Wadau hamjamboni nyote?
Niombe moderator uache Uzi huu ujitegemee wenyewe tafadhali
Sio lengo langu kubeza au kukashfu ila navyojua ratiba za mbinguni kwa maana ya siku, mwezi na mwaka hilo husalia kuwa siri ya mbingu
Pale mwanadamu anapojidai kujua ratiba za Mwana wa Mungu akiwa hukoo mbinguni ni jambo la kushtusha na kuogofya
Tafakuri ya kina kwa wenye hekima
Walihesabu Tangu Malaika Gabrile alipomwambia Daniel.
Kwamba hayo maono uliyoyaona ni ya wakati ujao. Nyakati hizi zimeamuliwa tangu zamani zile ilipotoka amri ya kuujenga mji wa Yerusalem hadi kukatiliwa mbali masihi Mkuu kutakuwa na majuma 70.
Habari hizi zinapatikana katika Kitabu cha Daniel Sura ya 8 na ya 9.
Kwa hiyo wakaanza kuhesabu Mwaka 457 B.C Ambao Tamko la Mfalme wa Uajemi Atashasta aliwaagiza waisraeli wakajenge mji wao.
Walakini wa tamko hili ni kuwa, Mfalme hakutoa tamko yeye bali Mfalme aliyekuwa amepita naye ni Kureshi Mkuu ndiye aliacha nyaraka hizo na Mfalme Dario pia alirejea agizo hilo akawaruhusu akina Ezra na wenzake Zerubabeli, Selaya, Modekai na kina Yoshua.
Sasa majuma 70 yalimegwa na kuwa siku 2300. Waka derive kwamba siku moja ni sawa na mwaka mmoja.....hii fomula sio formal.
Hivyo miaka 2300.
Tuanze kuhesabu......hadi kufikia mwaka zero, 0 yesu alipozaliqa tayari miaka 457 imekatika, so unatoa 2300-457 unapata 1844.
So Masihi angekuja mwaka huo.
Ikawa kinyume chake.
Helen G white akaja na ufafanuzi baada ya kuona unabii uliotangazwa na Mchungaji wake William Miler haukutimia. Akasema walikosea kumbe 1844 ulikuwa mwaka wa Yesu kuhama kutoka patakatifu kwenda patakatifu sana.
Sasa walijuaje Yesu alikuwa anahama? Basi rejea kitabu cha Ufunuo kinaeleza ni lini Yesu atafanya huduma ya utakaso. Baada ya utawala wa Mwovu shetani wa Nyakati, Nyakati mbili na nusu wakati au miezi 42.
So ukioanisha habari za Unabii wa Daniel na habari za unabii wa Yohana vinaendana.