DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
Mkuu nilikuwa sijasoma ripoti nzima aisee! Hapa kilichobaki ni kuishtaki Gaming Board kwa kukwamisha suala lako. Waite gaming board mahakamani na pia jitahidi kuita vyombo vya habari visaidie kuripoti taarifa yako. Huenda ikiwafikia wakubwa wakakusaidia kupaza sauti.
 
Hakuna makampuni yan rules ngumu kama kampuni la 1xbet la kirus na makampuni yaliyo copy hilo kampuni mfano paripesa yale yana masharti kibao sana.

Ukicheza kidogo huna akaunti..yani wale wakivurugwa huna akaunti nenda nao taratibu tu.
Wame copy kivipi mkuu🤣
 
Kampuni uchwara zinapata nguvu wapi kufanya wanayo fanya hata baada ya kuitwa na gaming board? Ilibidi huyu jamaa awe amelipwa na fidia juu na kampuni kupigwa fine.

Japo katika maelezo haya inaonekana kuna sehem ya story ina miss.

N hajaeleza kwanini asitumie wanasheria wamsaidie swala hili?

Kampuni inatoa sababu gani za msingi za kutolipa?
Mwisho wa siku wakimwona ni mwiba kwao wanaweza kumpoteza.
Kwa nilivyoelewa mkeka wake ulitakiwa ule 27.7m, pigabet wakaucancel wakarudisha stake yake. Huu mchezo wanafanya wengi sana.
 
We kwa akili yako hatuwezi kujafili jambo. Yaani uneweka 10,000 umekula 27M unazani nani anapata hasara hapo wakikupa?
Bwana mdogo wewe huifahamu biashara ya betting kaa utulie. Betting ni biashara inayotengeneza faida kubwa na biashara kama zilivyo biashara nyingine. Wewe unaangalia yeye aliyepata vipi kuhusu hao waliopoteza?
 
Wanasema ongeza viambatanisho mkuu
Screenshot_20261014-213922.png
 
Back
Top Bottom