Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani ni balaa. Hivi unazuiaje kwa mfano? 😕mmhh wivu hauzuiliki we jitaidi kupunguza tu
Pumzika kwa amani mkuuINGAWA MIMI MWENYEWE NI MSHAURI WA MAPENZI NA MAHUSIANO LAKINI HILI LIMENISHINDA. NAOMBA MNISHAURI.
Ndugu zangu na marafiki zangu,
Naandika hili nikihitaji ushauri wa kina, ushauri ambao utaniondoa katika kadhia hili.
Naomba msiangalie mimi ni nani, naomba msiangalie kile ninachokifanya bali naomba mnishauri kama mwanaJF mwenzenu. Ingawa ni mwandishi wa Riwaya zinazohusu mahusiano, lakini kwa hili limenishinda kulitatua.
Ndugu zangu nasumbuliwa na wivu. Wivu ndio unaonisumbua na kunitesa. Nikimpigia mpenzi wangu na kukuta simu yake inatumika basi kwangu mimi ni ugomvi. Hata kama mpenzi wangu ameachana na X wake tena kabla hata yangu miye. Akinihadithia naumia utafikiri bado wapo kwenye mahusiano.
Suala kama hili limenipa matatizo makubwa sana. Niliachana na kugombana na Wapenzi wangu waliopita sababu ya hili. Hata huyu wa sasa sina imani kama tutafika. Nampenda na sihitaji kumuacha ama kumpoteza. Kuna wakati nakasirika na kutaka kufanya maamuzi ya kuachana na mpenzi wangu lakini baadae napuuza nakujiona kuwa mimi ni mpuuzi.
Kabla sijampoteza huyu niliyenae naomba ushauri wenu. Ni vipi naweza kujiondoa katika hili? Je ni kipi nifanye ili nisimpoteze huyu mpenzi wangu? Kuna kipindi nakasirika sana na kutaka kuamua lolote. Lakini mapenzi yangu kwake ni makubwa sana. Siwezi kumuacha. Hata mama yangu hataki nimuache huyu mwanamke.
NAOMBA MNISHAURI NI NINI NIKIFANYE ILI HILI LISINITOKEE?
NAOMBA MSAADA.
Kulikoni kufufua huu uzi,!!??? Muhusika alishafarikiAisee wivu ni kwamba dhahiri humuamini mpenzi wako. Na ukimuoa ndo utazidi maradufu. Kwanza ondoa mawazo mabaya juu yake na kama ana zuri moja na mengine mabaya 9 basi upe kazi ya kuwaza hilo zuri moja na lipe kipaumbele na kusahau mengine.
Sent using Jamii Forums mobile app
Alisjafariki huyu mleta uzi.Kuwa na zaidi ya mmoja itakusaidia namaanisha backup
Mzee mbona umefukua kaburi la marehemu?