Nimeshindwa kumwelewa huyu Muingereza

Nimeshindwa kumwelewa huyu Muingereza

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Habari za leo, nilikuwa napiga story na mwingereza mmoja ambaye amewekeza kwenye sekta ya utalii hapa nchini hususani katika hoteli za kitalii, tulizungumza mengi kuhusu utalii nchini Tanzania.

Nilipo muuliza kuhusu namna alivyojipanga kupokea lundo la watalii baada ya filamu ya Royal Tour kuzinduliwa miezi michache ijayo, akacheka sana. Akaniamia "it was wastage of time" nikamuuliza kivipi akasema watu wazima hawapaswi kujadiliana utoto hivyo tubadili mada.

Nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu bwana.
 
INAHITAJI ZAIDI YA DOCUMENTARY KUKUZA UTALII

Ili mtalii akija TZ ibaki katika kumbukumbu za maisha yake Kama sehemu bora kabisa Basi hatuna budi kuchukua hatua zaidi ya documentary na ubaya ni kwamba huo userious hatuna

Kama kuna documentary ya Hawaii,Malibu au Ibiza then Nina uhakika ilikuja baada ya watu wengi kutembelea maeneo hayo na siyo Kabla
 
Hahahaha huenda akawa yupo sahihi lkn pia huenda akawa hayupo sahihi

Anachokiamini yy ni uwezo wake wa kujipambanua ili kukuza biashara yake

Lakini pia kimtazamo wa serikali kuwa na kitu kama iyo ROYAL TOUR ni sahihi sababu wameona kwa mataifa waliyofanya iyo approach na kufanikiwa

kwahiyo pande zote mbili zina mitazamo tofauti na hii ni kitu ya kawaida tu
 
Wengi wa hawa watu ninavyowafahamu hawajapenda abadani mtu mweusi ku run tourism businesses! Ujio wa technology ya internet ilitibua sana umiliki wa hii industry kwao! Lakini kama haitoshi, serikali iwekeze zaidi kwenye vichwa vya vijana na itumie vipaji vya vijana kukuza utalii na ubunifu katika marketing!

Miji na halmashauri ziwe bunifu saana katika mambo ya utalii haswa matamasha, foods seasons festivals na restaurants uniques , vitu kama hivi vinavuta watalii sana! Serikali na wizara husika toeni motisha vijana wajitokeze na ubunifu wa utalii na muwawezeshe hii kutegemea mbuga za wanyama tu haitoshi kuna watu mtaani wanavipaji ambavyo ni utalii tosha na wa nguvu!
 
Endelea kupiga nae story hadi mfikie conclusion..
 
Sisi Tanzania tunajivunia sana vivutio vya asili tulivyobarikiwa kuwa navyo, lakini bado tunapaswa kuweka miundombinu rafiki ya watu kuvifikia vivutio hivyo, na mazingira rafiki kwenye miji yetu, mifumo ya usafiri wa umma na hata gharama za maisha.

Naamini kuna nchi hazina vivutio vya asili, lakini zina mazingira rafiki sana ambayo yanavuta watalii wengi kwenda nchi zao kuliko sisi.

Mfano kwa jiji la Dar es salaam, kwa sehemu kubwa halina sehemu za umma za mapumziko (bustani), na bado mazingira ya usafiri wa umma sio rafiki sana kwa sasa, sababu ya foleni za barabarani na kukosekana ustaarabu kwa waendeshaji na watumiaji wa usafiri huo.

Taarifa nyingi hazipatikani kwa urahisi mitandaoni. Mfano kuna kipindi nilikuwa natafuta taarifa za kufika Mafia mtandaoni lakini sikuweza pata taarifa za kunitosha kufanya maamuzi juu ya safari hiyo nikaipotezea.
 
Habari za leo, nilikuwa napiga story na mwingereza mmoja ambaye amewekeza kwenye sekta ya utalii hapa nchini hususani katika hoteli za kitalii, tulizungumza mengi kuhusu utalii nchini Tanzania.

Nilipo muuliza kuhusu namna alivyojipanga kupokea lundo la watalii baada ya filamu ya Royal Tour kuzinduliwa miezi michache ijayo, akacheka sana. Akaniamia "it was wastage of time" nikamuuliza kivipi akasema watu wazima hawapaswi kujadiliana utoto hivyo tubadili mada.

Nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu bwana.
Nafikiri sio kutangaza tuu utalii, lazima kuwatengenezea mazingira ya utalii, barabara nzuri, usafiri, kuondoa rushwa kila sehemu, wizi ( usalama wao) nk. Mabalozi wangeweza kufanya hii kazi ya kutangaza utalii wa nchi
 
Wengi wa hawa watu ninavyowafahamu hawajapenda abadani mtu mweusi ku run tourism businesses! Ujio wa technology ya internet ilitibua sana umiliki wa hii industry kwao! Lakini kama haitoshi, serikali iwekeze zaidi kwenye vichwa vya vijana na itumie vipaji vya vijana kukuza utalii na ubunifu katika marketing!

Miji na halmashauri ziwe bunifu saana katika mambo ya utalii haswa matamasha, foods seasons festivals na restaurants uniques , vitu kama hivi vinavuta watalii sana! Serikali na wizara husika toeni motisha vijana wajitokeze na ubunifu wa utalii na muwawezeshe hii kutegemea mbuga za wanyama tu haitoshi kuna watu mtaani wanavipaji ambavyo ni utalii tosha na wa nguvu!
Extraordinary
 
Wazungu uzalenfo wa nationalism kuliko waswahili

Royal tour ilifanywa na wamarekani sio waingereza
Sasa wewe mleta mada unapomhoji mwingireza kuhusu royal tour iliyofanywa na mmarekani ulitaka ajibuje asifie marekani au?

Hata ungemuuliza msweden au mrusi angekujibu hivyo hivyo
Ndio maana akawa mkali kuwa achana kabisa na hiyo hoja alishachukia hapo ungeendelea kuhoji why angekutukana matusi kuwa nimekwambia acha you cockroach
 
Umeshindwa kumuelewa kwasababu Huna Akili na yeye pia Hana Akili

Habari za leo, nilikuwa napiga story na mwingereza mmoja ambaye amewekeza kwenye sekta ya utalii hapa nchini hususani katika hoteli za kitalii, tulizungumza mengi kuhusu utalii nchini Tanzania.

Nilipo muuliza kuhusu namna alivyojipanga kupokea lundo la watalii baada ya filamu ya Royal Tour kuzinduliwa miezi michache ijayo, akacheka sana. Akaniamia "it was wastage of time" nikamuuliza kivipi akasema watu wazima hawapaswi kujadiliana utoto hivyo tubadili mada.

Nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu bwana.
Inawezekana umeshindwa kumuelewa sababu hii Lugha ya Kiingereza INA CHANGAMOTO ZAKE
 
Habari za leo, nilikuwa napiga story na mwingereza mmoja ambaye amewekeza kwenye sekta ya utalii hapa nchini hususani katika hoteli za kitalii, tulizungumza mengi kuhusu utalii nchini Tanzania.

Nilipo muuliza kuhusu namna alivyojipanga kupokea lundo la watalii baada ya filamu ya Royal Tour kuzinduliwa miezi michache ijayo, akacheka sana. Akaniamia "it was wastage of time" nikamuuliza kivipi akasema watu wazima hawapaswi kujadiliana utoto hivyo tubadili mada.

Nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu bwana.
Wewe ukimpima kwa akili yako, uelewa wake yeye na wa kwako nani yuko juu ya mwingine? Isije ikawa ulimpiga swali ambalo asingeweza kutoa hoja kishahihi, akahofia kuwa jibu lake utalidharau hivyo akaona njia bora ni kukuacha kwenye mataa

Assuming kweli aliona kuwa it was a waste time, the fact kwamba yuko hapa nchini na mliyekuwa mnamwongelea ni Mkuu wa Nchi ambaye yeye huyo mgeni yupo kwenye nchi yake, mtu ambaye ana hekima angeweza kuvunga kwa kusifu huku moyoni akiwa anasema kuwa ilikuwa ni kupoteza muda. Mwenye hekima asingeweza kupasua hapo hapo kuwa "it was a waste of time"

Kuna mtu aliwahi kuletwa kijijini kwetu miaka ya mwanzoni mwa 90, na baada ya kumuona tu mimi nikawaambia kuwa huyu ni chizi, wakanikatalia. Unajua tena ngozi nyeupe halafu iko kijijini na inatembelea gari wakati msukuma wa kijijini hata baiskeli hana. Huyu mtu walikaa naye baada ya miaka michache sana kila mtu kijijini pale alikubaliana na mimi kuwa mtu huyo alikuwa chizi,
 
Back
Top Bottom