Nimeshauriwa na daktari kuanza kutumia dawa za kushusha pressure

Nimeshauriwa na daktari kuanza kutumia dawa za kushusha pressure

Tafuta chanzo cha pressure kupanda kwenye mwili wako kisha utatue hiyo changamoto, pressure ya kupanda ina hatari mbaya sana inaweza ikakuchukua mazingira ambayo hata haukutarajia.
 
Tafuta chanzo cha pressure kupanda kwenye mwili wako kisha utatue hiyo changamoto, pressure ya kupanda ina hatari mbaya sana inaweza ikakuchukua mazingira ambayo hata haukutarajia.
Sawa mkuu chanzo cha pressure ni changamoto za maisha zinazonikabili
 
Tafuta chanzo cha pressure kupanda kwenye mwili wako kisha utatue hiyo changamoto, pressure ya kupanda ina hatari mbaya sana inaweza ikakuchukua mazingira ambayo hata haukutarajia.
Exactly
 
Sawa mkuu chanzo cha pressure ni changamoto za maisha zinazonikabili
Una msongo wa mawazo? Je ulifanya check up tu ya kawaida ama ulikuwa unaumwa ndipo ukaenda hospital kutibiwa?
 
Una msongo wa mawazo? Je ulifanya check up tu ya kawaida ama ulikuwa unaumwa ndipo ukaenda hospital kutibiwa?
Nilikuwa nasumbuliwa na homa.
Miezi mitano iliyopita nilipima nikiwa siumwi ila jasho lilikuwa linanitoka sana na hasa nikiwa nimelala baada ya kupimwa pressure ilikuwa juu nilishauriwa nianze kutumia dawa lakini sikutumia.
Leo nilijisikia mwili hauna nguvu nikapima nikakutwa pressure iko juu ndiyo nimeanzishiwa dozi
 
Nina miaka 40s nimepima hospitali ya wilaya
Kwa 40s presha itakua imekuja mapema sana, unless kama una strong family history of hypertension.

Pia kuna ishu ya joto kali nowdays, ambayo sometimes inawasababishia vijana kupata hypertension na mwisho kuishia na heat stroke, sijajua hali za huko mikoani.

Btw, ingekua vyema kama wangefanya blood workup kucheki sababu nyengine ambazo zingepelekea tatizo kama hilo.
 
Joto ni la kawaida na hasa hiki kipindi cha masika
 
Pole mkuu, pressure mbaya Sana ilimsumbua Sana mzee wangu ilikua inafika hivyo 180,miguu inavimba, anahema harakaharaka mpaka tunaogopa, sema mzee wangu ni mbishi hakubali kushindwa kirahisi halafu Anajali Sana afya yake lakini ndo hivyo Tena umri ukisogea, alitumia dawa ya kienyeji mwaka jana ilimsaidia sana, juzi amepimwa Hindu kakuta pressure 128/80. Ana miaka 63.
Nakushauri anza kutumia hizo dawa za hospitali hiyo pressure ilipofika ni juu sana unaweza kuanguka wakati wowote,badili mtindo wa maisha,chumvi awe adui yako namba moja na mafuta ya kula yaepuke Sana.
Pole Sana punguza stress mkuu maisha ndo hayahaya tu.
 
Nilikuwa nasumbuliwa na homa.
Miezi mitano iliyopita nilipima nikiwa siumwi ila jasho lilikuwa linanitoka sana na hasa nikiwa nimelala baada ya kupimwa pressure ilikuwa juu nilishauriwa nianze kutumia dawa lakini sikutumia.
Leo nilijisikia mwili hauna nguvu nikapima nikakutwa pressure iko juu ndiyo nimeanzishiwa dozi
MalcoIM XII kakupa ushauli mzuri usikubali kupakamia madozi bila kujiridhisha...mimi nilikuwa nalowesha kitanda usiku kwa jasho, na nilikuwa nakohowa sana kura pia nilikuwa siwezi kibongo2 ningeambiwa nina TB nilikuwa na hema punzi jujuu luckily ..nimetibiwa hospital wanazokimbilia wanasiasa wetu ikaonekana ni Sarcoidosis...have you ever heard huu ugonjwa? Kapime hospital kubwa Aga Khan.. na nyingine ni afya yako hiyo bruda.
 
Ninaweza toa ushuhuda wa mzee wangu kwenye pressure labda inaweza saidia.

Miaka kadhaa imepita baba alipokuwa hajisikii sawa
Akawa anaipuuzia ile hali mpaka pale ambapo tukaona imefika stage sio.
Nikachukua jukumu la kumpeleka hospitali moja hivi ya private.
Wakampima magonjwa yote ya hatari na kugundua pressure iko juu so aanze kutumia madawa(yale ya kubugia kila siku na ikibaki kama siku mbili hivi kuisha dozi unafata njugu nyingine ili usikatize dozi)
Hospitali ile hawakuona ugonjwa mwingine zaidi ya pressure.

So tukarudi nyumbani na mabox yale ya dawa
mzee alikataa katakata kwamba ile pressure yake imefikia stage ya yeye kuwa mtumizi wa njugu za pressure.
Sababu alisema zile dawa ukianza inakuwa kama addiction hivi so siku ukiacha tu hapo ndipo pressure inapopita na wewe.

Tukamuelewa na kesho yake tukaenda hospitali nyingine ambayo ni ya serikali ikiwa na madaktari wa kutosha wakubwa wakubwa.

Aisee walivyompima upya wakamkuta na malaria.
ila kuhusu pressure huwa anayo but sio yakumfanya atumie madawa.

Alikaa sawa na mpaka leo yale madawa yapo nyumbani na hajawahi yagusa.
Na hapo umri wake ni 60+
 
Habari wataalamu wa tiba katika forums hii.
Nimekwenda kituo cha afya ikigunduliwa ni pressure iliyojuu sana ambapo iko kwa kiwango cha 180/117 kutokana na kiwango hicho nimeshauriwa nianze kutumia dawa za kushusha.
niombe kwenu wadau kama kuna yeyote hali hii ilishawahi mkuta na kutumia dawa siyo kwamba nitakaribisha matatizo zaidi kwani hali yangu ya afya iko vizuri changamoto ninayokutana nayo ni kutoka jasho jingi hasa wakati wa usiku.
Menya punje SITA za kitunguu swaumu,meza kama vidonge kabla hujalala Kila siku baada ya mwezi kapime Tena itashuka Hadi utashangaa!!

Vidonge vya hospital sio kabisa!!utatumia maisha yako tote na hutopona!!
 
Habari wataalamu wa tiba katika forums hii.
Nimekwenda kituo cha afya ikigunduliwa ni pressure iliyojuu sana ambapo iko kwa kiwango cha 180/117 kutokana na kiwango hicho nimeshauriwa nianze kutumia dawa za kushusha.
niombe kwenu wadau kama kuna yeyote hali hii ilishawahi mkuta na kutumia dawa siyo kwamba nitakaribisha matatizo zaidi kwani hali yangu ya afya iko vizuri changamoto ninayokutana nayo ni kutoka jasho jingi hasa wakati wa usiku.
Fuata ushauri wa daktari wako.

Vile vile fanya mabadiliko katika maisha yako. Tumia viungo vifuatavyo sana kwenye milo yako: Vitunguu swaumu (garlic), mdalasini (cinnamon), tangawizi (ginger), Iliki(Cardarmon), binzali ya njano (tumeric), majani ya chai -(lemongrass). Haya majani ya chai siyo yale unayonunua kwenye packet bali ni majani kabisa kama yaonekanvyo kwenye picha hii.
1708974406429.png
 
Back
Top Bottom