Nimeshangazwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutotaka Bodi ya kitaalam ya Walimu

Nimeshangazwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutotaka Bodi ya kitaalam ya Walimu

Waulize madaktari na wauguzi mateso wanayopata kwenye hizo bodi unazozililia,

Leseni laki na nusu, pepa laki na nusu, supp elfu 75,

Alafu unaambiwa utoe pesa ya mahafali ya leseni,

Yaani mkuu huwaonei huruma wenzako mimi nakufananisha na wachawi
 
hiyo bodi ni muhimu ili tuwe na walimu wenye uwezo,wanaojisomea na kujikumbushia ....sio walimu wanaojua kuchapa tu....
upande wa madaktari...wana bodi yao inayowataka wahudhurie semina na presentaions ili kuwa update na matibabu na teknologia mpya kwenye matibabu
 
Ili ubora na uwezo wa mwalimu ujulikane lazima aundiwe chombo cha kupunguza pato lake dogo? Walimu wanavyombo vingi vinavyowamulika. Ukaguzi, cwt, tsc nk hiyo bodi ina lipi jipya zaidi ya kutafuta kumnyonya mwalimu fedha zake ???
Kwani cwt hawalipi michango?? Ukaguzi jukumu lao sio kuhakiki ubora wa mwalimu ila kuona kama yaliyopangwa kufanyika yametekelezwa.
Na usichokujua wewe na walimu ni kwamba bodi hiyo itawasaidia walimu kuwatambulisha kimataifa kama wataalamu waliothibitishwa na sio waliosoma tu darasana.
Sisi kama Tanzania bara hatuna leseni za ualimu ila wenzetu znz wanazo kitu ambacho kinaiheshimisha taaluma ya ualimu. Hoja ingekuwa makato na tozo ila sio hicho chombo.
Na wanachopinga cwt na wahuni wengine ni kwamba bodi hiyo haitaundwa na ngumbaru kama walivyojazana huko cwt.
 
Habari!

CWT = Chama cha Walimu Tanzania, Press yao imenishangaza sana eti hawaungi kuwepo kwa bodi ya kitaaluma ya Walimu (Teachers' professional board). Tena kwa madai kuwa walimu watabebeshwa mzigo mkubwa wa makato ya tsh.50000/= kwa mwaka yakihusisha lesseni ya ufundishaji, semina kwa walimu nk.

Wakidai kuwa walimu hawaitaki hiyo bodi sijui CWT wamefanya utafiti lini na halmashauri ngapi?

Hawa hawajui kama hii iitatuondolea walimu wasio na uwezo waliojazana mashuleni. Kwa kuwa update na mizigo kusitishiwa lesseni ili ualimu usiwe kazi ya walio feli mitihani.

Hivi CWTHilo ndo tatizo la walimu pekee nchi hii: Mbona malalamiko ya walimu ni mengi;
Wapo wanaolilia kupanda madaraja
Wapo wanaolilia kikokotoo hiki kipya
Wapo wanaolilia makato ya CWT na kuambulia t-shirt kila mwaka yasiyo na mantiki.
Wapo wanaolilia makato ya bodi ya mikopo nje ya mikataba yao.

AJABU:
Mama Salma Kikwete anachangia bungeni eti walimu hawaitaki hiyo bodi.
Pia Mh. Ndaisaba Mbunge wa ngara nae katumwa na walimu eti hawaitaki hiyo bodi mpya.
Tuwaulize hao walimu kwani wanaitaka hiyo CWT yenyewe? Inayonuka kila aina ya ufisadi.la tiket za Lesotho na misri. Benki nk ni shida tu.

Naunga mkono hiyo bodi iwapo kama fani nyinginezo.

CWT Msiogope hakuna kisicho na mwisho.

Pilipili msizozila zinawawasha namna gani?

Mambo ya ngoswe yanakuhusu vipi jombi?
 
Waulize madaktari na wauguzi mateso wanayopata kwenye hizo bodi unazozililia,

Leseni laki na nusu, pepa laki na nusu, supp elfu 75,

Alafu unaambiwa utoe pesa ya mahafali ya leseni,

Yaani mkuu huwaonei huruma wenzako mimi nakufananisha na wachawi
Sio mchawi tu bali mtesi wa daraja la juu. Anachochea ili walimu wazidi kunyanyasika. Huyo hana tofauti na Kibwetere !!!
 
Sio mchawi tu bali mtesi wa daraja la juu. Anachochea ili walimu wazidi kunyanyasika. Huyo hana tofauti na Kibwetere !!!
Kwahiyo hiyo 50000 ni kubwa kuliko wanayochukua cwt.
 
Bodi siyo mbaya,ila waangalie namna ya kulipa hiyo ada ya mwaka.CWT humkata mwalimu asilimia mbili ya mshahara kila mwezi,ni bora waanze kukata asilimia moja na asilimia moja nyingine iende kwenye hiyo bodi ila siyo kuanzisha makato mapya
 
Maskinii walimu nawaona Wana andaliwa BOSS MPYA🤔🤔🤔,hivi hii kada kwann hudharaulika Sana hapa kwetu?!!kwanini Mwalimu huyu anayepokea mshahara kiduchu munamuongezea MABOSI wa kumsimamia?!!hizo efforts kwann tusizitumie kuongeza mishahara yao?!

Walimu tuukatae huu upuuzi,tumezidi kudhalilishwa!
Hatutaki bodi ya walimu kwani mabosi tulionao wanatutosha
TSC,AFISA ELIMU,CWT,WIZARA,TAMISEMI,Bodi!! Nooooo, enough is enough.kwa Sasa hakuna umuhimu wa Bodi TUNATAKA MASLAHI BORA.
 
Je TSC INAFANYA NINI? Bosi mpya anaandaliwa ulaji mpya kutoka kwenye mshahara kiduchu.
Makato mapya tena. Bongo kutoboa ni ngumu aisee.
 
CWT wanapigania ugali wao.
Mafala sana hao. Yaani wameshiba mpaka wamevimbiwa hela za walimu na hivyo hawataki wengine wale. Ukiwauliza ni kwa nini wanawakata walimu 2% kwenye mishahara yao, hawana majibu.

Si bora hata hiyo ada ya elfu 50 kwa mwaka, kuliko hela wanazo waibia walimu kila mwezi huku wakiwa ni useless tu! CWT ni zaidi ya makenge.
 
Habari!

CWT = Chama cha Walimu Tanzania, Press yao imenishangaza sana eti hawaungi kuwepo kwa bodi ya kitaaluma ya Walimu (Teachers' professional board). Tena kwa madai kuwa walimu watabebeshwa mzigo mkubwa wa makato ya tsh.50000/= kwa mwaka yakihusisha lesseni ya ufundishaji, semina kwa walimu nk.

Wakidai kuwa walimu hawaitaki hiyo bodi sijui CWT wamefanya utafiti lini na halmashauri ngapi?

Hawa hawajui kama hii iitatuondolea walimu wasio na uwezo waliojazana mashuleni. Kwa kuwa update na mizigo kusitishiwa lesseni ili ualimu usiwe kazi ya walio feli mitihani.

Hivi CWTHilo ndo tatizo la walimu pekee nchi hii: Mbona malalamiko ya walimu ni mengi;
Wapo wanaolilia kupanda madaraja
Wapo wanaolilia kikokotoo hiki kipya
Wapo wanaolilia makato ya CWT na kuambulia t-shirt kila mwaka yasiyo na mantiki.
Wapo wanaolilia makato ya bodi ya mikopo nje ya mikataba yao.

AJABU:
Mama Salma Kikwete anachangia bungeni eti walimu hawaitaki hiyo bodi.
Pia Mh. Ndaisaba Mbunge wa ngara nae katumwa na walimu eti hawaitaki hiyo bodi mpya.
Tuwaulize hao walimu kwani wanaitaka hiyo CWT yenyewe? Inayonuka kila aina ya ufisadi.la tiket za Lesotho na misri. Benki nk ni shida tu.

Naunga mkono hiyo bodi iwapo kama fani nyinginezo.

CWT Msiogope hakuna kisicho na mwisho.
Walimu wengi ni grade A,huko kwenye bodi inakuaje?
 
Profession Board ni muhimu kwenye profession yoyote ambayo inazingatia maadili na nidhamu ya wataalamu.

Nadhani hoja ilipaswa kuwa makato atabebeshwa nani. Mathalani, kumekuwepo na utaratibu usiorasmi kwa fields za uhasibu na ununuzi waajiri kuwalipia annual fees watumishi wao.

Nafikiri busara hiyo hiyo ingetumika kwa walimu pia. Lakin kwa kuondosha hyo busara na kuweka kuwa lazima inapaswa liwe ni swala la kisheria kwamba mwajiri anawajibika kulipa annual professional fees kwa watumishi wake kwa kuwa yeye ndo anatumia na kunufika na ujuzi wao.
 
Ili ubora na uwezo wa mwalimu ujulikane lazima aundiwe chombo cha kupunguza pato lake dogo? Walimu wanavyombo vingi vinavyowamulika. Ukaguzi, cwt, tsc nk hiyo bodi ina lipi jipya zaidi ya kutafuta kumnyonya mwalimu fedha zake ???
Kuingia CWT iwe ni hiyari, kwa sabau hiyo ni ‘trade union’ tu ina dili na maslahi ya walimu na si na ualimu kama taaluma.
Bodi ni muhimu ili tutambuane kwa leseni.
Kinachosumbua hapo ni mgongano wa maslahi– CWT na hisi atapaswa kuwa chini ya na ni kama wanazuia mabadiliko. Na vyama vingine vya walimu vitajitokeza, ualimu ni kada pana na siamini kama CWT wana ya 'adress' matatizo na changamoto ipasavyo zaidi ya ku 'suppress' watu ambao wanajipambanua kwamba wanamahitaji tofauti na wanahitaji umoja.

CWT ni mchanganyiko wa akili nyingi, kuanzia cheti, diploma na digrii. Mkusanyiko huu lazima unamahitaji tofauti; CWT inafaida kwa wachache wanaweza kupata ulaji umo.
Uwingi wa wanachama cheti>diploma>digrii, kuna kundi unaweza kulipelekesha unakotaka kuna kundi lazima linahoji kila kitu. Hata hivyo wote hao wanaitwa walimu!

Saizi kuna sisi walimu wa 'online' k.v THE OnlineChem Teacher Tz na tuition, wote tunahitaji leseni-tutambulike. CWT ibaki kwa wanaopenda kubaki. Makato kwa mwalimu yanaonekana yatakuwa makubwa kwa sababu 'mentality' ya kiongozi ni ile kwamba ni lazima kila mwl awe mwanachama CWT
 
Waulize madaktari na wauguzi mateso wanayopata kwenye hizo bodi unazozililia,

Leseni laki na nusu, pepa laki na nusu, supp elfu 75,

Alafu unaambiwa utoe pesa ya mahafali ya leseni,

Yaani mkuu huwaonei huruma wenzako mimi nakufananisha na wachawi
Kazi yoyote ili iwe Profession sifa mojawapo ni lazima iwe na board maalumu. Sasa CWT sio board; ni kitu kingine kinaangalia zaidi ‘maslahi ya mwalimu’ na si ‘ualimu wa mwalimu’. Ualimu kibongobongo ni kazi tu na wala si profession. Profession ina sifa zake: 1. Board of profession 2. Autonomy 3. Code of conduct etc. Tunahitaji 'Board of profession' sio 'trade union' kama hii CWT.
 
Back
Top Bottom