ndoleleji hapakuwa na Msikiti wakati ule.

Sina hakika na uwepo wake, japokuwa hadi 2015 yeye ndiye alikuwa Diwani wa Kata ya Shagihilu kabla ya kugawanywa kuwa Kata mbili yaani Kata ya Shagihilu na Kata ya Ndoleleji.
 
Okay , !
Kumbe alikuwa ni wa pale pale Ndoleleji !Sisi tulikuwa tunakula sana Maandazi pale Iddisa on our way back home Masanga Uduhe 😂☕👍
 
Same here 😂 I didn't know about parliamentary sessions
 
Bunge la 2020 - 2025 limekosq mvuto kabisa na hata wenyewe Wabunge wanaelewa hivyo.
 
Mkuu bunge lipo linaendelea na ni Zuri tu....likiongozwa na mwanamama makini kabisa,..
Tanzania kwa sasa haina bunge. Kuna wahuni ambao hawakupigiwa hata kura na wananchi, wakapora mamlaka ya wananchi, sasa wahuni hawa wanajiita ni wabunge

Hakuna mtu mwenye akili ana muda nao maharamia hawa. Ndiyo maana mleta mada, ambaye ninaamini ana akili na ana dhamira njema na nchi yake, hakyweza kujua kama hao wahuni bado wanaendelea na vikao vyao vya kuhalalisha malipo yao haramu. Hata mahakama kuu, japo haipo huru, lakini kwenye hili ilithubutu kitamka wazi kuwa hao watu siyowabunge.

Hawa tuwaone kuwa ni majizi, sawa kama wale wanaoripotiwa kila mwaka na CAG.
 
Hivyo vikao vya CCM watanzania washaachana navyo kitambo saana.
 
Wananchi wamekosa Imani na bunge, hasa pale wanapowatuma wabunge wao waende wakajadili hoja za msingi, mfano hoja juu ya utekaji na kupotea Kwa watu wakiwemo watoto lkn hiyo hoja inapigwa chini na spika, sasa sijui wanaitaji kujadili Nini chenye tija Kwa wakati tulionano.
Mwisho wa siku Wenye bunge lao wanalipotezea...
 
Next election kikweli vema vyama pinzani viweke watu makini wagombee ubunge ili kuamsha amsha bunge kwa hoja za maana hasa zile zinagusa wananchi..wale wataotumia mda wao kuchimba facts zinazohusu wananchi, na maovu ya watawala..tume ya uchaguzi isilete yale mambo ya 2020 ili wajae ccm bungeni..ule ulikuwa ni udhaifu mkubwa..this time waruhusu mseto penye nguvu ya upinzani basi tuwaone wapinzani..penye nguvu ya ccm basi tuone ccm..kazi iwe bungeni. Urais ni obvious ccm wanakuwa na wigo mpana kuliko wapinzani..
 
Back
Top Bottom