DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
WhatsApp Image 2026-09-11 at 17.23.462.jpeg
WhatsApp Image 2026-09-11 at 17.23.46w.jpeg
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
WhatsApp Image 2026-09-11 at 17.23.46.jpeg
WhatsApp Image 2026-09-11 at 17.23.45.jpeg
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
 
Hapa Tayari Gaming Board wameshachukua million 3 yako kwaajili ya kukunyamazisha, hii nchi inanuka rushwa sana.
 
Mnapata wapi nguvu ya ku-bet kampuni uchwara kama hizi.?
Kampuni uchwara zinapata nguvu wapi kufanya wanayo fanya hata baada ya kuitwa na gaming board? Ilibidi huyu jamaa awe amelipwa na fidia juu na kampuni kupigwa fine.

Japo katika maelezo haya inaonekana kuna sehem ya story ina miss.

N hajaeleza kwanini asitumie wanasheria wamsaidie swala hili?

Kampuni inatoa sababu gani za msingi za kutolipa?
Mwisho wa siku wakimwona ni mwiba kwao wanaweza kumpoteza.
 
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
Nitafute, twende mahakamani. Haki ya kisheria, inadaiwa kisheria na sio kwa njia nyingine. Njoo tupambane na hao wadaiwa wako, upate haki yako. Nicheki DM au kwa 0713368153
 
Dah!! Pole sana wanataka kukutapeli waziwazi hata jina tu la hiyo kampuni limekaa kiuwizi wizi tu, umewapiga parefu wameshindwa kukulipa , kama gaming board wameshindwa kukusaidia nenda wizarani kabisa uonane na waziri wa michezo ijapokuwa ni process ndefu ila unaweza kusaidika, na kwakuwa umelileta suala lako JF naamini litafika mbali na utapata usaidizi
 
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
 
Attachments

  • 1000024076.jpg
    1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 16
Mimi stori yangu ipo hivi nilicheza 1xBet na kwa bahati nikapata ushindi wa kama TSh milioni 3.8. Nikaamua kufanya withdrawal, lakini baada ya ku-request hela nikakutana na security verification.
Wakanitaka ni-verify kwa passport pamoja na namba ya simu iliyokuwa kwenye account.

Tatizo ni kwamba hii namba niliitumia wakati nafanya account, lakini SIM yenyewe niliinunua kwa mtu. Siwezi ku verify identity wanatishia ku block tena wanasema namba ina account 2

Haya makampuni ya kijinga sana yakiona umeyakula
 
Back
Top Bottom