Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
GS kama unanisikia endelea kujificha hivo hivo usionyeshe identity yako kwanza maana nawajua waswahili badala ya kukusafisha watakuchafua, wanajifanya sasa wanakupenda eti wanataka kukupa ushauri, utakapojionyesha tu utaniambia, kama wanakitu cha zaidi wataku PM.

Cha muhimu wewe nenda ongea na wapiga kura wako kama kuna member mtakutana naye kwenye field jua huyo ndiye supporter halisi sisi wengine ni wapiga domo tu ndugu yangu, jitambulishe uone moto watu wanaweza kukufungia safari waje jimboni kukumaliza believe me or not muulize Mwakalinga a.k.a Mtanzania atakusimulia.

Wanatolea mifano ya Dr. Slaa, Mnyika na Zitto, hawajui hao wamejiunga JF wakiwa tayari public figures. Kama ulivyosema kisisasa wewe bado mchanga komaa kwanza ndipo ujitambulishe hapa, hata kinda la njiwa hufundishwa kuruka kwa kupiga piga mabawa ndani ya kibweta kabla ya kutolewa nje, ila kama litajifanya limeshajua litaachwa litelemke chini ya mti na halitaweza kupanda tena. Take or don't take my opinion.

Angekuwa anataka kufanya hivyo aingesema kitu kuhusu ugombea wak hapa. Angewasiliana na watu privately.

Sasa watu tukisema huyu hana sifa wala uwezo wa kuongoza, na ni bishoo tu kaja kutulingishia kushinda kura ya maoni utakataa?

Mtu aliye serious na uchaguzi anaendesha kampeni mpaka sehemu nyingine ambazo hazifai, leo mtu ana uwanja anajidai usiri? Anaogopa nini?

Hatutaki wabunge waoga.
 
Hujanielewa inategemea unajificha wapi unaweza kujulikana kwenye TV lakini wapigakura wako wasikujue, hata wote JF tukimjua leo tutamsaidia nini, yeye amesema alikuwa jimboni kwa wiki tatu na alifanya hivyo bila wewe kujua.

Huko jimboni nako aliwakataza watu wasimwulize maswali?

Na unauliza hata tukimjua wote hapa JF tutamsaidia nini? Kama hatuna msaada wowote ule kwake kwa nini kajisumbua kuja kutuhabarisha kwamba atapeperusha bendera ya CHADEMA?
 
Angekuwa anataka kufanya hivyo aingesema kitu kuhusu ugombea wak hapa. Angewasiliana na watu privately.
Ukimsoma vizuri GS ni kama alikuwa anatoa taarifa tu kwa Members wenzake, vile vile ukisoma paragraph ya mwisho kasema tusimuulize inawezekana kabisa ana sababu zake. Sasa kama hukubaliani naye au unataka details zaidi unaweza kum PM.
 
The problem is that she is a rookie. No astute politician will say such nonsense!
 
Ukimsoma vizuri GS ni kama alikuwa anatoa taarifa tu kwa Members wenzake, vile vile ukisoma paragraph ya mwisho kasema tusimuulize inawezekana kabisa ana sababu zake. Sasa kama hukubaliani naye au unataka details zaidi unaweza kum PM.

Of course alikuwa anatoa taarifa kwa members wenzake, n mimi kama member mwenzake nime expose a fatal flaw katika kutoa taarifa hiyo, kwamba kama alikuwa hataki maswali asingetoa taarifa, maadam anataka uwakilishi maswali ni jadi ya hii kazi. Huwezi kuwa daktari wa upasuaji uanyetakiwa kuwapasua watu halafu hapo hapo unaogopa damu, ukiona damu tu unazimia na kutapika, utakuwa umeingilia kazi za watu. Huwezi kutaka ubunge halafu unataka kufanya mambo kisiri, utashindwa kabla ya kuanza.

Hii culture ya "tusimuulize" itatufugia mafisadi, leo anafanya kampeni tunasema tusimuulize, atapata ubunge kwa usirisiri, kesho atataka kuendesha ubunge kisirisiri, mwishowe yatakuwa mambo ya aibu.

Hapa ni mwendo wa uwazi, maadam kashasema mwenyewe kazi anaitaka hana budi kukubali uwazi, ama sivyo tutamuona mzugaji tu na mwoga wa mwisho.
 
Jamani ninawashukuru sana.Tupo pamoja,bado niko jimboni nafanya maandalizi kadhaa ya namna ya kujitambulisha..

Fidel endelea na maombi usiishie hapo,mambo ndio kwanza yameanza.bht afadhali umsisitize Fidel aanze kuomba for Dr Slaa nashangaa kwanini mpaka sasa alikuwa bado hajaanza,lakini hata hivyo hajachelewa kwa kuwa kwa MUNGU hakuna kuchelewa.

Dah nilizidisha maombi kwako kwanza.
Sasa nimehamia kwa Dr. mpaka kieleweke.
 
GS naona watu wanaanza kukukatisha tamaa...piga moyo konde songa mbele ...never let anyone tell you that you cant do it....yes you can..!
 
Kiranga,
Mimi nadhani GS ana kila haki ya kutojieleza hapa kwa jimbo lake. Na hakika ni vizuri wananchi wampigie kura kwa jinsi atakavyojiuza kuliko kumpa kura au support kwa sababu ni mwana JF. Kuhusu maswali nadhani kama wewe ni mgonjwa sidhani kama daktari anatakiwa kukupa vitisho vya damu itakavyo kutoka ktk upasuaji. Unamwona anajificha kwa sababu hujaingia chumba cha upasuaji, upo nje unataka kumwona daktari umhoji ili iwe nini?.
Binafsi nafikiri tumpe muda na tumpe maswali yanayolingana na nafasi yake. Ni vizuri zaidi tukitumia utamaduni wa kuuliza uwezo wake kuwakilisha wananchi badala ya kutaka kujua anafanana vipi kwani ndivyo wadanganyika wengi huchagua viongozi wao.
 
Hamna lolote, kama alikuwa hataki maswali sasa kaja kusema ili iweje?

Mimi namuona kama mtu anayependa show off na celebrity ya ugombea ubunge wakati hataki kufanya kazi ya kuwaridhisha wananchi kwa kujibu hoja, ni mwoga na quite possibly ana vitu vya kuficha.

Anataka kuila keki yake, halafu anataka ibaki. Anataka kuwatangazia watu kwamba anagombea ubunge, halafu hataki kuwaambia kikamilifu, dalili za usirisiri na undumilakuwili mbaya hizi.

N ninakupa guarantee kwamba, hata kama huyu si muhuni anayetaka kutuchezea akili tu hapa kwa maana ya kwamba hagombei popote (how can you dispute that) hata kama ni kweli anagombea, kashajionyesha kwamba yuko timid na hawezi kushindana na the CCM machine.
 
Huyu jamaa ni kituko cha mwaka! anani kumbusha zama za mchezaji mmoja wa zamani akiitwa Edward Hiza yeye anadai watu wakijaa uwanjani anababaika hawezi kucheza vizuri, sasa soka linanoga kwa uwepo wa watazamaji yeye hawataki! design ndio GS.

Hawa ndio viongozi m-badala kutoka chama m-badala michosho mitupu!
 
Hongera sana GS kila la kheri mimi nakushauri usi disclose identity yako
 
Huyu jamaa ni kituko cha mwaka! anani kumbusha zama za mchezaji mmoja wa zamani akiitwa Edward Hiza yeye anadai watu wakijaa uwanjani anababaika hawezi kucheza vizuri, sasa soka linanoga kwa uwepo wa watazamaji yeye hawataki! design ndio GS.

Hawa ndio viongozi m-badala kutoka chama m-badala michosho mitupu!

kanda2 hiyo analogy imenimaliza.
 
its gud GS.
Nakutakia mafanikio mema.
Lenga kushinda Ubunge na siyo "Viti Maaluma"
Dont take consituent as credit for "special seat".
You will be a good leader.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom