Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hongera.kama kilombero kuna wana jf naomba uwaweke kwenye kampeni. Mimi nasubiri mtu wa chadema kenye jimbo nilipo nimpe suport zote.
 
Hongera sana Dada Regy. You have my full endorsement! Go go go my sister!:violin::violin:
 
Hongera sana Ms. Regia
Wewe ni jasiri, umenifurahisha sana
Tuko pamoja na tunakutakia kila la heri
Mungu akutangulie
 
Nawashukuru wote.Nimezingatia maoni ya wenfi humu.Nimekuja na jina langu halisi hivyo GS imeshakufa haitakuwepo tena.

Historia kwa Ufupi sana.
Kifupi mimi ni Regia Estelatus Mtema,tuko twins na dada yangu ambaye yeye ni Kulwa mimi ni Dotto.Ni Watoto wa kwanza wa Bw Estelatus Mtema.Kabila langu ni Mmbunga niliyechanganyika na Mmanda.Nimezaliwa tarehe 21/04/1980 Ocean Road Hosp Dar.

Nilivunjika mguu mwaka 1987 wakati nacheza mpira(rede) na hivyo kulazimika kukatwa mguu.

Elimu.
Nimesoma shule ya Msingi Mchikichini Dar 1989-1995
Shule ya Sekondari Forodhani Dar- 1996-1999
Shule ya Wasichana Machame Moshi-2000-2002
Elimu ya Juu,Chuo KIkuu cha Kilimo Sokoine(SUA) 2003-2006-Digrii ya Uchumi na Lishe

Joined CHADEMA 2005 baadaye nikamua kujitolea kufanya kazi Makao Makuu 2007 mpaka sasa.

Sijaolewa wala sina mtoto.

Alunta continua

Hewalaaaaa, Twaib Twaib.

Haya sasa maneno, mgombea tunaye, jimbo tunalo, hata kama tunataka kusema tuna endorse mtu tunajua tuna mu endorse nani.
Haya ndiyo maneno.

Hongera sana. Kwa kuwa ulikuwa mwanachama makini wa JF siku nyingi, hilo tu linakupa pointi nyingi dhidi ya wapinzani wako kwani umeuona mjadala wa uongozi ukiendelea motomoto kutoka kwa vichwa vingi tofauti, hata vile vya wabishi wenye viranga.

Kwa sababu sijui maendeleo yeyote yaliyoletwa na mbunge wa sasa wa Kilombero, na kwa sababu nimejua umuhimu unaoweka katika kuleta umeme Kilombero (to say nothing of bei ya sukari, all locally produced products) na kwa kuwa naamini utaendelea kushirikiana nasi kama mbunge mwanachama, hususan kwa sababu umeonyesha moyo wa ushirikiano na kuonyesha unyenyekevu hata ulipopewa mzingo wa roho (unlike Shyrose) napenda kuchukua nafasi hii kukupendekeza rasmi na kuwaomba wapiga kura wa jimbo la Kilombero kukupigia kura kwa dhati.

Kura kwa Regia ni kura kwa kizazi kipya cha uongozi na JF.
 
Hongera sana Ms Regia aka GS

kuna swali zuri kakuuliza Semilong ungelijibu ningefurahi sana, maana ilikuwa kama huko biased katika gender

Kaka Kiranga Karibu utoe Hongera kwa dadako
 
Waungwana naomba nitoe ombi kama kuna uwezekano tujaribu kuunda kamati ya kampeni kwa wabunge hao watarajiwa, nina maana kama kuna uwezekano wa wana jf kwenda kilombero kutia nguvu japo kwq mkutano mmoja si haba, namaanisha kwa wale watakaokuwa karibu na jimbo
 
Hewalaaaaa, Twaib Twaib.

Haya sasa maneno, mgombea tunaye, jimbo tunalo, hata kama tunataka kusema tuna endorse mtu tunajua tuna mu endorse nani.
Haya ndiyo maneno.

Hongera sana. Kwa kuwa ulikuwa mwanachama makini wa JF siku nyingi, hilo tu linakupa pointi nyingi dhidi ya wapinzani wako kwani umeuona mjadala wa uongozi ukiendelea motomoto kutoka kwa vichwa vingi tofauti, hata vile vya wabishi wenye viranga.

Kwa sababu sijui maendeleo yeyote yaliyoletwa na mbunge wa sasa wa Kilombero, na kwa sababu nimejua umuhimu unaoweka katika kuleta umeme Kilombero (to say nothing of bei ya sukari, all locally produced products) na kwa kuwa naamini utaendelea kushirikiana nasi kama mbunge mwanachama, hususan kwa sababu umeonyesha moyo wa ushirikiano na kuonyesha unyenyekevu hata ulipopewa mzingo wa roho (unlike Shyrose) napenda kuchukua nafasi hii kukupendekeza rasmi na kuwaomba wapiga kura wa jimbo la Kilombero kukupigia kura kwa dhati.

Kura kwa Regia ni kura kwa kizazi kipya cha uongozi na JF.

poa mkuu
 
Waungwana naomba nitoe ombi kama kuna uwezekano tujaribu kuunda kamati ya kampeni kwa wabunge hao watarajiwa, nina maana kama kuna uwezekano wa wana jf kwenda kilombero kutia nguvu japo kwq mkutano mmoja si haba, namaanisha kwa wale watakaokuwa karibu na jimbo

Hii imetulia,imekaa vizuri..
 
Waungwana naomba nitoe ombi kama kuna uwezekano tujaribu kuunda kamati ya kampeni kwa wabunge hao watarajiwa, nina maana kama kuna uwezekano wa wana jf kwenda kilombero kutia nguvu japo kwq mkutano mmoja si haba, namaanisha kwa wale watakaokuwa karibu na jimbo

Naunga mkono hoja....
 
ombi la kituko lifanyiwe kazi kwa wagombea wote au kwa wachadema tu?
 
ha ha ha,unaona wivu?

nimeuliza tu ...................suala la wivu halijaingia hapo BADO.

nikisha kupata jibu ndio suala la wivu linaweza likaibuka au laweza lisiibuke vile vile
 
Alikuwa anamaanisha wagombea wote ambao ni active members wa JF
 
ombi la kituko lifanyiwe kazi kwa wagombea wote au kwa wachadema tu?

Swali muhimu sana, essentially ni swala la kuamua kama JF inaendorse CHADEMA au mbunge yeyote.

Uzuri wa JF ni sense ya individuality, tunapoanza ku act collectively tunaanza kuuliza maswali mengi kuliko tutakayojibu.Kwa mfano hili swali ni a can of worms. Tukisema tu endorse watu wa CHADEMA tu tuta confirm accusations kwamba JF ni mali ya CHADEMA, tukisema tu endorse wagombea regardless ya chama kuna watu humu hawaamini kwamba mgombea yoyote wa CCM anaweza kuleta mabadiliko.

The best thing ni kwa watu wanaokubaliana ndani ya JF kufanya effort ya pamoja, lakini JF officially inakuwa beyond party politics na campaigning.
 
Jibu zuri sana...
 
nilikuwa napata picha ya kuchekesha kichwani

JF inapigia kampeni chadema kwa weak points za ccm, na kupigia kampeni ccm kwa ama weak points za chadema au hizo hizo weak points za ccm kuzi express positively!
 
Hongera sana Regia. Nakutakia Kila la kheri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom