Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu hata mimi nilijiuliza hilo lakini nimefikiria kwa undani na hakika hana sababu ya kujitambulisha hapa kwani kura hazipigwi JF.
Sasa kwa nini kajitambulisha kama mgombea mtarajiwa hapa JF ? Wagombea wanapofanya kampeni kwenye TV, kwani kura zinapigwa kwenye TV? JF ni sawa na TV, ni media, na kama mgombea yuko hapa JF na ana access ya kujitambulisha na kufanya campaign hapa, lakini haitumii, mimi namuona hajiamini na hayuko serious katika campaign yake.Ni kama anaona privacy yake ni muhimu kuliko campaign na zaidi ya hapo anaonekana kama hajiamini kwamba atashinda, na hivyo anaogopa kuji expose for nothing.
Pili kama hukujiandikisha jimbo lake huwezi kumsaidia kwa kura ila kama anahitaji msaada ataandikia watu barua pepe.
Anajuaje kwamba wana JF hawajajiandikisha jimboni kwake ? Siku hizi mtandao upo kila kona TZ. Anajuaje kwamba hawezi ku spark cheche moja itakayoanzisha wildfire katika campaign yake ? Anajuaje anahitaji msaada wa aina gani na wa aina gani hahitaji ? Mpiga kampeni makini ni yule aliye tayari kusikiliza mawazo tofauti ya watu tofauti kuhusu kampeni yake, sasa watu watampa input gani ya maana wakati hata hawajui jimbo gani anagombea ?
Au kaja kutuambia anagombea ubunge kama showoff tu ?
Tatu, kama wewe upo jimboni kwake sidhani kama utampigia kura kwa sababu yupo JF isipokuwa kutokana na kujiuza kwa chama na YEYE hata kama akiwa ni Malaria_Sugu.
Right, lakini kama akitumia platform ya JF kutueleza mipango yake, atawapa nafasi watu kupata mambo fulani ambayo hawawezi kuyapata kirahisi kwa njia nyingine yoyote, mfano interactivity. Zaidi ya hayo, haki ya kupiga kura ni ya wananchi wa jimboni kwake, lakini hii haimaanishi mjadala wa mchakato wa ubunge unaishia kwa wananchi wa jimboni kwake, ingekuwa hivyo magazeti national yasingecover mbio za ubunge.Jf ni kama gazeti na watu wa JF wana haki ya kuuliza hata kama hawana haki ya kupiga kura. Sasa kama hataki kujitambulisha wengine watasema anaogopa maswali na hana skills za uongozi.
Haya ndiyo mabadiliko tunayotaka ? Wabunge waoga hata kufanya kampeni ? Kweli wanaweza kwenda kupingana na status quo ya ufisadi kwenye mjengo ?