Kiranga sijui ni kwanini mimi nawewe huwa hatuelewani..Nimesema kuna mtu alijenga hoja zilizoenda shule na ninarafiki yangu wa karibu,wala sijatunga nitunge ili iweje?ooh no..Sikutaka kujitaja wala sio kwamba sina msisimko ningekuwa sina wala nisingethbutu kugombea at the first place.Nilijificha kwa sababu ninazozijua mimi,mbona kule face book nilijiweka wazi?mbona kwenye vyombo mbalimbali habari ziko wazi?Ha ha ha,siko proactive,sina initiative,kugombea sio kitendo cha kishujaa,wewe unafikri kutaja jina lako halisi JF ndio initiative?hivi wewe umeanzisha nini cha maana hata humu Jf tu?
Mimi siko kama unavyoniweka,jaribu kufuatilia posts zangu zote humu na waulize watu wa karibu wanaonifahamu kama vile Mnyika,Dr Slaa,Mbowe,Zitto na wengineo wa CHADEMA na niliosoma nao wa kuanzia shule ya msingi haid chuoni they will tell you,Regia ni mtu wa namna gani..
Kifupi ni kwamba hoja zako wala sio costructive kama unavyodhani bali bi destructive...Kuniambia kwamba eti naweza nisifike mbali kwenye kampeni zangu hivi unafikiri hii inajenga?kisa eti nikubaliane na mawzo yako.Be blessed..
Mimi nimeanzisha cha maana hapa JF kukulazimisha wewe utaje jina lako, sio tunauziana mbuzi ndani ya gunia hapa.
Tatizo letu hatuwezi kuchukua constructive criticism.Ukweli ni kwamba unavyojibu hoja, unavyolialia, ulivyokosa initiative unaoneka huna ukomavu kisiasa na hunipi imani kwamba utashinda Kilombero, siyo kwa spidi hii.
Kuna wengine tunatoa kitu na boksi. Watu kama wanakupigia kura wanakupigia kwa sababu mgombea wa CHADEMA tu, na labda kwa sababu CCM ni incumbent wamebweteka, lakini huwezi kuniambia mpaka sasa umetuonyesha qualities za leadership.
Leadership gani hii ya kutaka kulia kutokana na makombora ya Kiranga hapa?
Huwezi kutegemea watu tukuamini kwa kusema kuna mtu alijenga hoja zilizoenda shule, hata mtu mwenyewe huwezi kumtaja ingawa jambo lenyewe (hoja zilizoenda shule) si dhambi, na actually ni jambo la fahari, sasa hata huyu naye unataka kuleta usiri katika hili. Tunarudi kule kule tulikokataa, kwa kuuziana mbuzi kwenye gunia, hatujui kama unatudanganya au ni kweli.
Watu wanaenda kwa verification, usipoweza kutupa verification usituambie kitu, kama huwezi kututajia jina lako na jimbo unalogombea usituambie unagombea. Kama huwezi kutuambia hata JF name (not real name) ya huyu muungwana, unaonekana unatunga hadithi tu, huna verification.Utafika mjengoni na kusema mambo bila verification ? Mara nyingine hata kama unasema kweli, bila verification huwezi kujitenga na waongo, muulize Kubenea akupe uzoefu wake na hili. Kwa hiyo nikisema huna exposure unaonyesha wazi kwamba huna exposure kwa mambo kama haya na wala si kwamba nakuzushia.
Unataka niwaulize watu wa karibu kama wako biased je? Kuna mtu wa karibu kaja hapa kashtuka kukuona unagombea, ingawa na yeye tunaweza kumuomba ushahidi zaidi wa mshtuko wake, kama ni ule wa "namjua huyu alikuwa mzembe mzembe tu chuoni" au "huyu alikuwa na tabia mbaya hii na ile"
Of course utasema hoja zangu si constructive na ni destructive, si zinakuliza na huwezi kuzijibu. nimeonyesha kwamba huna initiative, nimeonyesha kwamba huna exposure, nimeonyesha kwamba huna kipaji cha kuku set apart ukawa muwakilishi wa watu. Hata mjadala wa JF kuufuatilia tu unakushinda.
Siri siri siri, siri moja baada ya nyingine.
Yaani hapa tunategemea chama tu, lakini mgombea hamna. Na kwa chama kuchagua mgombea aliye intellectually weak kama huyu, ambaye hana hata talent ya commanding respect in communication - something an MP is supposed to do a lot- hata chama nacho kinanionyesha kwamba kiko weak.