Nimeshangazwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutotaka Bodi ya kitaalam ya Walimu

Nimeshangazwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutotaka Bodi ya kitaalam ya Walimu

Kazi yoyote ili iwe Profession sifa mojawapo ni lazima iwe na board maalumu. Sasa CWT sio board; ni kitu kingine kinaangalia zaidi ‘maslahi ya mwalimu’ na si ‘ualimu wa mwalimu’. Ualimu kibongobongo ni kazi tu na wala si profession. Profession ina sifa zake: 1. Board of profession 2. Autonomy 3. Code of conduct etc. Tunahitaji 'Board of profession' sio 'trade union' kama hii CWT.
Afadhali wew unaelewa, na hii ni kilio cha muda mrefu.
 
Kuingia CWT iwe ni hiyari, kwa sabau hiyo ni ‘trade union’ tu ina dili na maslahi ya walimu na si na ualimu kama taaluma.
Bodi ni muhimu ili tutambuane kwa leseni.
Kinachosumbua hapo ni mgongano wa maslahi– CWT na hisi atapaswa kuwa chini ya na ni kama wanazuia mabadiliko. Na vyama vingine vya walimu vitajitokeza, ualimu ni kada pana na siamini kama CWT wana ya 'adress' matatizo na changamoto ipasavyo zaidi ya ku 'suppress' watu ambao wanajipambanua kwamba wanamahitaji tofauti na wanahitaji umoja.

CWT ni mchanganyiko wa akili nyingi, kuanzia cheti, diploma na digrii. Mkusanyiko huu lazima unamahitaji tofauti; CWT inafaida kwa wachache wanaweza kupata ulaji umo.
Uwingi wa wanachama cheti>diploma>digrii, kuna kundi unaweza kulipelekesha unakotaka kuna kundi lazima linahoji kila kitu. Hata hivyo wote hao wanaitwa walimu!

Saizi kuna sisi walimu wa 'online' k.v THE OnlineChem Teacher Tz na tuition, wote tunahitaji leseni-tutambulike. CWT ibaki kwa wanaopenda kubaki. Makato kwa mwalimu yanaonekana yatakuwa makubwa kwa sababu 'mentality' ya kiongozi ni ile kwamba ni lazima kila mwl awe mwanachama CWT
Very correct ,watu wenye mashaka na competence yao ndo hawaitaki board.
 
Profession Board ni muhimu kwenye profession yoyote ambayo inazingatia maadili na nidhamu ya wataalamu.

Nadhani hoja ilipaswa kuwa makato atabebeshwa nani. Mathalani, kumekuwepo na utaratibu usiorasmi kwa fields za uhasibu na ununuzi waajiri kuwalipia annual fees watumishi wao.

Nafikiri busara hiyo hiyo ingetumika kwa walimu pia. Lakin kwa kuondosha hyo busara na kuweka kuwa lazima inapaswa liwe ni swala la kisheria kwamba mwajiri anawajibika kulipa annual professional fees kwa watumishi wake kwa kuwa yeye ndo anatumia na kunufika na ujuzi wao.
Mi napingana kidogo na wew ,acha walimu walipie ili board iwe huru. Pia suala hapo ni kuwa watu wawe na hiyari ya kujiunga na cwt au la. Ili atakae kubeba mizigo yote yaani board na cwt abebe asietaka aachwe.
 
Kwahiyo hiyo 50000 ni kubwa kuliko wanayochukua cwt.
Kwa hiyo cwt wachukue, uongeze tena 50,000/-ya bodi. Mkaianzishe huko iwahusu wabunge. Bodi ya kitaalamu ya wabunge!! Kwani wao Wana mini kiwasaidiacho kufanya majukumu yao kwa weledi? Waanzishe bodi, walimu Wana cwt , tsc nk. Huo upuuzi mwingine ni wa nini kwa walimu ??
 
Bodi siyo mbaya,ila waangalie namna ya kulipa hiyo ada ya mwaka.CWT humkata mwalimu asilimia mbili ya mshahara kila mwezi,ni bora waanze kukata asilimia moja na asilimia moja nyingine iende kwenye hiyo bodi ila siyo kuanzisha makato mapya
Mnajitengenezea ulaji kupitia mgongo wa mwalimu. Leave teachers alone. Mmewanyanyasa vya kutosha, mmewapuuza vya kutosha. Too much !!
 
Kila walimu sometimes huwa hawaeleweki wanataka nini
Hiyo bodi inakuja na michango wana haki ya kuikataa kila anayewaza kupika wazo la kwanza anawaza waalimu. Mishahara yao midogo lakn kila mtu anataa awapige
 
KUNA AKINA AKILIMALI HUMU KAMA YULE KIONGOZI WA TIMU FULANI,HAWAPENDI MAMBO YA KITAALAM WANAJUA KABISA YAKIINGIA TONGE LITATOWEKA.....
 
Back
Top Bottom