Nimeshindwa kulifungua begi la marehemu Mama yangu

Nimeshindwa kulifungua begi la marehemu Mama yangu

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Huenda ni kiandika haya naweza kupata faraja na comfort kutoka kwa wadao walio wahi kupitia hali kama hi (death trauma). Tarahe 13 June mwaka jana nilipoteza mama angu kipenzi, ni lipitia wakati mugumu sana kukubaliana na ukweli kama mama amefariki kweli, cijawahi kulia tangu ukibwani ila ni lilia kama mtoto mdogo kwa siku zaidi ya tano na mkia kaburini ili raho na nafsi yangu zikubaliane na ukweli kwamba ni kweli Mama amekufa na hatarudi.

Lakini bado niliendelea tu kulia na kuumia mpaka leo licha ya kua mimi ni mtu mzima of early 40s, kifo cha mama asikuambie mtu acha tu hakisahuliki, licha ya kua Baba mzazi alitangulia mbele ya haki miezi miwili nyuma ila sikua traumatised kama kifo cha Mama mpaka leo bado siamini, chagamoto eliopo sasa ni hi alinikabidhi begi lake lenye kila kitu chake chamaana kabla ya kusafiri vikiwemo na hati vyeti funguo nguo zake na vyakwangu pia.

Kila na potaka kulifungua begi na shindwa natetemeka na kububujika machozi na simanzi za hali ya juu, ni lijipa mwoyo kwamba huu mwaka kipindi cha likizo ya sense nta lifungua ila tena ni meshindwa nimelirudisha juu kwenye undrop, sitaki kulazimisha roho yangu na wakika nilio nao mama angu hakuamini ushirikina, ni lipenda mama angu sanaa kuliko anything lakini kinacho niuma zaidi naona kama nateseka peke yangu kaka zangu na wadogo zangu, wako oky normal sanaa hata hawakulia kwenye msiba wakulia kama mimi, licha yakua alikua ana wasaidia kupitia kwangu, kwasabb na wazidi kila kitu na nimeishi na mama ngu tangu ni memaliza Chuo 2008.
 
Kaka yng kaza roho jua kila nafsi itarudi kwa muumba wake. Mm mwaka 2015 mwezi wa 3 mama yng aliaga dunia kibaya zaid nilkuwa nje ya nchi kabla ya kuondoka kwenda nje nlkuwa naishi nae nlmuuguza mpaka alpopona kbsa nkasafiri baadae alfarki nikiwa sipo, najua maumivu yake ila kuwa Mwanaume sasa mwache apumzke
 
Huko kote nimekuelewa kabisa mkuu, na naungana na wewe kwenye haya maumivu, ninayajua sana ila kitu nachotaka kukupinga na kukutahadharisha futa kabisa hiyo roho unayotaka kuikaribisha kwa kusema 'lakini kinacho niuma zaidi naona kama nateseka peke yangu kaka zangu na wadogo zangu, wako oky normal sanaa hata hawakulia kwenye msiba wakulia kama mimi, licha yakua alikua ana wasaidia kupitia kwangu, kwasabb na wazidi kila kitu na nimeishi na mama ngu tangu ni memaliza Chuo 2008'

Jenga ukaribu na hao ndugu zako. Usianze kabisa kuona gap kati yenu. Kumbuka baba kafariki na mama kafariki, ni rahisi sana kuparaganyika kama ndugu. Binadamu tumeumbwa tofauti katika mapokeo ya vitu mbali mbali na ukimya wa ndugu zako haimaanishi wao hawakumpenda mama zaidi yako. Kama nakuelewa wewe ndio mkubwa, basi chukua nafasi yako kama kaka mkubwa na kumbuka no matter what maisha lazima yaendelee

Amka chukua begi fungua. Huwezi kujua labda kuna kitu kinataka kufanyiwa kazi kwenye begi na siku zinazidi kwenda
 
Mkuu pole sana I know what it means .....Kweli na jitahidi sana kwasasa uwezo wakulibeba begi nimeanza kuupata nyuma hata kuona nguo zake nilikua nalia sanaa, ila sasa hivi naweza kiasi, najua ntaweza tu, kaka mimi nimepitia mengi mimi ni hustler wa maisha ila hili limeniweza linagusa my pscho and mental ila litaisha
 
Huko kote nimekuelewa kabisa mkuu, na naungana na wewe kwenye haya maumivu, ninayajua sana ila kitu nachotaka kukupinga na kukutahadharisha futa kabisa hiyo roho unayotaka kuikaribisha kwa kusema 'lakini kinacho niuma zaidi naona kama nateseka peke yangu kaka zangu na wadogo zangu, wako oky normal sanaa hata hawakulia kwenye msiba wakulia kama mimi, licha yakua alikua ana wasaidia kupitia kwangu, kwasabb na wazidi kila kitu na nimeishi na mama ngu tangu ni memaliza Chuo 2008'

Jenga ukaribu na hao ndugu zako. Usianze kabisa kuona gap kati yenu. Kumbuka baba kafariki na mama kafariki, ni rahisi sana kuparaganyika kama ndugu. Binadamu tumeumbwa tofauti katika mapokeo ya vitu mbali mbali na ukimya wa ndugu zako haimaanishi wao hawakumpenda mama zaidi yako. Kama nakuelewa wewe ndio mkubwa, basi chukua nafasi yako kama kaka mkubwa na kumbuka no matter what maisha lazima yaendelee

Amka chukua begi fungua. Huwezi kujua labda kuna kitu kinataka kufanyiwa kazi kwenye begi na siku zinazidi kwenda
Ahsante sanaa mkuu ubalikiwe sanaa kwa mchango hu, kwanini ni mesema hivo ni kwasabb mimi sio mkubwa wao mimi ni number 3 kati ya watoto sita, wengine siku ya 40 hawakuweza kufika, bila sabb za msingi
 
Pole sana, usilie kama watu wasio na matumaini. Shirikisha ndugu zako mfungue hilo begi kama unaona lina umhimu.
 
Pole sana, usilie kama watu wasio na matumaini. Shirikisha ndugu zako mfungue hilo begi kama unaona lina umhimu.
Umuhimu upo kwa kweli na lazima nilifungue kabla ya mwaka hu kuisha
 
Kama una mume/mke mshirikiane kufungua begi kwa pamoja kama hao ndugu zako wa kuzaliwa hawapo interested.
Na endapo na huyo mwenzio hapendi mm nipo tayari kuja kukusaidia kulifungua.
Nimeona umeandika "ulimpenda sana mama yako kuliko chochote" binafsi nadhani hapo ulikosea ulitakiwa kumpenda sana Mungu kuliko chochote maana yeye hafariki anaishi milele.
Ni kweli tunawapenda wazazi wetu lakini wasiwe zaidi ya Mungu.

Pole sana kwa kufiwa na wazazi wako.
Be strong.
 
Lazima nilifungue kabla ya mwaka hu kuisha
Mkuu unawezaje kusema "lazima" wakati hakuna binadam aijuae kesho yake itakuaje?
Je kama haukupangiwa kufikisha hata week ijayo itakuaje?
Una ahadi na Mungu kwamba utaishi hapa duniani kwa muda gani?

Piga moyo konde, muombe Mungu ujasiri wa kulifungua hilo begi kwa usalama, na kama walivyosema baadhi ya wadau kwamb sio mbaya kuwashirikisha na ndugu zako.
Unaweza kuwambia tu, so watakaokuwa tayari mtalifungua pamoj nao, na wale ambao hawako tayari kulifungua basi mtaachana nao.
 
Kama una mume/mke mshirikiane kufungua begi kwa pamoja kama hao ndugu zako wa kuzaliwa hawapo interested.
Na endapo na huyo mwenzio hapendi mm nipo tayari kuja kukusaidia kulifungua.
Nimeona umeandika "ulimpenda sana mama yako kuliko chochote" binafsi nadhani hapo ulikosea ulitakiwa kumpenda sana Mungu kuliko chochote maana yeye hafariki anaishi milele.
Ni kweli tunawapenda wazazi wetu lakini wasiwe zaidi ya Mungu.

Pole sana kwa kufiwa na wazazi wako.
Be strong.
Umenena kweli 🙏
 
Back
Top Bottom