Natumia jina langu halisi pia. lakini tunajali mawazo zaidi kuliko identity ya mtu
Hii ina apply kwa JF members, ukishatuambia kwamba unavaa kofia ya mgombea ubunge kofia inayo apply inakuwa ya mgombea ubunge.
Huwezi kutaka kuwa public servant kwa usiri siri, public service na usiri haviendani, mtu anayetaka public service anatakiwa kuwa transparent.
Ukishavaa kofia ya ugombea ubunge una chaguzi mbili,
1.ujitaje jina lako na la jimbo lako, essentially ufanye kampeni hata kama ni kwa kujitambulisha tu. Huwezi kusema wewe umeshinda kura ya maoni kugombea ubunge bila kutaja jimbo na jina lako, kwa sababu kauli hii itakuwa haina uzito na haina tofauti na ndoto na hadithi za alinacha, how can anybody take you seriously? Indeed how can anybody verify what you are saying?
2. Usijitaje jina, uwambie watu kwamba una value usiri wako sana kuliko kazi ya kuongoza watu.Na kwa sababu ukisma hivi utajionyesha usivyo na perspective, usivyo na priority, usivyojua sacrifice za uongozi, tayari moja kwa moja utakuwa ume ji disqualify.
If anything kama ulikuwa hutaki kuhusisha maisha yako ya JF kabla ya kampeni ya ubunge na haya ya kampeni, ungeweza kirahisi kabisa kuomba ID nyingine, ambayo ingekutambulisha rasmi kama mgombea ubunge fulani wa jimbo fulani, hapa pasingekuwa na tatizo la ku compromise privacy ya ID yako.
Mimi napata matatizo sana na mtu anayetaka kufanya kampeni huku anaweka usiri,naona kuna woga hapo, hamna uwazi hapo, hakuna uwezo wa maamuzi hapo, hakuna kuelewa kazi ya utumishi wa umma hapo, kila indicator inanionyesha matatizo matupu mbeleni kwa mbunge kama huyu.