Nimeshindwa kuuthibiti wivu

Nimeshindwa kuuthibiti wivu

Ninachoamini sikuzote
Mapenzi hayaji kwa kulazimisha na wala hatokupenda kwa wivu uliokithiri
Maam hujamkuta bikra huwez mlinda acha ajilinde
Ukimlinda ni kazi bure

Cha muimu fanya yako
Jipende
Poteza mda wako katika mambo yako muhimu
Ukipata mda mpigie muongee usipopata mda usimpigie
Jipende na jipe thamani
Na akiona hili kwako lazima atakuona ana bahati kuwa na wewe
 
Wivu wa kumhisi mtu kitu hata kama huna ushahidi nacho ni hatari kwa afya yako.jiepushe na dhana(jumping to conclusions) ni hatari sana sio kwenye mapenzi tu,hata maisha ya kawaida,jifunze kuwa na mawazo chanya.

2.JIAMINI.mtoto wa kiume wewe usiwe na nafsi legevu,kama wa mpenda na ameonyesha kukupenda kwa kauli na vitendo waswas na gubu la nini ( wivu na gubu vinalandana).trust your self and your soulmate,tena ukizidisha wivu ndo unamtengenezea mazingira hatarishi ya .....

3.Give her space,hujamzaa huyo,usimgande sana,mpe uhuru aishi maisha yake,mwamini tu mwenzio mana akiamua kucheat worrying wont help.na anaweza akafanya na usijue.kama ni rizki yako basi hakuna atayeweza kukupindua.
 
Ukisikia kuanguka kwenye mapenzi ndio hiyo..sio wivu ni mapenzi..ila kumbuka moyo kazi yake kusukuma damu
 
INGAWA MIMI MWENYEWE NI MSHAURI WA MAPENZI NA MAHUSIANO LAKINI HILI LIMENISHINDA. NAOMBA MNISHAURI.

Ndugu zangu na marafiki zangu,

Naandika hili nikihitaji ushauri wa kina, ushauri ambao utaniondoa katika kadhia hili.

Naomba msiangalie mimi ni nani, naomba msiangalie kile ninachokifanya bali naomba mnishauri kama mwanaJF mwenzenu. Ingawa ni mwandishi wa Riwaya zinazohusu mahusiano, lakini kwa hili limenishinda kulitatua.

Ndugu zangu nasumbuliwa na wivu. Wivu ndio unaonisumbua na kunitesa. Nikimpigia mpenzi wangu na kukuta simu yake inatumika basi kwangu mimi ni ugomvi. Hata kama mpenzi wangu ameachana na X wake tena kabla hata yangu miye. Akinihadithia naumia utafikiri bado wapo kwenye mahusiano.

Suala kama hili limenipa matatizo makubwa sana. Niliachana na kugombana na Wapenzi wangu waliopita sababu ya hili. Hata huyu wa sasa sina imani kama tutafika. Nampenda na sihitaji kumuacha ama kumpoteza. Kuna wakati nakasirika na kutaka kufanya maamuzi ya kuachana na mpenzi wangu lakini baadae napuuza nakujiona kuwa mimi ni mpuuzi.

Kabla sijampoteza huyu niliyenae naomba ushauri wenu. Ni vipi naweza kujiondoa katika hili? Je ni kipi nifanye ili nisimpoteze huyu mpenzi wangu? Kuna kipindi nakasirika sana na kutaka kuamua lolote. Lakini mapenzi yangu kwake ni makubwa sana. Siwezi kumuacha. Hata mama yangu hataki nimuache huyu mwanamke.

NAOMBA MNISHAURI NI NINI NIKIFANYE ILI HILI LISINITOKEE?

NAOMBA MSAADA.
Pumzika kwa amani mkuu
 
Aisee wivu ni kwamba dhahiri humuamini mpenzi wako. Na ukimuoa ndo utazidi maradufu. Kwanza ondoa mawazo mabaya juu yake na kama ana zuri moja na mengine mabaya 9 basi upe kazi ya kuwaza hilo zuri moja na lipe kipaumbele na kusahau mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee wivu ni kwamba dhahiri humuamini mpenzi wako. Na ukimuoa ndo utazidi maradufu. Kwanza ondoa mawazo mabaya juu yake na kama ana zuri moja na mengine mabaya 9 basi upe kazi ya kuwaza hilo zuri moja na lipe kipaumbele na kusahau mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kulikoni kufufua huu uzi,!!??? Muhusika alishafariki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbele yako Nyuma yetu Kamanda.

Daima tutakukumbuka
 
Back
Top Bottom