DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hapo wewe ndio una makosa. Ingawa ku verify kwa njia ya passport ni kukuonea.
 
Suala lako ni toafauti mkuu wewe umepata haki yako kwasababu ni kosa kuwa na account zaidi ya moja pia ili uweze kutoa pesa nilazima utimize KYC Kwa mujibu wa sheria,, sasa utatoaje pesa bila ku verify account?
 
Afungue tu account kwa sababu hata akijificha kama guest hamsaidii kwa kuwa shauri lake linafahamika na anao walalamikia.

Tena wa nataka nipige picha nikiwa nimeshika passport na kuandika tarehe ya Leo na niweke proof kama hio namba ni ya kwangu kumbuka niko nje sina ile ID YA hii nchi sikuweza kusajili line kwa jina langu
 
Terma na condition zipoje? Ikiwa bet ilikubali kuwa placed maana yake kampuni inaweza kulipa. Hiyo sio sababu inayo fanya huyu asilipwe. Bado kuna kitu hajatuambia.
Katika waliochangia hapo mkuu wewe umetumia akili. Ili kampuni isikulipe ni either umeweka fixed game ambazo hazilipwi hata uende wapi. Pili kama ilikuwa ni bonasi na hujatimiza masharti ya bonasi. Milion 27 ni pesa ndogo sana kwa pigabet na haitatolea kampuni iruhusu kuweka ticket ambayo hawawezi kuilipa
 
Tena wa nataka nipige picha nikiwa nimeshika passport na kuandika tarehe ya Leo na niweke proof kama hio namba ni ya kwangu kumbuka niko nje sina ile ID YA hii nchi sikuweza kusajili line kwa jina langu
Verification nijambo la lazima mkuu,, ili kuzuia mtu asiibe account ya mtu mwingine pia ni sheria ya fedha kampuni za betting nilazima zifanye KYC ukitimiza hayo watakulipa pesa yako
 
Hapo Gaming Board ishapigwa mpunga, unatakiwa uishitaki kisheria pia gaming board mahakamani. Maana baada ya kushindwa kuwasuluhisha walitakiwa kukupa go ahead ya mahakamani.
Omba ufafanuzi wa kisheria mahakamani ili wote, Gaming board na Pigabet waje kusikiliza shauri kwa summons.
Watikise namna hiyo, hivi hivi hutapata hela hiyo, ambayo kimsingi ni haki yako. 😊
 
Kabla ya kwenda huko mahakamani ahakikishe mkeka wake sio fixed na ameshauliza sababu za yeye kutokulipwa ,, ila suala la kusema milion 27 kushindwa kumlipa sio sababu ya msingi maana hata leseni yao tu na domain yao inazidi hiyo pesa so Wataikamata alipwe pesa yake
 
Betway hawana longo longo.
Unamaliza kila kitu online.
Una deposite, withdraw pesa yako kwa njia ya simu bila verification Kibao au mauzauza ya pigabet na 1xbet au galsports au betpawa.
Aliyekwambia betway hawafanyi KYC Ninani? Acha upotoshaji mkuu. Shinda hela kubwa halafu uone kama unaweza kutoa bila kuthibitisha account yako ,, ulivyo fala unadhani unaweza kuruhusiwa kutoa milion 20 kwenye account ? Vipi kama umehack mfumo 🤣
 
Wahuni hao, tumalize hili kwanza
https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/watch/?v=988605313638635
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…