Uchaguzi 2020 Nimeshangaa Magufuli kusema ameongeza mishahara kwa watumishi wa Serikali kimya kimya miaka yote mitano

Uchaguzi 2020 Nimeshangaa Magufuli kusema ameongeza mishahara kwa watumishi wa Serikali kimya kimya miaka yote mitano

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,742
Reaction score
3,224
Akiwa mkoani Mara Mgombea wa CCM Dkt John Magufuli kwenye uzinduzi wa kampeni katika mkoa huo Mgombea amesema kuwa "naskia kuna mtu anasema sijaongeza mshahara watumishi wa umma ,Watumishi wa umma nimewaongezea mshahara kimya kimya "
Aliendelea na kusema kuwa ukipandisha madaraja huongezi mishahara ,ukipunguza PAYE sio kuongeza mishahara.

Ndugu zangu kupandishwa daraja ni haki ya mfanyakazi/mtumishi wa umma na automatic mtu akipanda daraja (scale ya mshahara inaongezeka pia) kwanza wewe hautakuwa wa kwanza kuingia daraja hilo..swali la kujiuliza je waliokutwa kwenye daraja hilo waliongezewa mshahara.

Je, kupunguza kodi kwenye mshahara wa mfanyakazi ni kuongeza mshahara ,hiyo ni sawa na mwezi avunje penseli kutoka mfuko wa kulia na kipande kingine aweke mfuko wa kushoto halafu aseme nina penseli mbili.

Magufuli tafadhali usituchonganishe na ndugu zetu wanaotutegemea. Kuna muda unajisahau unasema mkinachagua tena nitaongeoza mishahara muda huo huo unasema umeongeza kimya kimya. Watumishi wa umma unaosema umewaongezea mshahara wanafanya kazi nchi gani?

Wewe si ulisema unajenga mastandard gauge na madaraja na unanunua mandege tupande.

Wewe si ulisema tufanye kazi tuache tamaa ya kuongezewa mishahara.

Wewe si ulisema unafanya uhakiki wa Watumishi hewa.

Wewe si ulisema hautoongeza mshahara hauna hela ya kuchezea.

Mh. omba kura achana na propaganda zako za kusema ukipandisha mshahara kwa kutangaza kutatokea inflation hoja za kitoto..enzi za JK alikuwa anapandisha mishahara mbona vitu havikuongezeka bei...kwan hujui policy za ku-control inflation.

Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Jiwe amejijenga katika misingi ya uongo, hatujawahi kuwa na Rais Muongo kiasi hiki.

i.Jana tu amesema hawakuweza kuwapitisha makongiro na mdogo wake kisa walipata kura 5 na2.Mbona patrobas walimpitisha.

ii.Juzi amesema maendeleo hayana vyama alafu jioni akasema msimchague mpinzani hata kama anafaa.

iii.Bungeni alisema ameajiri watu M8.

iv. Ahadi ya milioni 50 kila kijiji.

V.Tanzania ya viwanda.

Vi. Kuk
 
Nakumbuka mwaka 2019 alisema kwenye mazimisho ya siku ya wafanyakazi ataongeza mshahara kabla ya miaka yake mitano kuishi kwaiyo wafanyakazi wamvumilie kwasababu miaka yake bado

Mwaka huu nadhani ndio wafanyakazi walikuwa wanasubiri kuongezewa mshahara lakini siku ya wafanyakazi akukuwa na mazimisho alitoa waraka tu wa kuwatakia wafanyakazi mazimisho mema akakaa kimya huo mshahara kaongeza lini anasema kapunguza kodi ya mshahara

Vipi kwenye makato ya mkopo wa chuo kikuu alivyoingia ulikuwa % na amepandisha % ngapi kwa kweli ni vile tu basi ila magufuli miaka 5 imemtosha kabisa
 
Akiwa mkoani Mara Mgombea wa CCM Dkt John Magufuli kwenye uzinduzi wa kampeni katika mkoa huo Mgombea amesema kuwa "naskia kuna mtu anasema sijaongeza mshahara watumishi wa umma ,Watumishi wa umma nimewaongezea mshahara kimya kimya "...
Kama hoja ndivyo zinajengwa hivi, basi athari za "missing gap" ya Mzee Mkapa ni kubwa mno. Maskini CCM pumzi imekata mapema sana. Hivi ni kweli watumishi wa umma waliopigika kwa miaka mitano mfululizo unaweza kuwapa matumaini mapya kwa kauli kama hii?
 
Mkuu inaonekana wewe hujasoma hesabu na hujui hesabu. Kitendo Cha kushusha thamani ya "PAYE" Kutoka 15% mpaka 9% lazima pesa itapanda na ukipandisha na mshahara utashukwa pia.

Mathematically; Makato ya mshahara (PAYE) is inversely proportional to the salary.
So the decrease the paye the increase the salary.
 
Jiwe amejijenga katika misingi ya uongo,hatujawahi kuwa na Rais Muongo kiasi hiki. i.Jana tu amesema hawakuweza kuwapitisha makongiro na mdogo wake kisa walipata kura 5 na2. Mbona patrobas walimpitisha...
Computer na laptop kila mwalimu.

Nyie hamuoni maendeleo yanawapita huwezi kumlisha mtoto wa jirani ukamuacha mtoto wako..sijui Bunda iko Kenya.
Kunbe Magu yupo empty kichwani hivo yan usipeleke maendeleo kisa upinzani.
 
Back
Top Bottom