Nimeshangazwa na hili la ubaguzi halmashauri ya Mbeya

Nimeshangazwa na hili la ubaguzi halmashauri ya Mbeya

Happycuit

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2013
Posts
646
Reaction score
542
Naandika kwa masikitiko hii taarifa jamani wakubwa zangu shikamooni,vijana wenzangu habarini za muda huu,...kama inavyofahamika wizara ya elimu imetoa tangazo la nafasi za masomo ya kidato cha tano na ualimu kwa wale waliopata div1* mpaka div3 kuanzia mwaka 2004 mpaka 2013 na kama tangazo linavyoelekeza kuwa maombi yatumwe kwa katibu mkuu wizara ya elimu kwa wale walio dar es salaam ila kwa sisi tulio MIKOANI maombi yetu tuyapeleke kwa afisa elimu wilaya, mimi nipo mbeya kwa sasa na kwakuwa nimeona deadline ni karibu sana nikaona bora niombee hukuhuku ila niliyokutana nayo katika ofisi ya afisa elimu yamenichosha na kunivunja nguvu kabisa,nilipofika baada ya kueleza shida yangu nikakumbana na maswali ya ajabu
1.WEWE MWENYEJI WA WAPI?
2.SHULE UMESOMEA MKOA GANI?
3.KWANINI USIENDE KUOMBEA HUKO NYUMBANI KWENU?
4.HAPA ANAKUJUA NANI?NA NANI ATAPITISHA HIYO BARUA YAKO?(nikamjibu wameandika kuwa afisa elimu awasilishe kwa katibu na sio apitshe)
5.(akajb)SISI HATUWEZI KUSHUGHULIKIA HILO SUALA LAKO UENDE UKAOMBEE DAR
 
jamani huu ni ubaguzi dhahiri naomba munishauri nifanye nini?
 
Mikoa ya njanda za juu kusini wabaguzi wa kupindukia!ukiona mahali mchaga ameshindwa kufanya biashara pakimbie
 
dah!yan nimeishiwa nguvu kabisa na sijui nifanye nini maana tar10july ndio mwisho wa kuomba na hawa watu wa posta imani nao imenitoka kabisa yani toka nianze kutumia posta sijawah kufanikiwa nahisi barua hazifiki dg
 
nimetokea kuuchukia huu mkoa na sasa ndio naanza kuamini hili ndilo linalofanya mkoa wao kutoendelea mijinga sana yani inataka misafwa na minykysa myenzao ndio iwahudumie wakati kodi tuvnalipa sote
 
Waamini tu posta utume kwa express sio njia ya kawaida itakuwa vizur zaid
 
Tumia Ems Nenda Posta Watakuelewesha Nadhani Ni Buku Kama Kumi Ivi, Wanakupelekea Hadi Kwa Muhusika, Usikate Tamaa Mungu Atakushindia, Ukiona Hayo Ujue Utafanikiwa Sana.
 
nimetokea kuuchukia huu mkoa na sasa ndio naanza kuamini hili ndilo linalofanya mkoa wao kutoendelea mijinga sana yani inataka misafwa na minykysa myenzao ndio iwahudumie wakati kodi tuvnalipa sote

acha kupiga kelele wewe maksi zako zinamakengeza.
 
kama wamekuzingua mbeya jiji nenda mbeya vijijini au vice versa ofis zao zipo karibu labda utasaidiwa si unajua watu wanavurugwa wakipata vinafas
 
nimetokea kuuchukia huu mkoa na sasa ndio naanza kuamini hili ndilo linalofanya mkoa wao kutoendelea mijinga sana yani inataka misafwa na minykysa myenzao ndio iwahudumie wakati kodi tuvnalipa sote

Hivi eeh!! Nilikuwa sijui kama Mby haiendelei. Sasa kama Mby haiendelei hii nchi yote itakuwa haiendelei maana ni mji wa wa tatu kwa ukubwa baada ya dar na mwanza, ni mji wa tatu pia kwa kukusanya mapato mengi, ni mkoa wa kwanza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na mengine mengi. Huduma za jamii nzuri, miundombinu mizuri pia. Labda wew unaona hauendelei kwa vigezo gani?
 
Haya malalamiko hayana ukweli wowote inaonekana ni ya kutunga tu, Inaoneka matokeo yako si mazuri hata Ualimu huna uhakika wa kupata ndo sababu umepanic hata kabla ya kutuma maombi,dead lina tar 10 july zaid ya wiki mbili mbele unachanganyikiwa leo? ha ha ha una matatizo tena makubwa tu,kwanini usitume huko unakofikiri hawabagui?,au kwa nini usimtumie ndugu yako akupelekee mkoa unaoutaka wewe? Unapiga kelele kwamba Mkoa haundelei una uhakika na hilo au sababu umefeli basi hata data za mikoa inayoendelea kwa kasi Tz huijui?
 
Matokeo yako yapoje tuanzie hapo kwanza. Maana isije ikawa unasingizia mji kumbe una div 5
 
Mikoa ya njanda za juu kusini wabaguzi wa kupindukia!ukiona mahali mchaga ameshindwa kufanya biashara pakimbie

Tatizo bado una mawazo mgando kwamba biashara wanafanya wachaga tu? inawezekana ndo uelewa wako umeishia hapo lkn ukzunguka vizuri Tz ndo utajua ukweli kwamba ni makabila mengi tu ya Tz wanajishugulisha na biashara kubwa kubwa zaid ya wachaga.
 
nimetokea kuuchukia huu mkoa na sasa ndio naanza kuamini hili ndilo linalofanya mkoa wao kutoendelea mijinga sana yani inataka misafwa na minykysa myenzao ndio iwahudumie wakati kodi tuvnalipa sote

Kwa uandishi wa namna hii napata wasiwasi na akili yako!! Inaonekana wewe mwenyewe haujitambui.

Pole' ila unapaswa kujua kuwa mtu yeyote yupo huru kufanya kazi sehem yoyote ya nchi ili mradi kama anakidhi vigezo na kapata kazi mahala husika..
 
sijitambui kivipi mkuu?mbona uandishi wangu unaeleweka na umeelewa ndio maana umechangia!
 
Back
Top Bottom