Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kiranga anagombea jimbo gani?
apate jimbo huyu labda la JF hata hilo hapati kura, huyu ni sawa na wale wanafunzi vimbele mbele wanaojifanya kuuliza maswali mengi darasani ikija test anapata 10.
 
unajifanya much know sana kila jukwaa upo kila thread upo na kuingilia mijadala ya watu kujifanya mjuvi unajua kila field wakati hatuoni kitu chochote zaidi ya pumba na matusi, jirekebishe.

Hahaha, sasa kama "najifanya" mbona unashindwa kupangua hoja unakuja na shutuma za jumla jumla ?
 
Hahaha, sasa kama "najifanya" mbona unashindwa kupangua hoja unakuja na shutuma za jumla jumla ?
sasa unapouliza mgombea ni mwanamke au mwanamme una hoja gani hapo unataka kuolewa.
 
apate jimbo huyu labda la JF hata hilo hapati kura, huyu ni sawa na wale wanafunzi vimbele mbele wanaojifanya kuuliza maswali mengi darasani ikija test anapata 10.
Hapati jimbo la uchaguzi na anapata 10 darasani, sawa, kwa nini unamjadili?
 
Mweh,sredi yangu imepoteza mwelekeo.Yangu macho tuone sasa hao wanaoweza kuface challenges za kila namna.
 
Mweh,sredi yangu imepoteza mwelekeo.Yangu macho tuone sasa hao wanaoweza kuface challenges za kila namna.

Tatizo hatuna utamaduni wa passionate debate.

Na kama hatuna passionate debate hatuwezi kukubali kujifunza vitu vipya na kufikiri critically.

Na kwa sababu hatuwezi kujifunza vitu vipya na kufikiri critically, hatuwezi kuendelea.
 
Ndio maana nilikuambia ni bora usingetangaza hapa.....ungewatangazia tu hao watu wa jimbo lako.

Nilishalisema hili mwanzo, the moment you announce this race here you open a can of worms.

Mbunge mtarajiwa hajui the art of not opening up cans of worms, anaweza hata ku spill classified documents za CHADEMA.
 
sasa unapouliza mgombea ni mwanamke au mwanamme una hoja gani hapo unataka kuolewa.

Hahahaha,

Avumaye ni Omari mpinzani wa Shyrose, kumbe wako wengi.

Luckily I am not the Shyrose type.
 
Ndio maana nilikuambia ni bora usingetangaza hapa.....ungewatangazia tu hao watu wa jimbo lako.
Mh... i see nothing wrong kuleta hapa kwani wa jimboni watakua wanajua na ndio maana alipata hizo votes
 
Ndio maana nilikuambia ni bora usingetangaza hapa.....ungewatangazia tu hao watu wa jimbo lako.

Nyani Ngabu,kulikuwa na kila sababu ya kujitangaza humu bila hata ya kufahamika..Ila basi tu watu wanataka niweke identity yangu hadharani..Kwani ingeishia tu kujua GS anagombea Ubunge jimbo X kingaharibika nini?what is the essence ya kujuana?lakini kwakuwa wa ubani kanishauri nijiwke hadharani ndio nafanya process za kuzungumza na mods ili niwe hadharani..Kwahiyo GS itanaenda kufa masaa machache yajayo..
 
Hii ni jeuri sasa. Kama hutaki kuulizwa yote hayo kwa nini umekuja kutuambia hapa kuwa umeshinda kura za maoni kwenye chama chako? Unachoogopa kuulizwa ni nini au kwa nini hutaki tusikuulize? Mantiki zingine bana...yaani hazina mbele wala nyuma.

Eti tusikuulize....tusikuulize kwani wewe ni nani? Ebo! Watu kama nyinyi hamfai kabisa kushika public office kwa sababu hamuelewi maana yake. Kama hutaki watu wakuulize maswali basi jitoe.

Mbunge gani mtarajiwa una jeuri hivyo.....Halafu kwani ukiulizwa unagombea jimbo gani nini kitaharibika? Kwa sababu siyo kwamba unamwaga mbinu na mikakati yako hadharani.....

Umeshanitibua na kwenye uchaguzi mkuu na ushindwe kwa sababu hustahili kuwatumikia watu wa jimbo lako.
ni wewe kweli mkuu?
TULIZA MUNKALI.
 
Nyani Ngabu,kulikuwa na kila sababu ya kujitangaza humu bila hata ya kufahamika..Ila basi tu watu wanataka niweke identity yangu hadharani..Kwani ingeishia tu kujua GS anagombea Ubunge jimbo X kingaharibika nini?what is the essence ya kujuana?lakini kwakuwa wa ubani kanishauri nijiwke hadharani ndio nafanya process za kuzungumza na mods ili niwe hadharani..Kwahiyo GS itanaenda kufa masaa machache yajayo..

Unapogombea public office unajinadi kwa watu kwamba wewe unafaa, unapojinadi ni muhimu kabisa kuhakikisha una uwazi, ili watu wakujue fika, isije kuwa una vitu ambavyo havitakikani katika ubunge halafu watu wakashindwa kujua.

Sasa ukija hapa kusema unagombea wakati hutaki kujitaja mimi naona.

1. Hujiamini na unaogopa mijadala ambayo ni muhimu kabisa katika kupata uwakilishi.
2. Kuna kitu unaficha hutaki watu wajue
3.Unataka ujiko wa kujulikana unagombea ubunge lakini kwa sababu hujiamini, unaogopa disappointment kwa sababu huamini kwamba utashinda.
4.Huna track record ya kutosha kuku qualify

Mtu anayejiamini, hana la kuficha na ana track record hawezi kuogopa kujitangaza hapa. Hata kama ingebidi kwa kutumia jina jipya.
 
kumuuliza yeye mwanamke au mwanaume wewe unachotaka nini ndoa? huna hoja, haya mimi mwanamme ni PM nikuelekeze nilipo.

duuuuu,mkuu mnakoelekea kubaya.

Nina mashaka huyu Quinine ndiye yule Omar aliyepigwa na Shyrose anataka kuja kumalizia hasira zake hapa.

Kwa taarifa yako tu mimi rijali kwa mabinti ila ma.s.h.oga situmii, kwa hiyo kama unataka kushikishwa ukuta tafuta bwana sehemu nyingine.
 
mmmmmh, NILIJUA MUDA SI MREFU MTAFIKIA HAPA..............ACHENI HIZO LUGHA.......USHAURI;KWA NN, KIRANGA QUININE1.VUMILIANENI
2.KAMA UNAONA JAMAA KAKUUDHI,TULIA KWA MUDA KWANZA KABLA HUJASEMA CHOCHOTE.......HASIRA IKIISHA...UNAENDELEA
3.BADO TUNAHITAJI SANA MICHANGO YENU HAPA JF.
USHAURI KWA GS
1.SIASA INA MIKIKIMIKIKI YA AJABU NA MAMBO PENGINE USIYOYATEGEMEA KABISA.
2.UTAFIKIA MAHALI UTATUKANWA,KUDHARAULIWA,KUTISHWA, NA HATA KUDHALILISHWA.....PIGA MOYO KONDE
3.USIJE UKAMKASIRIKIA AU KUMJIBU MTU YEYOTE VIBAYA KWA KUTOA MAWAZO YAKE VILE USIVYOTAKA.
NINACHOKIONA;
1.UNACHANCE KUBWA YA KUSHINDA.
2.NA UKISHINDA SINA SHAKA UTAKUWA KIONGOZI BORA.........HAYO NDIYO MAONI YANGU.
 
Sasa kinachokuwasha kuuliza jinsia ya mgombea ni nini.
 
Tall

Mimi sina tatizo ila ninachotaka ni heshima kwa mgombea si huyu tu bali wagombea wote wapewe heshima stahili, mtu anakuja na maswali ya ajabu ajabu kwanini asijibiwe kiajabu ajabu. Unauliza mgombea ni wa kike au wa kiume hilo litasaidia nini jimboni kwake.

Huyo kiranga angekuwa anauliza maswali kama mgombea atawafanyia nini wapiga kura wake au kwenye jimbo lake kuna matatizo gani makuu nafikiri GS atakuwa mjinga kutojibu maswali kama hayo.
 
Sasa kinachokuwasha kuuliza jinsia ya mgombea ni nini.

Sijauliza jinsia ya mgombea, kuna mtu kauliza huyu Gender Sensitive ni mwanamme au mwanamke? Nikasema huyu hajulikani kashawahi kukataa kwamba ni mwanamke na kashawahi kukataa kwamba ni mwanamme.

Nikapoint out kwamba ana usiri mkubwa sana si kwa jina na jimbo, bali hata jinsia yake.

Jifunze kusoma au nenda kachekiwe glaucoma.
 
Tall

Mimi sina tatizo ila ninachotaka ni heshima kwa mgombea si huyu tu bali wagombea wote wapewe heshima stahili, mtu anakuja na maswali ya ajabu ajabu kwanini asijibiwe kiajabu ajabu. Unauliza mgombea ni wa kike au wa kiume hilo litasaidia nini jimboni kwake.

Huyo kiranga angekuwa anauliza maswali kama mgombea atawafanyia nini wapiga kura wake au kwenye jimbo lake kuna matatizo gani makuu nafikiri GS atakuwa mjinga kutojibu maswali kama hayo.

Mgombea yuko wapi hapa? Mgombea gani? wa jimbo gani?

Hivi mtu yeyote akija na kusema yeye mgombea kwa kutumia username ya JF bila kukupa anything else utaamini hivyo?

Muhuni yeyote akitaka kuchota akili za watu kwa kusema tu "mimi mgombea" mtakubali tu ?

Utaulizaje mgombea atawafanyia nini wagombea wake wakati humjui mgombea waljibua jimbo? Utajuaje kwamba unapouliza haya maswali katika kuyajibu huoni mgombea huyu, hata kama ni mgombea kweli atachukua risk ya kutaja specifics zitakazomfanya ajulikane wakati yeye hataki kujulikana?

Unona kwa nini ni muhimu mgombea kujitaja sasa? Huwezi kuuliza swali lolote kabla mgombea hajajitaja kwa sababu swali lolote utakalouliza lina chance ya kumjulisha mgombea huyu.

Anajificha ficha nini? Anaogopa? Kuna kitu kibaya kafanya? Hajiamini ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom